Yesu sio Mungu

Yesu sio Mungu

Kama imani ni kusadiki mambo yasiyothibitishika, waamini hamna haja ya kuthibitishiana chochote kwa kuwa wote mnaamini tu mambo ya kusadikika.
Kila mmoja aendelee kuamini simulizi za za kitoto za mzungu au mwarabu kwa kujinafasi.
 
Sasa ndio naelewa kuwa wewe huna elimu yoyote na sio unajua unachokiongea asante sana
Nimekujibu Kwa upande wa wakristo mitume ni wanafunzi wa Yesu na wengine wasambaza injili manabii ni walotumwa na MUNGU sio wafuasi wa Yesu wala wanafunzi

Sasa hapo ujaelewa nini na hii mada inahusu wakristo na Yesu
 
Mtoa mada ili kupata majibu ya swali lako inabidi tujiulize haya maswali matatu
1. Yesu Kabla Hajaja Duniani: Alikuwa nani?
2. Yesu Akiwa Duniani: Alikuwa Nani? na Alikuwa na Uwezo Gani?
3. Baada ya Yesu kufa na kufufuka alienda wapi
4. utofauti wa yesu na Wanadamu Wengine na viumbe wengine.

Twende sasa

1. Yesu Kabla Hajaja Duniani: Alikuwa nani?
Kabla ya kuja duniani, Yesu alikuwa Neno wa Mungu, ambaye alikuwa na Mungu na alikuwa Mungu mwenyewe. Hili linathibitishwa na Yohana 1:1, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwa kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.” Yesu hakuanza kuwepo alipofanyika mwili, bali aliishi milele akiwa na Baba. Katika Wakolosai 1:16 tunafundishwa kuwa kwa yeye vitu vyote viliumbwa, vya mbinguni na vya duniani – hii inaonyesha kuwa Yesu ni Muumba na si kiumbe. Kwa hiyo, kabla ya kuzaliwa duniani, Yesu alikuwa na uungu kamili, mamlaka ya kiungu, na alishiriki utukufu na Baba tangu milele (Yohana 17:5).

2. Yesu Akiwa Duniani: Alikuwa Nani? na Alikuwa na Uwezo Gani?
Yesu alipokuja duniani, alichukua mwili wa kibinadamu lakini hakuwacha uungu wake. Alikuwa na asili mbili kwa pamoja: Mungu na mwanadamu. Wafilipi 2:5–8 inaeleza kuwa, ingawa alikuwa sawa na Mungu, alijinyenyekeza akajifanya kuwa mtumishi na akawa kama wanadamu. Akiwa duniani, Yesu alionyesha uwezo wa kiungu: alisamehe dhambi (Marko 2:5), alijua mawazo ya watu (Mathayo 9:4), alituliza dhoruba kwa neno moja (Mathayo 8:26), na alifufua wafu kama Lazaro (Yohana 11). Mambo haya hayawezi kufanywa na mwanadamu wa kawaida; ni sifa za Mungu pekee. Hii inathibitisha kuwa hata akiwa duniani, Yesu alikuwa Mungu kwa uwezo na mamlaka.

3. Baada ya Yesu kufa na kufufuka alienda wapi
Baada ya Yesu kufa msalabani na kufufuka, hakurudi tu mbinguni bali alirudia utukufu wake wa awali akiwa sasa na mwili wa utukufu. Wafilipi 2:9–11 inasema kuwa Mungu alimwadhimisha sana na kumpa jina lipitalo kila jina, na kwamba kila goti lipigwe na kila ulimi ukiri kuwa Yesu ni Bwana. Hii inaonyesha kuwa Yesu alirudi katika hali yake ya Uungu wa milele akiwa na mamlaka juu ya kila kitu. Biblia pia inamwonyesha Yesu kama anayeketi katika mkono wa kuume wa Mungu (Waebrania 1:3), akifanya kazi kama Kuhani Mkuu na Mwombezi wetu mbinguni.

