Yanayojiri bungeni Dodoma leo tarehe 27 Mei, 2015

Madani ya makandarasi karibu ni sawa na bajeti nzima ya wizara yako----800+ Billions vs 900+ billions respectively. Kuwa mkweli utazilipaje katika hali ya kifedha ya taifa hili? Unadangnya mchana kweupeeeeeeeeeeeeeeee
Anaongea urongo
 
ninaangalia bunge, nimeona hoja za mh matiku binti mdogo kabisa akiwa na msigwa, anabishana na mbunge wa nzega dr. kigwangala na ole sendeka. lakini ninavyomwona mh naibu spika ndugai anaonekana anafanya utani utani mwingi sana, hayuko serious, hivi kwanini mama makinda asikalie kile kiti? kwanini watu wazima wanakuwa wanaongea kichama zaidi badala ya walau kuficha ukada?yaani makinda kamzidi ndugai mbali sana jamani.
 
Hivi hujui kuwa wabunge wana dharau sana?
Hawapo pale kwa ajili ya wananchi, wapo kurudisha gharama zilizowawezesha kuingia bungeni.
 
Mbunge kutokuwepo bungeni bila sababu ya msingi sana na bado anakinga mkono posho ya vikao ni ufisadi. Kwa hiyo pata picha nchi hii ina mafisadi wangapi
 
Hao ndio wawakilishi wa wananchi pole mama yetu TZ siku hizi bwana kila kitu kimekuwa siasa kiukweli inasikitisha sana watu tumewatuma wakatuwakilishe badala yake ndio unayo yaona, yaani hizo ndio akili za wawakilishi wetu inshort hao jamaa wa mjengoni awatutendei haki, wengi wa viongozi wetu wana uwezo wa kuongoza familia zao wala wasikupe shida utaumia bure ndivyo walivyo, wote wako tenga moja, hakuna mwenye afadhali. Waliopo hatuwataki tunao wataka hatuwaamini, pigania familia yako achana nao.
 
Mambo mengine lazma tuseme ukweli...tuache ushabiki usio na maana....sote tunaamini kambi ya upinzani kazi yao ni hiyo aliyoifanya mkosamali ila kiukweli hii wizara imefanya kazi kubwa sana asilimia zaid ya 80 ya barabara ipo katika kiwango kizuri na cha kupitika...zile barabara zote korofi nchini zimejengwa tena kwa kiwango kizuri..... Mkosamali anataka barabara zilizo kwenye mipango ya utekelezaji, nani asiyejua uwezo wa nchi zinazoendelea tena kubwa kama tanzania uwezo wake katika kutekeleza miradi mikubwa kama hii....tuache ushabiki na unafiki usio na maana penye jambo zuri tujaribu kusema....halafu watanzania tunaofaidika na barabara hizo tulizozipigia kelele wenyewe leo tunakuja kwenye mitandao ya kijamii kuponda....THIS IS TOTALY UKWARD......HONGERA MAGUFULI KWA KAZI KUBWA MLIYOIFANYA KIKUBWA ENDELENI KUTEKELEZA MAJUKUMU YENU KWA SPIDI ZAIDI


Hizo barabara unazosema zilizojengwa kwa kiwango kizuri ni za wapi? Ni kuwa huoni ajabu kuwa barabara zinajengwa hazina hata miaka miwili zimechoka wakati kuna barabara watu walijenga kipindi cha mwalimu bado zipo? Nani sas ndiyo analeta ushabiki hapo?

Hebu tufikirie critically cabla ya kusema.
 
Anatekeleza sera na Ilani ya CCM,ukitaka kukosa na serikali ya CCM kuwa MKWELI utaipata joto ya JUA! Na mifano ipo muulizeni Mh.Lyatonga ni shahidi! Kwahiyo anachofanya Magufuli,utii kwa serikali yake sikivu!
 
Bunge letu linasikitisha sana, Hoja ya Ester Matiko ya kutaka maelezo ya gharama ya kununua MV Dar es salaam ambayo kwa mujibu wa waziri ni TZS 7.9billion akilinganisha na gharama ya Ferry ya Azam ambayo ilinunuliwa kwa TZS 4billion. Ajabu ni kuwa feri ya Azam inaaenda Zanzibar kwa saa moja na nusu na inabeba watu 500 na ni nafuu ukilinganisha na MV Dar inayoenda Bagamoyo kwa masaa mawili na inabeba watu 300. Badala ya kujadili hiyo difference wanaanza kimwambia kuwa hajaipanda ameambiwa na watu so hajafanya utafiti,sasa sielewi alitakiwa kufanya utafiti upi wakat waziri mwenyewe kathibitisha hilo.
 
May 27th 2015



Kama unadhani mipasho ipo katika nyimbo za taarabu tu, hakika utakuwa umekosea sana.

Hapa bungeni kauli zenye utata, kejeli na dhihaka ni mambo yaliyoshika hatamu tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti Mei 12.

Unajua ilikuwaje? Juzi usiku wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, waziri wa wizara hiyo Sofia Simba ni kama alijisahau kuwa yupo bungeni.

Mwanamama huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya CCM (UWT) baada ya kubanwa na wabunge wa upinzani kuhusu suala la taasisi zisizo za kiserikali zilizosajiliwa chini ya wizara hiyo, aliwafananisha wabunge na upinzani na mtu ‘anayewashwa'.

Sijui bwana sababu ya waziri huyo kudai wabunge hao wanawashwa na sina hakika huko kuwashwa ni kwa aina gani ingawa yeye mwenyewe alidadavua baadaye kwamba hata akili ya mtu inaweza kuwasha.

Sitaki kunukuliwa vibaya bwana, kwani wewe mtu akikuambia unawashwa wakati hajakuona ukijikuna unadhani atakuwa anamaanisha nini?


Udaku Special Blog
 
Back
Top Bottom