Yanga FC yaingia mkataba mpya na SportsPesa wa miaka 3 wenye thamani ya Tsh Bilioni 12

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,288
9,923
Yanga leo inakwenda kuweka historia nyingene, Futilia live hapa

Ni mKataba wenye thamani ya tshs bilioni 12 na Milioni 300 kwa miaka 3, Kila Mwaka Yanga itakuwa inapata bilioni nne, pia yanga akichukuwa ligi milioni 150, na ikifika Fainali FA itapata Tshs Milioni 75.

---

1658915686739.png
Mabingwa wa kihistoria na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Dar Young Africans (Yanga) leo wamesaini mkataba mpya wa udhamini na kampuni ya michezo ya kubashiri ya Sport Pesa mkataba ambao unaweza kuwa wenye thamani zaidi kwa timu za Ligi Kuu nchini Tanzania.

Mkataba huo wenye thamani ya Shilingi Bilioni 12.335 wa miaka mitatu unaifanya SportPesa kuwa mdhamini mkuu wa Yanga kuanzia msimu mpya unaoanza wa Ligi.

Katika mkataba mpya kwa Mwaka Yanga watachota zaidi ya Shilingi Bilioni 4 tofauti na mkataba uliopita ambapo Yanga walikuwa wanapata Bilioni 1 pekee kwa Mwaka, hii ina maana hili ni ongezeko la zaidi ya Bilioni 3 kwa mwaka.

Maboresho mengine katika mkataba huo ni kuwa "Bonus" ya Ubingwa wa Ligi Kuu imeongezeka kutoka Milioni 100 hadi 150.

Huku Bonus ya kombe la FA ambayo haikuwepo hapo awai ikiongezwa ambapo Yanga watapata Milioni 75 kwa kufika hatua ya Fainali.
 
Mabingwa wa kihistoria na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Dar Young Africans (Yanga) leo wamesaini mkataba mpya wa udhamini na kampuni ya michezo ya kubashiri ya Sport Pesa mkataba ambao unaweza kuwa wenye thamani zaidi kwa timu za Ligi Kuu nchini Tanzania

Mkataba huo wenye thamani ya Shilingi Bilioni 12.335 wa miaka mitatu unaifanya SportPesa kuwa mdhamini mkuu wa Yanga kuanzia msimu mpya unaoanza wa Ligi.

Katika mkataba mpya kwa Mwaka Yanga watachota zaidi ya Shilingi Bilioni 4 tofauti na mkataba uliopita ambapo Yanga walikuwa wanapata Bilioni 1 pekee kwa Mwaka, hii ina maana hili ni ongezeko la zaidi ya Bilioni 3 kwa mwaka.

Maboresho mengine katika mkataba huo ni kuwa "Bonus" ya Ubingwa wa Ligi Kuu imeongezeka kutoka Milioni 100 hadi 150.

Huku Bonus ya kombe la FA ambayo haikuwepo hapo awai ikiongezwa ambapo Yanga watapata Milioni 75 kwa kufika hatua ya Fainali.
 
Hii Sasa Sifa mkataba wa bilion nne na ushee Kwa mwaka!! Nyie Sport pesa mnawafanya Yanga waende kuchukua vikombe vyote msimu ujao. Ina maana ni mara tatu ya mkataba walio ingia Simba.

Kama Yanga watafanikiwa kupata udhami kwenye kampuni nyingine na jumla ya udhamini wao ukafika bilioni nane basi hakuna Sababu yoyote ya kufanya timu isifike robo fainali Kila msimu wa mashindano ya Caf champion league.
 
Hii Sasa Sifa mkataba wa bilion nne na ushee Kwa mwaka!! Nyie Sport pesa mnawafanya Yanga waende kuchukua vikombe vyote msimu ujao. Ina maana ni mara tatu ya mkataba walio ingia Simba.

Timu kubwa
 
Back
Top Bottom