Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Wakuu!
Kabla hili la Yanga SC halijapoa, tuzungumze kidogo kuhusu kilichotokea.
Labda wengi hawakutarajia kwamba klabu maarufu ya Yanga (Wananchi) ingejikuta katikati ya mjadala mkubwa wa Kitaifa hivi karibuni. Yanga imejikuta ikijadiliwa sana na kukosolewa vikali baada ya kuchangia kiasi cha Tsh. 100 milioni katika harambee ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyolenga kukusanya Tsh. bilioni 100 kwa ajili ya kampeni za Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025. Mchango huo, ulitolewa na Rais wa timu hiyo, Eng. Hersi Said.
Sasa wenye mpira wao FIFA wanasemaje kupitia Kanuni?
FIFA, kama Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu, lina kanuni za wazi kabisa zinazozuia vilabu vyake wanachama kuchangia vyama vya siasa. Sheria na kanuni za FIFA zinaeleza bila shaka kwamba vyama wanachama lazima vizingatie maagizo ya shirikisho, ikiwa ni pamoja na kanuni ya kutoegemea upande wowote kisiasa na kutojitenga na vyombo vya nje.
Kwa mfano, Kanuni za FIFA, Kifungu cha 4, kinakataza ubaguzi wa kisiasa na ushawishi wa kisiasa katika soka. Kifungu hiki kinahakikisha kwamba vilabu vya mpira vinapaswa kubaki na uhuru wa utendaji kazi, bila kujihusisha na siasa au kushawishiwa kisiasa.
Aidha, Kanuni za FIFA, Vifungu vya 14 na 19, vinavyohusiana na usimamizi wa vilabu na mashirikisho ya soka, vinataka vyombo hivi viwe huru na bila ushawishi wa kisiasa. Hii inamaanisha kuwa vilabu vya mpira vinapaswa kufanya shughuli zao za kimaendeleo kwa manufaa ya mchezo, na siyo kwa maslahi ya kisiasa au vyama vya siasa.
Kwa hivyo, mchango wa Yanga SC kwa CCM, ingawa ni suala la kisiasa, unaweza kuwa na athari kwa kanuni hizi, kwani inakiuka dhana ya uhuru wa vilabu wa kutoshawishika kisiasa.