Yanayojiri bungeni Dodoma leo tarehe 27 Mei, 2015

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,486
Waziri wa Ujenzi ndugu John Pombe Magufuli leo amewasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake ya ujenzi mnamo majira ya saa nne na nusu asubuhi kwa muda wa Afrika ya Mashariki.

Katika hotuba yake ambayo ni ya mwisho kwake katika uhai wa serikali ya awamu ya nne, ameainisha mipango na mafanikio katika wizara hiyo kama vile ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, madaraja, nyumba za watumishi wa serikali pamoja na vivuko.

Ameainisha miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara na madaraja ambapo hadi kukamilika kwake, zinahitajika zaidi ya trilion nne za kitanzania. Aidha ametumia michoro mbalimbali na ramani kuonyesha miradi iliyopo kwenye mpango huo wa ujenzi katika wizara yake.

Kwa sasa anaomba zaidi ya bilioni 932 ili kukamilisha miradi iliyopo kwenye mpango wa sasa.

===updates===
Hotuba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni imewasilishwa na mh. Mkosamali ambapo hotuba yake imejikita katika madeni yanayodaiwa na makandarasi katika wizara hiyo ambapo madeni hayo yanakadiriwa kuwa zaidi ya bilioni 800, kiasi ambacho ni karibia kiasi kinachoombwa na wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

HOTUBAYA WAZIRI WA UJENZI, MHESHIMIWADKT. JOHN POMBE MAGUFULI (MB),AKIWASILISHABUNGENI MPANGO NAMAKADIRIO YA MAPATONA MATUMIZI YA FEDHAKWA MWAKA WA FEDHA 2015/16

UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa fedha 2014/15. Aidha, naomba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2015/16. Aidha, napenda kutoa Taarifa kuwa Takwimu za Aya ya 14 ya Kitabu cha Hotuba yangu zimerekebishwa na marekebisho yake yameambatishwa.

Mheshimiwa Spika, napenda kumshukuru sana Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kunijalia afya njema kutekeleza majukumu ya kuiongoza Wizara ya Ujenzi ambayo inatoa mchango mkubwa wa maendeleo ya Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, naomba pia nichukue fursa hii kwa heshima kubwa kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuendelea kuiongoza nchi yetu vyema katika kipindi chote cha Serikali ya Awamu ya Nne (2005– 2015).

Mhe. Rais atabaki katika kumbukumbu za Watanzania kwa mchango wake uliotukuka katika kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na miundombinu ya usafiri ikiwemo barabara, madaraja na vivuko ambavyo ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika taifa letu.

Aidha, nawapongeza Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna ambayo wamemsaidia Mheshimiwa Rais kusimamia na kuongoza shughuli zote za Serikali ya Awamu ya Nne.

Mheshimiwa Spika, kipekee nakupongeza wewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa hekima, umahiri na busara mnazotumia katika kuliongoza Bunge hili Tukufu.

UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM KATIKA KIPINDI CHA 2005 – 2015

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ujenzi imeendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni Chama Tawala kuanzia mwaka 2005 hadi 2015.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne, Serikali imepata mafanikio makubwa katika kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja nchini. Katika kipindi hicho, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 17,762 zimekuwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji ambapo barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 5,568 zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.

Aidha, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 3,873 zimeendelea kujengwa kwa kiwango cha lami. Katika kipindi hicho, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 4,965 zimefanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na Serikali inatafuta fedha za kuzijenga kwa kiwango cha lami. Vilevile, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara zenye jumla ya kilometa 3,356 unaendelea.

Mheshimiwa Spika, kuhusu ujenzi na ukarabati wa madaraja, jumla ya madaraja makubwa 30 yapo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Kati ya hayo, madaraja makubwa 12 yamekamilika kujengwa, ambayo ni Rusumo (Kagera), Umoja (Mtwara), Mwanhuzi (Simiyu), Kikwete (Kigoma), Nangoo (Mtwara), Ruhekei (Ruvuma), Mbutu (Tabora), Mwatisi (Morogoro), Ruvu (Pwani), Nanganga (Mtwara), Maligisu (Mwanza) na daraja la waenda kwa miguu la Mabatini (Mwanza).

Aidha, madaraja makubwa 6 yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi, ambayo ni Kigamboni (Dsm), Kilombero (Morogoro), Kavuu (Katavi), Sibiti (Singida), Ruvu Chini (Pwani) na Lukuledi II (Mtwara).

Madaraja makubwa 12 yako kwenye maandalizi ya kujengwa ambayo ni Momba (mpakani mwa Rukwa na Mbeya), Mwiti (Mtwara), Simiyu (Mwanza), Wami (Pwani), Ruhuhu (Ruvuma), Ubungo Interchange (Dar es Salaam), TAZARA Flover (Dar es Salaam), Selander (Dar es Salaam), Daraja jipya la Wami Chini (Pwani), Pangani (Tanga), Kirumi (Mara) na daraja la waenda kwa miguu la Furahisha (Mwanza). Sambamba na ujenzi wa madaraja makubwa, madaraja madogo madogo zaidi ya 7,200 yamejengwa na kukamilika.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2015 Serikali pia imeimarisha Mfuko wa Barabara ambapo mapato ya Mfuko yameongezeka kutoka Shilingi bilioni 73.08 katika mwaka wa fedha 2005/06 hadi Shilingi bilioni 751.7 katika mwaka wa fedha 2014/15 ikiwa ni ongezeko la asilimia 928.6.

