Yesu sio Mungu

Hiyo MUNGU alitaka kuja Duniani aongee na watu wake umeitoa wapi?
 
Nani aliye fufuka mwenyewe na aliyesema atafufuka kwa muda flani baads ya kifo chake ili isiwe bahati au uzushi wake ?
Yesu kufa na kufufuka ilikua inajulika na aliwaambia wanafunzi wake sio jambo la bahati mbaya, pili wapo wengi waliofufuka Eliya na Elisha walifufua pia wafu, Kwauwezo wa MUNGU hakuna linaloshindikana hvo hoja yako ya kufa na kufufuka sio kigezo cha kusema Yesu ni MUNGU
 
Nasema hivi mtu akija na hoja yeye mashiko kuwa Yesu ni mungu nampa laki 1 niliiweka kwenye kibubu kwa zaidi ya miezi mitatu, ntakupa akiba yangu yote.

Uje umekula mambo ya matusi, sijui roho mtakatifu usiyalete hapa leta hoja nzito

Arianism
Arianism ni nini?
 
Kwanini unazani yesu sio mungu ili tuanze kujadili kwenye upande huo ? unajua mimi bado najifunza kama umegundua kitu kipya kiseme hapa
 
Nasema hivi mtu akija na hoja yeye mashiko kuwa Yesu ni mungu nampa laki 1 niliiweka kwenye kibubu kwa zaidi ya miezi mitatu, ntakupa akiba yangu yote.

Uje umekula mambo ya matusi, sijui roho mtakatifu usiyalete hapa leta hoja nzito

Arianism
Uzuri huko mbinguni kila mtu atawajibika peke yake. Wanaoamini acha waamini na wewe usiyeamini baki na imani yako hiyo hiyo.
 
Mitume hawakuwa makamanda wa jeshi lolote au hawakuwa wapiganaji au mafunzo ya upanga wengi walikuwa wavuvi na watu wa kawaida nani alikuwa mpiganaji kwenye mitume ?
Mitume Gani kwanza unaowaongelea wa Yesu au wa MUNGU kama Mussa, Daudi, Yoshua,Suleiman, Ibrahim wote walipgana vita
 
Kwa nini hukuuliza pia kufufuka?
Ungeleta kwanza sifa za mwenyezi mungu according to biblia tuone kama Kuna sifa ya mungu kufa na kufufuka.

Ukiniuliza vipi kuhusu kufufuka kwake ntakujibu kuwa ni mungu ndio alimfufua
 
Musa na daudi na youshua hawakuwa mitume bali manabii

niambie nini maana ya nabii

na nini maana ya mitume
Sikilza ww Mimi sio mjinga Kwa wakristo mitume niwale wanafunzi wa Yesu na wanaosambaza injili hili nalijua

Kwa mantiki hiyo basi usingesema mtume Muhammad angesema nabii Muhammad Toka ulivoanza maana Muhammad hakua mwanafunz wa Yesu wala msambaza habari za Yesu
 
Nini maana ya mitume

na nini maana ya nabii

msaada tafadhali hebu tuongee kama marafiki tu
 
Ungeleta kwanza sifa za mwenyezi mungu according to biblia tuone kama Kuna sifa ya mungu kufa na kufufuka.

Ukiniuliza vipi kuhusu kufufuka kwake ntakujibu kuwa ni mungu ndio alimfufua
Ulizonazo wewe ni zipi?
 
Wewe unaamini yesu ni mungu lakini bado umepungukiwa unachanganya roho mtakatifu na mungu baba bado hujui muundo huu utakuwa vipi, kwahiyo hoja yako wewe hapa nikumtambua yesu kama mungu huko pengine unapotosha
Mimi naongea kwa maandiko na Aya:
Sitaki waropokaji kuni nukuu na kuongea pumba zao:
Siku nyingine ukitaka kuongea na mimi ongea kwa Aya
 
Mtoa mada ili kupata majibu ya swali lako inabidi tujiulize haya maswali matatu
1. Yesu Kabla Hajaja Duniani: Alikuwa nani?
2. Yesu Akiwa Duniani: Alikuwa Nani? na Alikuwa na Uwezo Gani?
3. Baada ya Yesu kufa na kufufuka alienda wapi
4. utofauti wa yesu na Wanadamu Wengine na viumbe wengine.

