Yanga ichukuliwe hatua kwa uharibifu iliyofanya juzi uwanja wa Mkapa

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,131
7,902
Juzi katika mechi ya Yanga vs Al Ahly uwanja wa Mkapa, mashabiki wa Yanga waling'oa viti na kuwarushia mashabiki waliokuwa wanaishangilia Al Ahly. Inteligensia yangu imeniambia kuwa mashabiki wa Yanga walifanya hivyo baada ya kuudhiwa na kitendo cha mashabiki wa Al Ahly kuwasha moshi uliosambaa upande walilokuwa.

Nakumbuka mwishoni mwa msimu uliopita, Yanga walifanya gwaride na kwa wingi wao walipita mtaa wa Msimbazi ili kuikebehi Simba na wakawasha fataki na moshi. Wengine walidai ule ni utani wa jadi ila tunasahau busara huwa inatumika hata viwanjani kuwatenganisha mashabiki wa pande mbili pamoja kwamba huo utani wa jadi upo.

Nakumbuka baada ya gwaride la Yanga niliwahi kusema, siku mashabiki wa Simba wakisherehekea kwa kupita makao makuu ya Yanga na kufanya kile kile walichofanya Yanga, mashabiki wa Yanga watawafanyia vurugu. Leo maneno yangu yanathibitisha kuwa hilo litakuja kutokea.

Tukio walilofanya mashabiki wa Yanga kupita na kuwasha moshi mtaa wa Msimbazi lingeweza kuleta maafa makubwa sana, tushukuru tu ustaarabu ulioonyeshwa na mashabiki wa Simba. Kama maafa yangetokea, wa kulaumiwa wangekuwa ni vyombo vya ulinzi na usalama vilivyoruhusu jambo lile kufanyika.

Kitendo walichofanya Yanga kimelitia dosari taifa. Tunategemea Mwenyekiti wa chama cha vilabu Afrika ambaye uzuri alikuwepo uwanjani, atoke hadharani aikemee klabu ya Yanga kwa kitendo hicho na pia TFF waipigishe faini klabu ya Yanga na kupewa onyo kali.
 
Serikali imetumia hela kuboresha uwanja,hata Simba wana sehemu jasho lao katika kurepair na hayo yote yalifanywa kwa ajili ya kuheshimisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa hasa African football league,club bingwa na AFCON, uwanja sasa hata timu mbali mbali za mataifa mengine wanaulipia na kucheza hapo, lakini hawa wennzetu hawana uchungu, TFF inatakiwa iwapige faini pamoja na Yanga kutoa hela kwa uharibu wote uwanja urekebishwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona wanaoonekana Kwenye picha ni mashabiki wa Simba wakishangilia na waume zao baada ya kufunga goli?

View attachment 2833345
Utasemaje mashabiki wa Simba wakati Simba haikuwa inacheza hapo? Hata kwa sheria za CAF, hawawezi kuwatambua hao kama ni mashabiki wa Simba. Hao hapo wote walikuwa wanaishangilia Al Ahly.
 
Uzuri Yanga hatuna ujinga huo wenye tabia hizo wanajulika,mechi zao wanasusa ila za wenzao wanakuja kufanya fujo. Wazee wa kujifariji kwa matokeo ya Yanga.
Kwani wapi nilipomzuia mtu kushabikia timu? Mimi ninachopinga ni kusema mashabiki wa Yanga ndio wameng'oa viti wakati kwenye picha wanaoonekana ni mashabiki wa Simba!
Ninao uthibitisho wa wazi unaoonyesha mashabiki wa Yanga wakirusha viti upande wa mashabiki wa Al Ahly. Clip uliyotuma haioneshi hao mashabiki wa Al Ahly wakirusha viti zaidi ya kushangilia tu
 
Ninao uthibitisho wa wazi unaoonyesha mashabiki wa Yanga wakirusha viti upande wa mashabiki wa Al Ahly
Weka hapa, ila hao wanarukaruka juu ya viti nazani umewaona ni mashabiki wa 5imba ......... au nao wanasingiziwa. Maana mechi haiwahusu za kwenu mnasusa,basi tizameni burudani mshangilie kiustaraabu mnaruka juu ya viti,plus mafataki.Then lawama wanatupiwa Yanga.
 
Hawa viumbe ni waharibifu sana
FB_IMG_1700028629335.jpg
 
Msimu huu mashabiki wa simba mnaongoza kulalamika kwa kila jambo ,mna hasira sana halafu mmeiga tabia zoooteee za Yanga mlizokua mnazilalamikia kama kushabikia timu pinzani mliita umalaya ambao hamna muda nao. Ila now day mmekua zaidi ya MALAYA
 
Msimu huu mashabiki wa simba mnaongoza kulalamika kwa kila jambo ,mna hasira sana halafu mmeiga tabia zoooteee za Yanga mlizokua mnazilalamikia kama kushabikia timu pinzani mliita umalaya ambao hamna muda nao. Ila now day mmekua zaidi ya MALAYA
Yanga haijawahi kuwa na tabia za kishamba kama hizi,hawa 5imba wanafosi Yanga ionekane mbovu au ifanye vibaya ili tu wapate pa kupumulia,Yanga tuliisapoti timu yetu wakati inatembeza bakuli na si kuisusa hawa wajinga 5imba wataweza!
 
Back
Top Bottom