Mheshimiwa Spika, wakati Serikali ya Awamu ya Nne inaingia madarakani mwaka 2005, vivuko vya Serikali vilivyokuwa vinatoa huduma vilikuwa kumi na tano (15) tu. Hadi kufikia Aprili, 2015, idadi ya vivuko vya Serikali vinavyotoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini imeongezeka na kufikia ishirini na nane (28).

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa nyumba na majengo ya Serikali, Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ilijenga nyumba 173 za makazi ya Viongozi wa Umma na kuanza mradi wa ujenzi wa nyumba 10,000 za Watumishi wa Umma ambapo nyumba 643 zilikamilika katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2015 na nyumba 270 zinaendelea kujengwa.

Aidha, Wizara kupitia TBA imeendelea kuhakikisha kwamba ujenzi wa nyumba na majengo yanayotumiwa na umma unazingatia mahitaji maalum hususan kwa watu wenye ulemavu. Suala hililimeendelea kutekelezwa kupitia miradi ya ujenzi wa majengo yote ya Serikali ambayo Wakala wa Majengo umesanifu na kusimamia kama ifuatavyo: Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara, Majengo ya Ofisi za Wakuu wa Wilaya za Bariadi, Rorya, Kilolo, Nyamagana na Mvomero.

Mengine ni jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi – Kitengo cha Wakimbizi, jengo la hospitali ya Manyara na ukumbi wa mikutano na Vituo vya Afya ya Msingi (Primary Health Centre Institutions – PHCI) – Iringa, majengo ya Ofisi za Wakuu wa Mikoa ya Katavi, Njombe, Geita na Simiyu pamoja na majengo ya Ofisi za Wakuu wa Wilaya 19 za Buhigwe, Busega, Butiama, Chemba, Gairo, Ikungi, Itilima, Kalambo, Kaliua, Kakonko, Kyerwa, Mbogwe, Mkalama, Mlele, Momba, Nyang`hwale, Nyasa, Uvinza na Wanging'ombe.

Mheshimiwa Spika, Kitabu cha Taarifa ya Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne katika Sekta ya Ujenzi kwa kipindi cha Mwaka 2005 hadi Tarehe 23 Mei, 2015 kimegawanywa kwa Waheshimiwa Wabunge pamoja na Kitabu cha Hotuba yangu. Naomba Bunge ipokee Taarifa ya Kitabu hicho kama Kiambatisho cha Hotuba yangu ya Bajeti na vijumuishwe kwenye 'Hansard'.

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2014/15

Bajetiya Matumizi ya Kawaida:

Mheshimiwa Spika, maelezo ya bajeti ya kawaida yameelezwa Ukurasa wa 12 - 13 wa Kitabu cha Hotuba yangu ya Bajeti.

UTEKELEZAJIWA MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2014/15

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Wizara iliidhinishiwa na Bunge Shilingi 662,234,027,000.00 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Fedha zilizotolewa hadi Aprili, 2015 ni Shilingi 444,729,086,445.00.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayosimamiwa na Wizara unaendelea vizuri. Kwa upande wa barabara kuu, jumla ya kilometa 504.4 kati ya kilometa 539 zilizopangwa kujengwa kwa kiwango cha lami zilikuwa zimekamilika hadi kufikia Aprili, 2015. Aidha, kilometa 87.75 zilikua zimekarabatiwa kwa kiwango cha lami. Kwa upande wa barabara za mikoa, kilometa 40.5 zilijengwa kwa kiwango cha lami.

Vile vile, kilometa 450 zilifanyiwa ukarabati kwa kiwango cha changarawe katika kipindi hicho.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Madaraja ya Mbutu na Maligisu ulikamilika katika mwaka 2014/15. Aidha, ujenzi wa madaraja makubwa sita (6) unaendelea, ambayo ni Kigamboni, Ruvu Chini, Lukuledi II, Kavuu, Kilombero na Sibiti. Vilevile, usanifu wa daraja la Ruhuhu umekamilika.

HATUAZINAZOCHUKULIWA NA WIZARA YA UJENZI KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MAGARIDAR ES SALAAM

Mheshimiwa Spika, suala la kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es salaam ni suala MTAMBUKA linalohusisha Wizara na Mamlaka mbalimbali zikiwemo Halmashauri za Jiji. Katika Wizara ya Ujenzi hatua mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa kukabiliana na tatizo hilo la msongamano wa magari. Naomba nizielezee hatua hizo pamoja na gharama ambazo Serikali inagharimikia.

Mheshimiwa Spika, maandalizi ya ujenzi barabara ya njia sita ya Dar es Salaam – Chalinze – Morogoro (km 200) sehemu ya Dar es Salaam – Chalinze (km 100) imepangwa kujengwa kwa kiwango cha "Expressway". Maandalizi ya mradi huu utakaotekelezwa kwa utaratibu wa ubia baina ya Serikali na Sekta Binafsi (Public Private Partnership - PPP) yameanza. Hadi kufikia Aprili, 2015, Mshauri Mwelekezi (Transaction Advisor) ambaye ni Kampuni ya Cheil Engineering Company Limited kutoka Korea ya Kusini alikwishateuliwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 7.72 na amekamilisha utafiti wa mwelekeo wa barabara (route survey).

Mwelekeo wa barabara uliochaguliwa unaanzia Charambe katika barabara ya Kilwa kupitia Kisarawe, Kibamba, Kibaha, Mlandizi hadi Chalinze. Barabara hii yenye urefu wa kilometa 128 itakuwa ya njia sita (6) na barabara za juu (interchanges) tano (5) katika maeneo ya Charambe, Kisarawe, Kibamba, Mlandizi na Chalinze. Aidha, kutakuwa na vituo vikuu viwili (2) vya kulipia tozo ya barabara (Toll Plaza) maeneo ya Charambe na Chalinze. Pia barabara hii itakuwa na eneo la kupumzika (rest station) pale Visiga na maeneo mawili (2) ya kuegesha malori ambayo yatakuwa Mbezi na Mbala. Vilevile Mshauri Mwelekezi atafanya utafiti wa jinsi ya kuunganisha barabara hii kutoka Charambe hadi bandari ya Dar es Salaam.