Twende sasa

1. Yesu Kabla Hajaja Duniani: Alikuwa nani?
Kabla ya kuja duniani, Yesu alikuwa Neno wa Mungu, ambaye alikuwa na Mungu na alikuwa Mungu mwenyewe. Hili linathibitishwa na Yohana 1:1, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwa kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.” Yesu hakuanza kuwepo alipofanyika mwili, bali aliishi milele akiwa na Baba. Katika Wakolosai 1:16 tunafundishwa kuwa kwa yeye vitu vyote viliumbwa, vya mbinguni na vya duniani – hii inaonyesha kuwa Yesu ni Muumba na si kiumbe. Kwa hiyo, kabla ya kuzaliwa duniani, Yesu alikuwa na uungu kamili, mamlaka ya kiungu, na alishiriki utukufu na Baba tangu milele (Yohana 17:5).

2. Yesu Akiwa Duniani: Alikuwa Nani? na Alikuwa na Uwezo Gani?
Yesu alipokuja duniani, alichukua mwili wa kibinadamu lakini hakuwacha uungu wake. Alikuwa na asili mbili kwa pamoja: Mungu na mwanadamu. Wafilipi 2:5–8 inaeleza kuwa, ingawa alikuwa sawa na Mungu, alijinyenyekeza akajifanya kuwa mtumishi na akawa kama wanadamu. Akiwa duniani, Yesu alionyesha uwezo wa kiungu: alisamehe dhambi (Marko 2:5), alijua mawazo ya watu (Mathayo 9:4), alituliza dhoruba kwa neno moja (Mathayo 8:26), na alifufua wafu kama Lazaro (Yohana 11). Mambo haya hayawezi kufanywa na mwanadamu wa kawaida; ni sifa za Mungu pekee. Hii inathibitisha kuwa hata akiwa duniani, Yesu alikuwa Mungu kwa uwezo na mamlaka.

3. Baada ya Yesu kufa na kufufuka alienda wapi
Baada ya Yesu kufa msalabani na kufufuka, hakurudi tu mbinguni bali alirudia utukufu wake wa awali akiwa sasa na mwili wa utukufu. Wafilipi 2:9–11 inasema kuwa Mungu alimwadhimisha sana na kumpa jina lipitalo kila jina, na kwamba kila goti lipigwe na kila ulimi ukiri kuwa Yesu ni Bwana. Hii inaonyesha kuwa Yesu alirudi katika hali yake ya Uungu wa milele akiwa na mamlaka juu ya kila kitu. Biblia pia inamwonyesha Yesu kama anayeketi katika mkono wa kuume wa Mungu (Waebrania 1:3), akifanya kazi kama Kuhani Mkuu na Mwombezi wetu mbinguni.

4. utofauti wa yesu na Wanadamu Wengine na viumbe wengine.
Yesu Kristo ni wa kipekee kabisa kati ya wanadamu wote waliowahi kuishi. Tofauti kuu ni kwamba Yesu hakuwa na dhambi hata siku moja. Watu wote wanakosea, lakini Biblia inasema wazi kwamba Yesu hakutenda dhambi wala hakuwa na hila yoyote (1 Petro 2:22). Hii inamfanya Yesu awe mtakatifu kabisa, tofauti na wanadamu wengine ambao wanahitaji wokovu na msamaha wa dhambi.

Zaidi ya hayo, Yesu si tu mwana wa Mungu kwa njia ya imani, bali ni Mwana wa Mungu kwa asili ya milele. Hii inamaanisha Yesu hakuzaliwa tu kama binadamu, bali alikuwa na asili ya kiungu tangu milele (Yohana 3:16). Wanadamu wote ni watoto wa Mungu kwa imani, lakini Yesu ni wa pekee katika hii hali, akiwa na uhusiano wa kipekee na Baba yake mbinguni.

Tofauti nyingine kubwa ni kwamba Yesu si kiumbe kama malaika au mwanadamu wa kawaida, bali ni Muumba wa vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani. Biblia inasema kwa Yesu vitu vyote viliumbwa, ikiwa ni viti vya enzi, mamlaka, na viumbe vyote (Wakolosai 1:16-17). Hii inaonyesha kuwa Yesu ni chanzo cha maisha na nguvu zote, tofauti kabisa na viumbe aliyeumba.

Pia, Yesu ana mamlaka ya kiungu ambayo hakuna mwanadamu au kiumbe mwingine anayeweza kuipata. Alisamehe dhambi, jambo ambalo ni haki ya Mungu peke yake (Marko 2:5-7), alipokea ibada kutoka kwa wafuasi wake (Mathayo 14:33), na alishinda mauti kwa kufufuka kwake, akawa hai milele (Ufunuo 1:18). Kwa hivyo, Yesu ni wa kipekee katika kila upande — mtakatifu, Mwana wa Mungu, Muumba wa viumbe vyote, na Mwenye mamlaka ya milele.

Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…