4. utofauti wa yesu na Wanadamu Wengine na viumbe wengine.
Yesu Kristo ni wa kipekee kabisa kati ya wanadamu wote waliowahi kuishi. Tofauti kuu ni kwamba Yesu hakuwa na dhambi hata siku moja. Watu wote wanakosea, lakini Biblia inasema wazi kwamba Yesu hakutenda dhambi wala hakuwa na hila yoyote (1 Petro 2:22). Hii inamfanya Yesu awe mtakatifu kabisa, tofauti na wanadamu wengine ambao wanahitaji wokovu na msamaha wa dhambi.

Zaidi ya hayo, Yesu si tu mwana wa Mungu kwa njia ya imani, bali ni Mwana wa Mungu kwa asili ya milele. Hii inamaanisha Yesu hakuzaliwa tu kama binadamu, bali alikuwa na asili ya kiungu tangu milele (Yohana 3:16). Wanadamu wote ni watoto wa Mungu kwa imani, lakini Yesu ni wa pekee katika hii hali, akiwa na uhusiano wa kipekee na Baba yake mbinguni.

Tofauti nyingine kubwa ni kwamba Yesu si kiumbe kama malaika au mwanadamu wa kawaida, bali ni Muumba wa vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani. Biblia inasema kwa Yesu vitu vyote viliumbwa, ikiwa ni viti vya enzi, mamlaka, na viumbe vyote (Wakolosai 1:16-17). Hii inaonyesha kuwa Yesu ni chanzo cha maisha na nguvu zote, tofauti kabisa na viumbe aliyeumba.

Pia, Yesu ana mamlaka ya kiungu ambayo hakuna mwanadamu au kiumbe mwingine anayeweza kuipata. Alisamehe dhambi, jambo ambalo ni haki ya Mungu peke yake (Marko 2:5-7), alipokea ibada kutoka kwa wafuasi wake (Mathayo 14:33), na alishinda mauti kwa kufufuka kwake, akawa hai milele (Ufunuo 1:18). Kwa hivyo, Yesu ni wa kipekee katika kila upande — mtakatifu, Mwana wa Mungu, Muumba wa viumbe vyote, na Mwenye mamlaka ya milele.

Asante
Muendelezo.
Utatu Mtakatifu na Umungu wa Yesu

Utatu Mtakatifu unafundisha kuwa kuna Mungu mmoja tu, lakini Mungu huyu huonekana katika nafsi tatu tofauti: Baba, Mwana (Yesu Kristo), na Roho Mtakatifu. Kila nafsi ni Mungu kamili, mwenye asili ya kiungu, nguvu, na utukufu sawa, lakini si watu watatu tofauti, bali ni nafsi tatu katika Mungu mmoja.

Katika muktadha huu, Yesu ana asili ya kiungu na ni Mungu, lakini si Baba; ni nafsi ya pili ya Utatu. Roho Mtakatifu pia ni Mungu, nafsi ya tatu. Hii inaonyesha uwamoja na usawa wa kiungu kati ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, ingawa kila mmoja ana kazi zake tofauti katika mpango wa wokovu.

Kwa hiyo, Yesu ni Mungu kwa asili, si kiumbe wala malaika, bali sehemu ya Utatu Mtakatifu – Mungu mmoja, nafsi tatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu), wote wakiwa Mungu mmoja kwa uungu na mamlaka.
 
Sijawahi ona uchawi katika maisha yangu. Kwanini umeuliza hivyo mkuu😆
Mkuu ngoja nikuonesha sehemu ya kuona uchawi Kuna vipindi vya america live talent show search YouTube utaona uchawi live
 
Nimekujibu Kwa upande wa wakristo mitume ni wanafunzi wa Yesu na wengine wasambaza injili manabii ni walotumwa na MUNGU sio wafuasi wa Yesu wala wanafunzi

Sasa hapo ujaelewa nini na hii mada inahusu wakristo na Yesu
Kusema mitume ni wanafunzi wa yesu hii sio maana ya mitume mkuu ?

pengine tukijua maana ya mitume

na nini maana ya nabii kidogo tutaweza kuelewana tatizo hujui hivi vitu ni nini ?
 