Kwa sasa Mshauri Mwelekezi anaendelea na kazi ya kuandaa nyaraka za zabuni na baadaye atasimamia taratibu za kumpata Mbia/Mwekezaji (Concessionaire) wa mradi huu. Gharama za mradi huu wa ujenzi zinakadiriwa kufikia Shilingi Trilioni 2.397 na utatekelezwa kwa njia ya Ubia na Sekta Binafsi (PPP).

Mheshimiwa Spika, kuhusu ujenzi wa Daraja Jipya la Selander ambalo lengo kuu ni kupunguza msongamano wa magari katika eneo la Selander, Serikali ya Korea Kusini imekubali kuipatia Serikali ya Tanzania mkopo wa masharti nafuu kwa ajili ya ujenzi wa Daraja jipya la Selander. Upembuzi yakinifu wa mradi huu umekamilika na maandalizi ya kutiliana saini makubaliano ya mkopo wa kugharamia ujenzi wa daraja kati ya Korea Exim Bank (kwa niaba ya Serikali ya Korea Kusini) na Serikali ya Tanzania yanaendelea.

Daraja hili pamoja na barabara zake za maingilio litakuwa na urefu wa jumla ya kilometa 7.2 na litaanzia eneo la Koko Beach kupitia Kenyatta Drive na kuingia baharini na kisha kuungana na barabara ya Barack Obama eneo la Hospitali ya Aghakan. Mradi huu utagharimu Shilingi Bilioni 197.5. Aidha, Daraja la Kigamboni linaendelea kujengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 236.524.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara za juu (flyovers na interchanges) na maboresho ya makutano ya barabara katika jiji la Dar es Salaam,. Hadi Aprili, 2015 hatua ya utekelezaji iliyofikiwa ni kama ifuatavyo:

Barabaraya Juu(Flyover) yaTAZARA:
Usanifuwa kina umekamilika chini ya ufadhili wa Serikali ya Japan. Taratibuza kumpata Mkandarasi wa ujenzi atakayekidhi vigezo zinaendelea hukoJapan. Tenda zitafunguliwa Tarehe 29 Mei, 2015 na Mkataba kusainiwaTarehe 03 Juni, 2015. Kazi ya ujenzi wa Flyoverya TAZARA ambayo itagharamiwa na Serikali ya Japan ikishirikiana naSerikali ya Tanzania inatarajiwa kuanza mwezi Juni, 2015. Gharama zamradi huu ni ShilingiBilioni 93.622.

Interchangeya Ubungo:
Benkiya Dunia imekubali kugharamia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wabarabara za juu (Interchange)katika makutano ya Ubungo. Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina waInterchangeya Ubungo umekamilika.

Zabuni ya kumpata Mhandisi Mshauri kwa ajiliya usimamizi wa ujenzi zimetangazwa. Aidha, Serikali inakamilishataratibu kwa ajili ya kutangaza zabuni za kumtafuta Mkandarasi waujenzi. Interchangeya Ubungo itakuwa na levelstatu ambapo magari yanayotoka katikati ya jiji la Dar es Salaamkuelekea Morogoro yatapita chini, magari yanayotoka TAZARA kuelekeaMwenge yatapita juu na magari yanayokata kulia yatapita katikati.Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa ShilingiBilioni 126.661.

Upanuzi wa barabara ya Gerezani (Bendera Tatu – KAMATA) unakadiriwakugharimu ShilingiBilioni 29.135.Pia maandalizi ya Maboreshoya Makutano ya Chang'ombe, Magomeni, Mwenge, Tabata, KAMATA, Uhasibuna Morocco yanaendelea.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Wizara imeendelea kutekeleza miradi ya barabara za kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam zenye urefu wa kilometa 109.35.

Barabara hizo ni pamoja na Ubungo Bus Terminal – Mabibo – Kigogo Roundabout (km 6.4); Kigogo Roundabout – Bonde la Msimbazi – Twiga/Msimbazi Jct (km 2.7); Jet Corner – Vituka – Devis Corner (km 10.30); Tabata Dampo – Kigogo (km 1.60); Ubungo Maziwa – External (km 0.65); Mbezi (Morogoro Road) – Malambamawili – Kinyerezi –Banana (km 14); Tegeta Kibaoni – Wazo Hill – Goba – Mbezi Mwisho (km 20); Tangi Bovu – Goba (km 9); Kimara Baruti–Msewe (km 2.6); Kimara – Kilungule – External Mandela Road (km 9); na Kibamba – Kisopwa (km 12.0).

Pia ukarabati unaoendelea katika barabara za Ukonga – Mombasa – Msongola , Kimbiji – Tundwisongani, Misheni – Kijichi – Zakhem, barabara ya Uhuru, Kutengeneza Mifereji ya Maji, uhamishaji miundombinu maeneo ya miradi, malipo ya fidia, n.k. vyote vinakadiriwa kugharimu Shilingi Bilioni 181.795.

Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea na Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (Bus Rapid Transit Infrastructure – BRT) ambao unajumuisha Ujenzi wa Barabara ya Morogoro kutoka Kimara hadi Kivukoni, barabara ya Kawawa kutoka Magomeni hadi Morocco na barabara ya Msimbazi kutoka Fire hadi Kariakoo zenye jumla ya urefu wa kilometa 20.9. Pia kuna vituo vya mabasi 29, vituo vikubwa vitatu na madaraja ya waenda kwa miguu matatu.

