wewe party yako itakuwa ni mitama!lazima nirudi hapa ni kama nyumbani, hata mwana mpotevu alichukua mgao wake kwa majivuno akasepa yalipomkuta majanga alirudi and guess what akapokelewa kwa bonge moja la party
Mh! mimi nitakuwa mvunjifu wa amani tu!😀 😀 😀 mkuu uwepo wako ndio mafanikio ya sherehe hio
halafu anakuja mtu mithiri ya dr janabi...🤣Hilo halina tatizo cha muhimu uhudhurie, nikikamata mic nasema "naomba kutambua uwepo wa boss wa maboss tajiri papaa mipesa mobimba Kenzy"
Kataa ndoa, ndoa ni Shimo la tewa lenye joka la mdimu ndani yake.Kwa kipindi fulani nimekua siamini katika suala la kuunganishwa watu wawili waliokutana ukubwani kisha kuwe na utulivu baina yao, kuwe na furaha, amani na upendo wa dhati baina yao, niliamini jambo kama hilo linahitaji muda mrefu sana angalau miaka mitano ndipo rasmi waunganishwe kuepusha mitafaruku.
Niliamini kuwa katika muunganiko huo kabla ni hatari sana, maana wakati wowote mwenzangu anaweza kubadilika akadai kila mtu ashike hamsini zake.
Nilijenga dhana kuwa "dah yani kila siku niwe naamka pembeni ya limtu ambalo lazima nihustle kulihudumia aah usinitanie" na wakati nimetoka litakuwa linanicheat na kuleta mabwana ndani hapana! hapana!...
Niliamini muunganiko huu unamnufaisha zaidi mwenzangu kuliko mimi, lakini kumbe sivyo nilikuwa najiua nilikufa kiimani nikazikwa nafsi nikawa mfu anaetembea kimahusiano, nikawa naabudu lakini sielewi nachoabudu...
Kwa nini wakatoliki wana vitabu 72 huku madhehebu mengine yakiwa na vitabu 66 kibindoni.Mpaka sasa utakuwa unajiuliza huyu anazungumzia nini, nazungumzia mahusiano ya kiroho baina yangu na kristo na mahusiano kimapenzi kati yangu na mwanadamu (mwanamke).
Kiimani mimi naamini katika ukristo(naamini), Yesu kristo alikufa kwaajili ya dhambi zetu dhambi hizo ni nyingi sana kiasi kwamba wenyewe tusingeweza kuzifidia hata kwa sadaka za malori ya wanyama.
Wizi,uongo,ibada za sanamu, na uzinzi, kwa leo nitaongelea uzinzi na unavyoletwa na kataa ndoa.
Katika 1 Wak 7:1 na kuendelea imeandikwa mwanaume akae katika hali ile ile yaani asioe, lakini kwa sababu ya tamaa na kuepuka uzinzi mwanaume awe na mwanamke wake mwenyewe.
Uzinzi ni mbaya sana, umekemewa mara nyingi nyingi, kwenye amri kumi, usizini. Kwenye 1 Wak 6 ikimbie zinaa maana dhambi zote ni nje ya mwili, sasa kwa muda mrefu...
Kuna binti amekuwa akinipenda sana amefikia hatua ya kulia sana kwa sababu nilimwambia siwezi kumuoa sina mpango wa kuoa, wakati huohuo nawaka tamaa nifanye ngono, nilikufa katika uzinzi wa roho wa team kataa ndoa...
Yes, hii ni kauli ya kijana anayeelekea kukomaa kiakili.Ndege Sikupingi nachoamini kuoa ni maamuzi personal na kila mtu ataamua kwa wakati wake kwa sasa nimeamua kuwa kataa ndoa mpaka hapo nitakapoachia uanachama 2028
Never put in one post things you can put in two.Ngoja Kiranga aje ili umuelekeze hiyo historia ya ukristo vizuri, maana nili Soma kitabu fulani Nika ona ni janja janja tu.
Kila mtu ana muda wake mkuu hata mimi huwa nasemaga kuna jamaa mda mwingi huwa anakuja pm kunipa angalizo na nyuz zangu ila jibu langu kubwa ni kuwa mimi na maisha yangu ujui napitia nn huku 😂😂😂😂😂Nishawahi kusema kila mtu atachanganyikiwa kwa wakati wake, mkuu humu tupo kuhave fun tu ila maisha yetu halisi tunayajua wenyewe ID zinaficha mengi, kwa sababu fulani fulani unajikuta unaandika ujingaujinga haha
Daima naamini ndoa ni ngumu, mtu asikudanganye kwamba ooh mkiwa wavumilivu, ooh ukioa bikra mara ooh mpende sana mkeo atatulia, changamoto zipo ni wewe kujua tu nitawezaje kuzikabili maana. Taa inayomulika vizuri utaijua kukiwa na giza sio kukiwa na mwanga, hata mke bora utamjua kwenye changamoto. Kukataa ndoa kupo hatukati ilimradi kuna vitu vinafanya tukatae ndoa, vitu hivyo lazima ujue kuvikabili ili uikubali ndoa.Yes, hii ni kauli ya kijana anayeelekea kukomaa kiakili.
Ni kweli kabisa siri ya maisha yako unaijua wewe mwenyewe, mtu asikupangie uoe au usioe, ila kila jambo na wakati wake kuna muda utakataa ndoa kwa sababu fulani, kuna muda utataka ndoa kwasababu fulani. Hakuna jambo linalotokea bila sababu.Kila mtu ana muda wake mkuu hata mimi huwa nasemaga kuna jamaa mda mwingi huwa anakuja pm kunipa angalizo na nyuz zangu ila jibu langu kubwa ni kuwa mimi na maisha yangu ujui napitia nn huku
Hujawahi kusikia kuwa Martin Luther alichomoa vitaba sita katika bibilia ya mwanzo na kubakiza vitabu 66?Mimi sio mkatoliki mkuu naamini katika biblia yenye vitabu 66 tu zingatia neno NAAMINI
Kila kitu kinatokea kwa sababu.Ni kweli kabisa siri ya maisha yako unaijua wewe mwenyewe, mtu asikupangie uoe au usioe, ila kila jambo na wakati wake kuna muda utakataa ndoa kwa sababu fulani, kuna muda utataka ndoa kwasababu fulani. Hakuna jambo linalotokea bila sababu.