Muendelezo.
Utatu Mtakatifu na Umungu wa Yesu

Utatu Mtakatifu unafundisha kuwa kuna Mungu mmoja tu, lakini Mungu huyu huonekana katika nafsi tatu tofauti: Baba, Mwana (Yesu Kristo), na Roho Mtakatifu. Kila nafsi ni Mungu kamili, mwenye asili ya kiungu, nguvu, na utukufu sawa, lakini si watu watatu tofauti, bali ni nafsi tatu katika Mungu mmoja.

Katika muktadha huu, Yesu ana asili ya kiungu na ni Mungu, lakini si Baba; ni nafsi ya pili ya Utatu. Roho Mtakatifu pia ni Mungu, nafsi ya tatu. Hii inaonyesha uwamoja na usawa wa kiungu kati ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, ingawa kila mmoja ana kazi zake tofauti katika mpango wa wokovu.

Kwa hiyo, Yesu ni Mungu kwa asili, si kiumbe wala malaika, bali sehemu ya Utatu Mtakatifu – Mungu mmoja, nafsi tatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu), wote wakiwa Mungu mmoja kwa uungu na mamlaka.
Haya maelezo alitoa Yesu mwenyw au katika kikao Cha nicaea miaka miatatu baada ya Yesu kupazwa?
 
Nipe hiyo Aya anayosema MUNGU alitaka kuja kuongea nasisi Duniani ndo akaja kama binadamu
Wewe umeweka Aya ipi ?

Mika 1:1
Hili ndilo neno la Bwana lililomjia Mika, Mmorashti, katika siku za Yothamu, na Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda; maono aliyoyaona katika habari za Samaria, na Yerusalemu.

2 Sikilizeni, enyi watu wa kabila zote; sikiliza, Ee dunia, na vyote vilivyomo; Bwana MUNGU na ashuhudie juu yenu, yeye Bwana kutoka hekalu lake takatifu.

3 Kwa maana, angalieni, Bwana anakuja akitoka mahali pake, naye atashuka, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka.

4 Na hiyo milima itayeyuka chini yake, nayo mabonde yatapasuliwa, kama vile nta iliyo mbele ya moto, kama maji yaliyomwagika tena kutelemka gengeni.
..........
Ninaposema Mungu simaanishi kiumbe Allah:
Ukimuwaza kiumbe Allah huwezi kuelewa andiko la Nabii Mika hapo Juu
Allah is a Satan:
 
Kusema mitume ni wanafunzi wa yesu hii sio maana ya mitume mkuu ?

pengine tukijua maana ya mitume

na nini maana ya nabii kidogo tutaweza kuelewana tatizo hujui hivi vitu ni nini ?
Kwa dini ipi? Kwa ukristo nipo sahihi Kwa uislamu nimekosea nakubali, lkn hapa tunaongea kuhusu ukristo hivo jifunze tena
 
Mkuu ngoja nikuonesha sehemu ya kuona uchawi Kuna vipindi vya america live talent show search YouTube utaona uchawi live
Mi wala sitaki kuona uchawi wala sitaki kuufatilia. Sijawahi kuogopa uchawi kwasababu siujui
 
Ulizonazo wewe ni zipi?
-Mungu hanyi mavi
-Hali mikate na hajawahi kusikia njaa
-Hajawahi kuzaliwa
-Mungu hajawahi kujamba mifuzi
-Mungu hawezi kuteswa na kidhalilishwa, kuchapwa fimbo na kiumbe alichokiumba yeye mwenyewe.
-Mungu hafi hata Kwa sekunde na kwa sababu hiyo basi hata kufufuka hawezi
 
-Mungu hanyi mavi
-Hali mikate na hajawahi kusikia njaa
-Hajawahi kuzaliwa
-Mungu hajawahi kujamba mifuzi
-Mungu hawezi kuteswa na kidhalilishwa, kuchapwa fimbo na kiumbe alichokiumba yeye mwenyewe.
-Mungu hafi hata Kwa sekunde na kwa sababu hiyo basi hata kufufuka hawezi
Mungu anaweza au hawezi kufanya jambo fulani?
 