Pia Ujenzi wa Karakana (Depot) na Kituo cha Mabasi cha Ubungo; Ujenzi wa Karakana (Depot) ya Jangwani; Ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi (Terminal) cha Kivukoni; Ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi (Terminal) cha Kariakoo; Ujenzi wa Vituo vya Mlisho (Feeder Stations - Urafiki, Shekilango, Magomeni Mapipa, Kinondoni, Mwinyijuma na Fire); na Uhamishaji wa Miundombinu ya Umeme. Mradi huu utagharimu Shilingi Bilioni 423.9.

Aidha, miradi ya upanuzi wa Barabara ya New Bagamoyo (Mwenge – Tegeta) ambao umegharimu Shilingi Bilioni 99.062 na sehemu ya Morocco – Mwenge ambao unakadiriwa kugharimu Shilingi Bilioni 56.784. Ujenzi wa Barabara ya Pete kutoka Pugu – Kifuru – Mbezi – Mpiji Magoe – Bunju (km 33.7) unakadiriwa utagharimu Shilingi Bilioni 534.4.

Mheshimiwa Spika, miradi hii yote ambayo Wizara imepanga kuitekeleza katika Jiji la Dar es salaam pekee hadi itakapokamilika itagharimu zaidi ya Shilingi Trilioni 4.394.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2015 Wizara ya Ujenzi kupitia TEMESA imetekeleza kazi zifuatazo:

  1. [*=center] Taratibu za kumpata Mkandarasi wa kujenga kivuko kipya cha Magogoni – Kigamboni, kivuko cha Pangani – Bweni, na kukarabati kivuko cha MV Magogoni zipo katika hatua za mwisho.

  1. [*=center] Taratibu za ununuzi wa mashine za kielektroniki za kukatia tiketi katika Kivuko cha Ilagala – Kajeje zinaendelea.
    [*=center] Ujenzi wa maegesho ya Iramba – Majita unaendelea. Aidha, ujenzi wa maegesho ya kivuko kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo eneo la Magogoni na Mbegani umekamilika na kivuko MV Dar es Salaam kinafanya kazi hivi sasa.

  1. [*=center] Jumla ya magari 10,991 yalifanyiwa matengenezo katika karakana za mikoa yote.
    [*=center] Ujenzi wa vituo vitatu vya maegesho ya kivuko cha MV TEMESA katika maeneo ya Luchelele, Igogo na Sweya kwa ajili ya kupunguza msongamano wa magari jijini Mwanza.

  1. [*=center] Ukarabati wa karakana za MT. Depot na Dodoma, na ujenzi wa karakana mpya ya mkoa wa Manyara unaendelea.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2015, TBA imeendelea na utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya viongozi na watumishi wa umma, majengo ya ofisi za Serikali na majengo ya biashara ambapo utekelezaji wa miradi ifuatayo upo katika hatua za umaliziaji: ujenzi wa jengo la ghorofa 8 lenye ‘flats' 16 lililopo eneo la SIDA Estate (Dar es Salaam); jengo la ghorofa 4 lililopo eneo la Mbezi Beach EX – NMC ( Dar es Salaam); jengo la kitega uchumi lililopo barabara ya Wachaga (Arusha) na jengo la ghorofa 6 lililopo mtaa wa Moshi (Dodoma). Aidha, Wakala umesimamia jumla ya miradi 58 ya Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali za Umma ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Usanifu wa miradi hii umezingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu. Vile vile, Wakala umeendelea na mradi wa ujenzi wa nyumba 10,000 za Watumishi wa Umma ambapo umekamilisha ujenzi wa nyumba 155 zilizopo eneo la Bunju B, Dar es Salaam. Wakala pia umeendelea kuimarisha Kikosi chake cha ujenzi kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya "Tunnel Formwork System" ili kuongeza kasi ya ujenzi na kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba za watumishi wa Serikali. Kwa upande wa ujenzi wa nyumba za TAMISEMI, Wakala umeanza ujenzi wa nyumba 149 katika mikoa 20 ya Tanzania Bara ambapo utekelezaji wake upo katika hatua mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2015 Bodi ya Mfuko wa Barabara ilikua imepokea kutoka Hazina jumla ya Shilingi 284,118,900,002. Bodi ilizigawa fedha hizo kwa Bodi yenyewe, TANROADS, TAMISEMI na Wizara ya Ujenzi. Aidha, Bodi imekwishaanza ujenzi wa jengo la ofisi Mjini Dodoma; utaratibu wa kununua vifaa vya kupimia ubora wa kazi unaendelea, utafiti wa maeneo mapya ya vyanzo vya mapato unaanza mwezi Juni 2015, ukaguzi wa kiufundi wa kazi za matengenezo ya barabara unaendelea nchini na maandalizi ya hadidu za rejea kwa ajili ya kazi ya kuhakiki takwimu za barabara zimekamilika.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2015 Bodi ya Usajili wa Wahandisi ilisajili wahandisi 966 na makampuni ya ushauri wa kihandisi 16 na kufikisha jumla ya wahandisi 15,062 waliosajiliwa katika ngazi mbalimbali na makampuni ya ushauri wa kihandisi 279. Kati ya wahandisi waliosajiliwa 13,636 ni wazalendo na 1,426 ni wageni, makampuni ya ushauri wa kihandisi 201 ni ya kizalendo na 78 ni ya kigeni. Mafundi Sanifu (Engineering Technicians) 63 walisajiliwa.

