Daima naamini ndoa ni ngumu, mtu asikudanganye kwamba ooh mkiwa wavumilivu, ooh ukioa bikra mara ooh mpende sana mkeo atatulia, changamoto zipo ni wewe kujua tu nitawezaje kuzikabili maana. Taa inayomulika vizuri utaijua kukiwa na giza sio kukiwa na mwanga, hata mke bora utamjua kwenye changamoto. Kukataa ndoa kupo hatukati ilimradi kuna vitu vinafanya tukatae ndoa, vitu hivyo lazima ujue kuvikabili ili uikubali ndoa.
Ndoa ni agano, kuna wakati najiuliza kwanini MUNGU hakuacha duniani tuwe wanaume tu kwanini akaumba wanawake akasema tuzae nao tuijaze dunia.