Wewe umeweka Aya ipi ?

Mika 1:1
Hili ndilo neno la Bwana lililomjia Mika, Mmorashti, katika siku za Yothamu, na Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda; maono aliyoyaona katika habari za Samaria, na Yerusalemu.

2 Sikilizeni, enyi watu wa kabila zote; sikiliza, Ee dunia, na vyote vilivyomo; Bwana MUNGU na ashuhudie juu yenu, yeye Bwana kutoka hekalu lake takatifu.

3 Kwa maana, angalieni, Bwana anakuja akitoka mahali pake, naye atashuka, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka.

4 Na hiyo milima itayeyuka chini yake, nayo mabonde yatapasuliwa, kama vile nta iliyo mbele ya moto, kama maji yaliyomwagika tena kutelemka gengeni.
..........
Ninaposema Mungu simaanishi kiumbe Allah:
Ukimuwaza kiumbe Allah huwezi kuelewa andiko la Nabii Mika hapo Juu
Allah is a Satan:
Wewe hauko timamu kwahyo hizo Aya ndo zilikua zinatabiri ujio wa Yesu au?
 
Rafiki, Yesu ni Mungu kamili na ni mwansdamu kamili; asili mbili ndani ya mmoja. Kuhusu Uungu wa Yesu nitakupa ushahidi wa namna mbili moja ni uzoefu wangu na ya pili ni kimaandiko.
1. Yesu ni Mungu mana anafanya mambo ambayo mwansdamu hawezi kufanya:
a) ameniokoa dhambini (kwa jina lake Nina ushindi dhidi ya dhambi)
b) amenipa Amani, furaha na Upendo ambayo sikuwahi kupata kabla sijamjua
c) amenijaza Roho wake, it is quiet and amazing experience
2. Yesu you hai Leo na anajidhihirisha kwangu ref. Yoh. 14:22