Aidha, Bodi iliendelea kuwaapisha Wahandisi Viapo vya Utii wa Maadili ya Taaluma (Professional Oath) ambapo idadi ya wahandisi 1,909 walikula viapo. Aidha, Bodi ilifuta usajili kwa wahandisi watalaam 95, wahandisi washauri 24 na Kampuni za Ushauri wa Kihandisi 5 kwa kukiuka sheria ya usajili wa wahandisi.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2015, Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi ilisajili Wabunifu Majengo 40 na Wakadiriaji Majenzi 43 na kufanya jumla ya Wabunifu Majengo waliosajiliwa hadi sasa kufikia 398 na Wakadiriaji Majenzi kufikia 294. Aidha, Bodi ilisajili Kampuni za Ubunifu Majengo 9 na Ukadiriaji Majenzi 8 na kufanya jumla ya Kampuni za Ubunifu Majengo zilizosajiliwa kufikia 327 na Ukadiriaji Majenzi 321.

Vilevile, Bodi ilifanya ukaguzi wa shughuli za wataalam kwenye miradi katika mikoa 25 ya Tanzania Bara kama ifuatavyo: Dar es Salaam (870), Tanga (42), Pwani (81), Kigoma (30), Tabora (30), Dodoma (99), Singida (72), Mwanza (128), Mara (28), Shinyanga (50), Arusha (91), Kilimanjaro (26), Mbeya (30), Rukwa (16), Manyara (18), Ruvuma (11), Iringa (48), Morogoro (92), Simiyu (25), Kagera (50), Lindi (5), Mwanza (22), Njombe (14), Katavi (5) na Geita (21). Kazi nyingine zilizofanywa na Bodi ni kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu 42 katika fani ya Ubunifu Majengo na Ukadiriaji Majenzi na kutoa elimu kuhusu taaluma za Ubunifu Majengo na Ukadiriaji Majenzi kwa TAMISEMI na Askari Polisi katika mikoa ya Dodoma, Mbeya, Pwani, Morogoro, Singida, Tabora, Ruvuma, Njombe, Iringa, Katavi na Rukwa.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2014/15, Bodi ya Usajili wa Makandarasi hadi kufikia Aprili, 2015 ilisajili Makandarasi wapya 936 wa fani mbalimbali na kusajili miradi 2,497 ambayo ina thamani ya kuanzia Shilingi milioni 10. Bodi pia ilikagua miradi 2,700 ya ujenzi, ambapo miradi 921 ilikutwa na kasoro. Makandarasi katika miradi yenye upungufu walichukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ikiwemo kutozwa faini, kusimamishwa kufanya kazi za ukandarasi na kufutiwa usajili. Aidha, Bodi iliendesha kozi za mafunzo 5 zenye lengo la kukuza uwezo wa makandarasi ambapo jumla ya makandarasi 212 walishiriki mafunzo hayo.

Mheshimiwa Spika, maelezo zaidi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Barabara Nchini ikiwa ni pamoja na ile ya kupunguza msongamano wa magari Jijini Dar es salaam, Madaraja, Nyumba, Vivuko, Miradi iliyotekelezwa kwa Fedha za Mfuko wa Barabara, Usalama Barabarani na Mazingira, Utekelezaji wa Masuala Mtambuka na Utekelezaji wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yametolewa kwa kina katika Kitabu cha Hotuba yangu ya Bajeti Ukurasa wa 13 – 111.

MAKADIRIO YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2015/16

Matumiziya Kawaida na Makadirio ya Mapato

Mheshimiwa Spika, bajeti ya Matumizi ya Kawaida ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2015/16 ni Shilingi 42,142,581,000.00. Kati ya fedha hizo, Shilingi 36,778,993,000.00 ni kwa ajili ya Mishahara ya Watumishi na Shilingi 5,363,588,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo ya Wizara na Taasisi. Aidha, Wizara ya Ujenzi inatarajia kukusanya mapato ya jumla ya Shilingi 47,765,000.00 katika mwaka wa fedha 2015/16.

Makadirioya Bajeti ya Miradi ya Maendeleo:

Mheshimiwa Spika,katika mwaka wa fedha 2015/16, Wizara imetengewa jumla ya Shilingi 890,572,770,000.00 kwa ajili ya kutekeleza Miradi ambayo ni ya kimkakati (Strategic) na Miradi isiyo ya kimkakati (Non–Strategic). Kati ya fedha hizo Shilingi 198,360,000,000.00 ni fedha za ndani, Shilingi 85,572,770,000.00 ni fedha za nje na Shilingi 606,640,000,000.00 ni fedha zilizotengwa kwa ajili ya Mfuko wa Barabara. Mgawanyo wa fedha za maendeleo pamoja na miradi iliyotengewa fedha kwa mwaka wa fedha 2015/16, ni kama inavyooneshwa katika Kiambatisho Na.1 katika Kitabu changu cha Hotuba ya Bajeti. Aidha, maelezo ya kila mradi ni kama ifuatavyo: –

MIRADIYA VIVUKO, UJENZI WA NYUMBA NA MAJENGO YA SERIKALI:

Mheshimiwa Spika,Ujenzi wa Maegesho ya Vivuko Shilingi Milioni 2,774.118 zimetengwa, Ununuzi wa Vivuko Vipya zimetengwa Shilingi Milioni 2,036.620, na Ukarabati wa Vivuko zimetengwa Shilingi Milioni 661.350.

Mheshimiwa Spika, Ujenzi na Ukarabati wa Nyumba na Majengo ya Serikali Shilingi Milioni 2,689.463 zimetengwa.

