SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,193
- 8,009
Juzi katika mechi ya Yanga vs Al Ahly uwanja wa Mkapa, mashabiki wa Yanga waling'oa viti na kuwarushia mashabiki waliokuwa wanaishangilia Al Ahly. Inteligensia yangu imeniambia kuwa mashabiki wa Yanga walifanya hivyo baada ya kuudhiwa na kitendo cha mashabiki wa Al Ahly kuwasha moshi uliosambaa upande walilokuwa.
Nakumbuka mwishoni mwa msimu uliopita, Yanga walifanya gwaride na kwa wingi wao walipita mtaa wa Msimbazi ili kuikebehi Simba na wakawasha fataki na moshi. Wengine walidai ule ni utani wa jadi ila tunasahau busara huwa inatumika hata viwanjani kuwatenganisha mashabiki wa pande mbili pamoja kwamba huo utani wa jadi upo.
Nakumbuka baada ya gwaride la Yanga niliwahi kusema, siku mashabiki wa Simba wakisherehekea kwa kupita makao makuu ya Yanga na kufanya kile kile walichofanya Yanga, mashabiki wa Yanga watawafanyia vurugu. Leo maneno yangu yanathibitisha kuwa hilo litakuja kutokea.
Tukio walilofanya mashabiki wa Yanga kupita na kuwasha moshi mtaa wa Msimbazi lingeweza kuleta maafa makubwa sana, tushukuru tu ustaarabu ulioonyeshwa na mashabiki wa Simba. Kama maafa yangetokea, wa kulaumiwa wangekuwa ni vyombo vya ulinzi na usalama vilivyoruhusu jambo lile kufanyika.
Kitendo walichofanya Yanga kimelitia dosari taifa. Tunategemea Mwenyekiti wa chama cha vilabu Afrika ambaye uzuri alikuwepo uwanjani, atoke hadharani aikemee klabu ya Yanga kwa kitendo hicho na pia TFF waipigishe faini klabu ya Yanga na kupewa onyo kali.