SASA USHAHIDI WA KIMAANDIKO
Ushahidi wa Kimaandiko Kuwa Yesu ni Mungu
Biblia inatoa ushahidi mwingi unaoashiria kwamba Yesu ni Mungu. Zifuatazo ni baadhi ya dondoo muhimu za kimaandiko zinazoelezea uhusiano huu:
Madai ya Yesu Mwenyewe Kuhusu Uungu Wake
Yesu mara kadhaa alijitambulisha kwa njia zilizowazi na zisizo wazi kuwa Yeye ni Mungu, au kuwa na mamlaka na sifa za Kimungu:
* "Mimi na Baba tu umoja" (Yohana 10:30): Kauli hii ilielezwa kuwa ni kashfa na Wayahudi, kwani walielewa wazi kuwa Yesu alikuwa akijifananisha na Mungu.
* "Mimi Ndimi Njia, Kweli na Uzima; mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi" (Yohana 14:6): Hii inaonyesha mamlaka ya kipekee ya Yesu katika uhusiano na Mungu Baba, na kwamba hakuna anayeweza kumkaribia Mungu isipokuwa kupitia Yeye.
* "Kabla Abrahamu hajakuwapo, mimi niko" (Yohana 8:58): Hapa Yesu anatumia jina la Mungu lililotumika katika Agano la Kale, "Mimi NIKO" (Kutoka 3:14), akijifananisha na Mungu asiye na mwanzo wala mwisho. Hili pia liliwachukiza sana Wayahudi na walitaka kumpiga mawe.
* Kusamehe Dhambi (Marko 2:5-7): Yesu alidai uwezo wa kusamehe dhambi, jambo ambalo Wayahudi waliamini linaweza kufanywa na Mungu pekee.
Madai ya Waandishi wa Biblia Kuhusu Uungu wa Yesu
Waandishi mbalimbali wa Biblia walimtambua Yesu kama Mungu:
* Yohana 1:1-3, 14: "Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu... Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli." Hapa Yohana anamwita Yesu "Neno" na anasema "Neno alikuwa Mungu" na kisha anathibitisha kuwa "Neno alifanyika mwili," akimaanisha Yesu.
* Wafilipi 2:5-8: Paulo anaeleza kuwa Yesu, "aliyekuwa na namna ya Mungu, hakuhesabu kuwa kunyakua kuwa sawa na Mungu, bali alijifunua mwenyewe, akatwaa namna ya mtumwa." Hii inaonyesha kwamba Yesu alikuwa Mungu tangu mwanzo.
* Wakolosai 1:15-17: "Yeye ndiye mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote; kwa maana kwa yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo duniani, vinavyoonekana na visivyoonekana, ikiwa ni viti vya enzi au enzi au falme au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa yeye na kwa ajili yake." Hapa, Paulo anamwonyesha Yesu kama Muumbaji wa vitu vyote, sifa ambayo ni ya Mungu pekee.
* Waebrania 1:8: "Bali kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Ee Mungu, ni cha milele na milele; Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya uadilifu." Mwandishi wa Waebrania anamwita Yesu waziwazi "Mungu."
* Tito 2:13: "tukitarajia tumaini lenye baraka, yaani, kujidhihirisha kwa utukufu wa Mungu wetu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo." Paulo anamwita Yesu "Mungu wetu mkuu na Mwokozi wetu."
* Isaya 9:6 (Unabii wa Agano la Kale): "Maana mtoto amezaliwa kwa ajili yetu, tumepatiwa mtoto mwanamume; na ufalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa jina lake Mshauri wa Ajabu, Mungu mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani." Unabii huu, ambao kwa ujumla unaaminika kumhusu Yesu, unampa majina yanayoelezea uungu wake.
Miujiza na Mamlaka ya Kimungu ya Yesu
Yesu alifanya miujiza na kudhihirisha mamlaka ambayo yanaweza kutokea kwa Mungu pekee:
* Kutuliza Dhoruba (Marko 4:35-41): Yesu alituliza dhoruba kali kwa amri yake, akionyesha mamlaka juu ya asili.
* Kufufua Wafu (Yohana 11:43-44, Luka 7:11-17): Yesu alifufua watu kutoka kwa wafu, ikiwemo Lazaro, binti ya Yairo, na mwana wa mjane wa Naini.
* Kuzidisha Chakula (Marko 6:30-44): Alilisha maelfu ya watu kwa chakula kidogo tu, akionyesha mamlaka ya kimuujiza juu ya ugavi.
* Kukubali Ibada (Mathayo 28:17, Luka 24:52): Baada ya kufufuka kwake, wanafunzi walimwabudu Yesu, na Yeye hakukataa ibada hiyo. Katika Biblia, ibada inapaswa kutolewa kwa Mungu pekee.

Huu ni muhtasari wa baadhi ya ushahidi wa kimaandiko unaoelezea kuwa Yesu ni Mungu.
Porojo tupu,, hayo yote ni maneno ya watu ambao wengine hata hawakumdiriki Yesu mwenyewe

Kalamu za waandishi zinawaingiza mkenge wakristo, hawajui kutofautisha ni yepi Maneno ya YESU na ni yepi maneno ya waandishi.

Kwani mtu akisema mimi na Rais wangu ni wa moja? Hii inaamaanisha kuwa yeye pia ni Rais na ana mamlaka ya Urais?

Au Yesu aliposema mimi ni ndimi njia ya ukweli na uzima ....Ndio inamaanisha kuwa yeye ni Mungu?
Kwanini isitafsirike kuwa yeye kapewa muongozo na utume kutoka kwa Mungu ili awaongoze Wana Israel katika njia ya sawasawa?

Hivi haya maneno mnayaweka katika mizani gani? Mbona mnatumia matamanio ya nafsi zenu ili kupotoa?


Na kuhusu jambo la kufa na kufufuka kwa YESU ni story ya kubuni tu kutoka kwa wapagani Haina ushahidi wowote kielimu.