MIRADIYA BARABARA NA MADARAJA

Mheshimiwa Spika,barabara ya Wazo Hill – Bagamoyo – Msata na Bagamoyo – Saadani – Tanga (km 178) zimetengwa Shilingi Milioni4,410.000. Pia barabara ya Usagara – Geita – Kyamyorwa (km 422) sehemu ya Uyovu – Biharamulo (km 112) zimetengwa Shilingi Milioni 4,970.000. Aidha, barabara ya Kigoma – Kidahwe – Uvinza – Kaliua – Tabora (km 504.70) Shilingi Milioni 11,298.915 zimetengwa.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Marangu – Tarakea – Kamwanga/ Bomang'ombe – Sanya Juu (km 173), Arusha – Moshi – Holili (km 140), Marangu – Rombo Mkuu na Kilacha – Mwika (km 32), KIA – Mererani (km 26), Kwa Sadala – Masama – Machame Junction (km 16.0) na Kiboroloni – Kiharara – Tsuduni – Kidia (km 10.8) zimetengwa Shilingi Milioni 12,010.636.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Nangurukuru – Mbwemkuru (km 95) zimetengwa Shilingi Milioni 810.000, Mbwemkuru – Mingoyo (km 95) Shilingi milioni 217.000, na barabara ya Dodoma – Manyoni (km 127) imetengewa Shilingi Milioni 1,015.000.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Port Access (Nelson Mandela km16.8) zimetengwa Shilingi Milioni 967.000, Dumila – Kilosa (km 63) Shilingi Milioni 3,363.000.

Mheshimiwa Spika, Ujenzi wa Madaraja ya Kirumi, Nangoo, Sibiti, Kilombero, Kavuu, Mbutu, Ruhekei, Ruhuhu, Momba, Simiyu, Wami, Lukuledi II, Selander na Ununuzi wa Emergency Bridge Parts zimetengwa Shilingi Milioni 9,587.000.

Mheshimiwa Spika, barabara ya New Bagamoyo (Kawawa Jct – Tegeta Km 17.1) imetengewa Shilingi Milioni 1,013.000, Barabara ya Kyaka – Bugene – Kasulo (km 178)zimetengwa Shilingi Milioni 2,446.000. Aidha, barabara ya Isaka – Lusahunga (km 242) na Lusahunga – Rusumo na Nyakasanza – Kobero (km 150) zimetengwa Shilingi Milioni 8,766.000.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Manyoni – Itigi – Tabora (km 264) imetengewa Shilingi Milioni 8,711.000 na barabara ya Korogwe – Handeni (km 65) Shilingi milioni 2,576.000 imetengwa. Aidha, barabara za Mikoa zimetengewa Shilingi Milioni 12,391.116. Pia barabara ya Handeni – Mkata (km 54) imetengewa Shilingi milioni 1,817.000.

Mheshimiwa Spika, barabara za kupunguza Msongamano wa Magari Katika Jiji la Dar es salaam (km 109.35) ikiwa ni pamoja na Flyovers na Makutano ya Barabara zimetengwa Shilingi Milioni 30,157.933. Barabara ya Dar es Salaam – Chalinze – Morogoro (km 200) sehemu ya Dar es Salaam – Chalinze (km 100) kwa kiwango cha "Expressway" kiasi cha Shilingi milioni 2,450.000 kimetengwa kwa ajili ya kazi ya upembuzi yakinifu, maandalizi ya ujenzi na ukarabati wa sehemu ya Mlandizi – Chalinze (km 44.24). Aidha, Daraja la Kigamboni na Barabara ya Maingilio zimetengwa Shilingi Milioni 2,215.000. Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na NSSF ambapo Serikali inachangia asilimia 40 na NSSF wanachangia asilimia 60.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Ndundu – Somanga (km 60) zimetengwa Shilingi Milioni 3,598.260. Pia barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupilo – Malinyi – Londo – Lumecha/ Songea (km 396) imetengewa Shilingi Milioni 533.851. Aidha, barabara ya Tabora – Ipole – Koga – Mpanda (Km 359) Shilingi Milioni2,941.000 zimetengwa.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Makutano – Natta – Mugumu/ Loliondo – Mto wa Mbu (km 452) zimetengwa Shilingi Milioni 3,897.000. Aidha, barabara ya Ibanda – Itungi/ Kiwira Port (km 26)Shilingi Milioni 405.000 zimetengwa. Pia barabara ya Tanga – Horohoro (km 65) Shilingi milioni 53.000 zimetengwa.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Nzega – Tabora (km 114.7) zimetengwa Shilingi Milioni 5,336.000. Pia barabara ya Sumbawanga – Mpanda – Kidahwe (km 438) Shilingi Milioni 11,692.000 zimetengwa. Aidha, barabara ya Nyanguge – Musoma (km 183) na Mchepuo wa Usagara – Kisesa (km 17) na Bulamba – Kisorya (km 51) zimetengwa Shilingi Milioni 8,957.000. Upande wa barabara ya Magole – Mziha (Magole – Turiani km 48.8) imetengwa Shilingi Milioni 2,495.00.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Mwigumbi – Maswa – Bariadi – Lamadi (km 171.8) (Bariadi – Lamadi km 71.8) zimetengwa Shilingi Milioni 4,247.000. Pia barabara ya Tabora – Ipole – Rungwa (Ipole – Rungwa km 173.2) imetengewa Shilingi Milioni 504.000. Aidha, barabara ya Kidahwe – Kasulu – Kibondo – Nyakanazi – (km 310) zimetengwa Shilingi Milioni 7,086.000.