Et YESU awe Mungu alafu atumie maneno ya kimafumbo kujificha ili watu wasimfahamu kwa kuhofia kupingwa au kuuliwa ni Mungu gani huyo mwenye udhaifu namna hiyo?? Subhanallah!!!

Ikiwa mitume hawakuweza kuficha utume wao kwa Kaumu zao na wao ni wanaadamu hawakuweza kufanya hivyo, je kwa Mungu mwenye madaraka yote, muumbaji, mteza nguvu, anafanya atakalo bila ya kuhukumiwa, mwanzilishi wa maisha, anaefisha , anaehuwisha itawezekanaje?

Wakristo tumieni akili mbona mnakuwa mambumbumbu kwa vitu vidogo kama hivi?

Na ndio maana mkaihujumu injili ya Barnabas kwa kuingiza hekaya zenu za uzushi kama hivi.

Kuingiza imani ya utatu mtakatifu ikiwa YESU mwenyewe hakuanzisha Wala haitambui.
Kama YESU Kaianzisha lete ushahidi wa kielimu!!

Nimalizie tu ukifa katika ukristo juwa wewe unaenda motoni milele bila ya shaka yoyote.
 
Mungu anaweza au hawezi kufanya jambo fulani?
Mungu Allah huwa hawezi mambo mengi tu:
Unaposema Mungu lazima umtaje jina lake ili watu wafahamu hivyo.
Alicho fanikiwa Allah ni kuwashawishi baadhi ya watu kuimba kila siku.
Munguuuu Mkubwaaa
Yaani Allahhh Akbarrrr
 
MUNGU sio jina ni cheo ie. Muumbaji. Kitabu cha Kutoka wakati Mungu anaongea na Musa kwenda kwa farao Mungu alimwambia Musa
Kutoka 3
13. Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n’nani? Niwaambie nini?
14. Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO;<br> akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO<br> amenituma kwenu.
Kwa hoja hii neno Mungu sio jina bali ni cheo ambacho hata miungu ya Misri ilikuwa nayo Musa anataka jina la Mungu na Mungu anajifunua jina lake kuwa hapo kama "NIKO AMBAYE NIKO".
Yohana 8
54. Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu.
55. Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika.
56. Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.
57. Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu?
58. Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.

Kumbe wayahudi walimwita Mungu wasiyemjua Yesu anawaambia yeye anamjua hivyo wamuulize atawaambia kuhusu huyo Mungu. Ni mfano na umeenda ofisini ile uko nje unamuulizia boss wa ofisi na uliyemkuta nje ndio yeye Ila hajajifunua maana hayuko na hujamkuta ofisini akaanza kukuuliza una shida gani wewe unang'anana kutaka kuongea na boss huku unatoa maneno ya kashfa anakuambia ukiniona Mimi umemuona boss wewe unang'ang'ana kutaka kumwona boss kumbe ni yeye Ila anaku enjoy tu Mara anakufukuza kisha anakuja mtu kukutonya kuwa huyo ndio boss sijui utafanyaje maana ulidhani boss at a kuwa kwenye suit Kali, kiatu kikali, yuko ofisini wakati wote, hachangamani na kuwa na ukaribu na watu n.k

Wafilipi 2
5. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
6. ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
7. bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
8. tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
9. Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
10. ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
11. na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Anaposema kwa hiyo Mungu akamkilimia jina inamaanisha Mungu (ofisi) ikamkamkilimia. Mungu ni ofisi tu na sio kitu chochote mnachofikilia

Yohana 1
18. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.
Sasa wewe uliyemuona Mungu said Yesu mfunue hapa huyo mungu tumuone.

Kibinafsi nasema Yesu ni Mungu kwa sababu anajua alipitia magumu yote katika mwili akashinda hivyo anajua udhaifu wangu vizuri. Sasa huyo Mungu wako asiyejua njaa, majaribu ya wanawake, ukata n. K simtaki maana ni mungu mjinga na muoga asiyejua hustle tunazopitia wanadamu yeye akae huko alike Sisi tunabanana na Mungu na Bwana wetu Yesu Kristo mfufuka mpaka atufukishe mbinguni. Amen.
 
Back
Top Bottom