Mheshimiwa Spika, barabara ya mchepuo kuingia Uwanja wa Ndege wa Mafia (Mafia Airport Access Road km 14) zimetengwa Shilingi Milioni 1,001.000. Pia barabara ya Chuo Kikuu cha Dodoma (km 12) imetengewa Shilingi Milioni 1,216.000.

Mheshimiwa Spika, Fedha za Mfuko wa Barabara zimetengwa Shilingi Milioni 606,640.000. Fedha hizi ni kwa ajili ya matengenezo na ukarabati wa barabara, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, udhibiti wa uzito wa magari, usalama barabarani na mazingira na kazi zinazohusika na ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara.

Mheshimiwa Spika,barabara ya Tunduma – Sumbawanga (km 222.8) imetengewa Shilingi Milioni 2,450.000. Pia barabara ya Kagoma – Lusahunga (km 154) zimetengwa Shilingi Milioni3,890.000. Aidha, barabara ya Arusha – Namanga (km 105) Shilingi Milioni903.000 zimetengwa. Barabara yaSingida – Babati –Minjingu - Arusha (km 321.5) imetengwa Shilingi Milioni 1,535.340.

Mheshimiwa Spika,barabara ya Msimba – Ruaha/Ikokoto Mafinga – Igawa (km 655.3) imetengewa Shilingi Milioni 11,893.763. Aidha, barabara ya Korogwe – Mkumbara – Same Shilingi Milioni 8,953.316 zimetengwa. Ujenzi wa barabara ya Mbeya – Makongolosi (km 115) umewekewa Shilingi Milioni 5,405.000

Mheshimiwa Spika,barabara ya Chalinze – Segera - Tanga (km 244.9) zimetengwa Shilingi Milioni 693.000. Pia barabara ya Itoni – Ludewa – Manda (km 211) Shilingi Milioni 1,783.000 zimetengwa.Aidha,daraja jipya katika Mto Ruvu (Ruvu Chini) kwenye barabara ya Bagamoyo – Msata limetengewa Shilingi Milioni 284.000. Barabara ya Dodoma – Iringa (km 260) Shilingi Milioni 4,234.318 zimetengwa.

Mheshimiwa Spika,barabara ya Dodoma – Kondoa – Babati (km 261) Shilingi Milioni 15,722.272 zimetengwa. Barabara ya Masasi – Songea – Mbamba Bay (km 623.3) imetengewa Shilingi Milioni 34,896.165. Aidha, Ujenzi wa Makao Makuu ya Wakala wa Barabara umetengewa Shilingi Milioni 2,157.000. Pia Ujenzi wa barabara ya kuingia Uongozi Institute Shilingi Milioni 612.796 zimetengwa.

Mheshimiwa Spika, Usalama Barabarani umetengewa Shilingi Milioni 2,124.000. Pia Usalama, Mazingira na Marekebisho ya Mfumo Shilingi Milioni 226.000 zimetengwa. Aidha,Menejimenti na Utunzaji wa Mazingira imewekewa Shilingi Milioni 220.836

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2015/16, Mfuko wa Barabara unatarajiwa kukusanya jumla ya Shilingi 866,630,000,000.00. Kati ya fedha hizo, Wizara ya Ujenzi na Taasisi zake imetengewa Shilingi 606,640,000,000.00. Kwa upande wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI kiasi cha Shilingi 259,990,000,000.00 kimetengwa.

Maelezozaidi na Mpango wa Matengenezo ya Barabara kwa fedhaza Mfuko wa Barabara zilizotengwa kwa ajili ya Wizara ya Ujenzi naWakala wa Barabara (TANROADS) na kazi zitakazofanyika kwa Mwaka waFedha 2015/16 vimeonyeshwa katika Ukurasa173 – 186 na Viambatisho Na. 3, 4 na 5A hadi 5E katika Kitabu chaHotuba yangu ya Bajeti.

Mheshimiwa Spika, Mpango wa Utekelezaji Kazi katika taasisi zilizo chini ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2015/16 ambazo ni pamoja na Wakala wa Barabara, Wakala wa Majengo ya Serikali, Wakala wa Ufundi na Umeme, Bodi ya Mfuko ya Barabara, Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Bodi ya Usajili wa Makandarasi, Baraza la Taifa la Ujenzi , Vikosi vya Ujenzi, Chuo cha Ujenzi Morogoro, Chuo cha Matumizi ya Teknolojia Stahiki ya Nguvukazi (Appropriate Technology Training Institute – ATTI) – Mbeya, Kituo cha Usambazaji wa Teknolojia Katika Sekta ya Ujenzi na Usafirishaji (Tanzania Transportation Technology Transfer Centre), Masuala Mtambuka yameelezwa kwa kina katika Kitabu cha Hotuba yangu ya Bajeti ukurasa 186 – 200.

SHUKURANI

Mheshimiwa Spika, napenda nitumie nafasi hii kukushukuru wewe Mheshimiwa Spika, Naibu Spika na wenyeviti kwa kuiongoza Bunge letu hili kwa weledi mkubwa. Aidha, niwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote wa Bunge hili tukufu na kipekee kuishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwa ushauri wao wenye tija katika kuendeleza sekta ya ujenzi.

Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii pia kuzishukuru Nchi na Mashirika mbalimbali ya Kimataifa walioendelea kushirikiana nasi katika kutekeleza programu na mipango yetu katika kuendeleza Sekta ya Ujenzi. Washirika hao ni pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Benki ya Dunia (WB), Japan (JICA), Korea Kusini, Abu Dhabi Fund, Denmark (DANIDA), Marekani (MCC), Uingereza (DFID), Jumuiya ya Nchi za Ulaya (EU), Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID), Kuwait Fund, OPEC Fund, Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Sekretarieti ya Jumuiya ya Nchi za SADC.

Mheshimiwa Spika, kwa dhati kabisa napenda kuwashukuruviongozi wenzangu katika Wizara nikianzia na Mhe. Eng. Gerson H. Lwenge (Mb.), Naibu Waziri; Eng. Mussa I. Iyombe, Katibu Mkuu; Eng. Joseph M. Nyamhanga, Naibu Katibu Mkuu; Wakuu wa Idara/Vitengo; Wenyeviti wa Bodi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi; Viongozi wa Taasisi na wafanyakazi wote wa Wizara ya Ujenzi na Taasisi zake kwa kujituma katika kutekeleza majukumu tuliyopewa na taifa.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kuwashukuru wadau wote wa Sekta ya Ujenzi, ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari ambao wametupa ushirikiano wa kutosha katika kuendeleza Sekta hii. Nitumie fursa hii pia kuishukuru Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kwa kuchapa hotuba hii kwa wakati. Nawashukuru pia wapiga kura wangu wa Jimbo la Chato kwa ushirikiano wao mkubwa walioutoa kwangu nikiwa mbunge wao. Aidha, napenda pia niishukuru familia yangu kwa kunifariji na kuniombea wakati nikitekeleza majukumu yangu ya kitaifa.

Mheshimiwa Spika, hotuba yangu hii inapatikana katika tovuti ya Wizara ya Ujenzi – (www.mow.go.tz).

MAOMBIYA FEDHA KATIKA MWAKA WA FEDHA 2015/16:

Mheshimiwa Spika, ili Wizara iweze kutekeleza majukumu yake ya kuendeleza Sekta ya Ujenzi, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla ya Shilingi 932,715,351,000.00 kwaajili ya matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2015/16. Kati ya fedha hizo, Shilingi 42,142,581,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambazo zinajumuisha Shilingi 36,778,993,000.00 za Mishahara ya Watumishi na Shilingi 5,363,588,000.00 kwa ajili ya Matumizi Mengineyo. Shilingi 890,572,770,000.00 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleoambazo zinajumuisha Shilingi 198,360,000,000.00 fedha za ndani, Shilingi 606,640,000,000.00 za Mfuko wa Barabara na Shilingi 85,572,770,000.00 ni fedha za nje.

MUHTASARIWA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI KWA MWAKA WA FEDHA 2015/16

Matumizi ya Kawaida

MAELEZO
KIASI (SHILINGI)
Mishahara

36,778,993,000.00

Matumizi Mengineyo

5,363,588,000.00
Jumla Fedha za Matumizi ya Kawaida

42,142,581,000.00

Fedha za Maendeleo

Fedha za Ndani za Miradi ya Maendeleo

198,360,000,000.00
Fedha za Nje za Miradi ya Maendeleo

85,572,770,000.00
Fedha za Mfuko wa Barabara

606,640,000,000.00
Jumla Fedha za Maendeleo

890,572,770,000.00
JUMLA YA FEDHA ZA MATUMIZI YA KAWAIDA NA MAENDELEO

932,715,351,000.00

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

Naombeni basi hata Link tu nisikilize aiseeee, natamani hizi clips zingekuwa zinatembea kwenye Whatsapp hawa jamaa nina uhakika wangetoka roho
 
Ndio mana nasema kwamba kwa hasa mkoa wa Kigoma atakayeichagua CCM Mungu amlaani kwa sababu tulishadanganywa saaana, lakini mpaka leo ukitaka kusafiri unabidi utoke kwako na koleo na viatu vya tope mana lazima ukutane na misukosuko, iwe masika au kiangazi hukuna tofauti. Kikwete amemaliza barabara aliyowaahidi waliompigia kura Kigoma haipo, sijui yatawapigia kura tena au?
 
nsuka
Mkuu Kigoma si Dubai huko?

Magufuli ana mbwebwe sana halafu wabunge wa CCM wanaunga mkuno hoja 100%, baadae anaanza kulalamika hadi kengele inalia.
 
hivi mbunge yule viti maalumu wa maswa na mkuu wa wilaya aliechangia mwanzo ni nani??

maana amesema barabara ya mwigumbi to bariadi tayari imeshaanza.

nipeni jina limenipita plz
 
Waziri wa Ujenzi ndugu John Pombe Magufuli leo amewasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake ya ujenzi mnamo majira ya saa nne na nusu asubuhi kwa muda wa Afrika ya Mashariki.

Katika hotuba yake ambayo ni ya mwisho kwake katika uhai wa serikali ya awamu ya nne, ameainisha mipango na mafanikio katika wizara hiyo kama vile ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, madaraja, nyumba za watumishi wa serikali pamoja na vivuko.

Ameainisha miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara na madaraja ambapo hadi kukamilika kwake, zinahitajika zaidi ya trilion nne za kitanzania. Aidha ametumia michoro mbalimbali na ramani kuonyesha miradi iliyopo kwenye mpango huo wa ujenzi katika wizara yake.

Kwa sasa anaomba zaidi ya bilioni 932 ili kukamilisha miradi iliyopo kwenye mpango wa sasa.

===updates===
Hotuba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni imewasilishwa na mh. Mkosamali ambapo hotuba yake imejikita katika madeni yanayodaiwa na makandarasi katika wizara hiyo ambapo madeni hayo yanakadiriwa kuwa zaidi ya bilioni 800, kiasi ambacho ni karibia kiasi kinachoombwa na wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
​Sasa hili linahitaji kamati kweli?mi naona ni jambo lisilowekezana,maana wakandarasi wakilipwa hiyo Bil 800, jamaa atabaki na Bil 132
 
Back
Top Bottom