Nilikuwa namtazama na kumsikiliza Mh. Rose Kirigini mbunge wa viti maalumu wa CCM na mkuu wa wilaya ya Maswa wakati akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya ujenzi katika television akisema uongo wa waziwazi kabisa dhidi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami inayotoka Mwigumbi - Maswa - Bariadi - Lamadi, kwamba mkandarasi yuko site tayari kuanza ujenzi. Nasikitika sana kwamba amejidanya yeye mwenyewe, kakidanganya chama chake cha CCM na zaidi sana kawadanganya wananchi wa Maswa mchana kweupe.
Ukweli ni kwamba hakuna ujenzi wowote unaoendelea na wala hata dalili tu kuwa labda mkandarasi anafanya maandalizi ya kuanza ujenzi hakuna kinyume na yeye alivyosema kuwa kampuni ya kichina ya CHICO iko site. Mimi nashangaa sana viongozi kama hawa wanatuonaje sisi wananchi iwapo wanasimama tena kwenye forum muhimu na ya kipekee kama bunge kusema uongo wa wazi kama huu badala ya kuiambia ukweli serikali ili iwatekeleze wajibu wake.
Ni kweli kuwa wananchi wa mkoa wa Simiyu na hususani wilaya za Bariadi na Maswa tangu mwaka 2005 na kisha 2010 waliahidiwa na serikali hii ya CCM chini J.M. Kikwete kujengewa barabara hii kwa kiwango cha lami.Inawezekana kabisa kazi za awali kama upembuzi yakinifu (feasebility study) zilishafanyika, lakini ni ukweli ulio wazi pia kwamba na hasa kwa wananchi wa wilaya kongwe ya Maswa iliyozaa wilaya za Kishapu, Meatu, Bariadi na sasa ni mkoa mpya wa SIMIYU , hakuna ujenzi wowote wa kiwango cha lami ambao umekwisha kuanza achilia mbali kuona tu maandalizi ya vifaa vya mkandarasi vikiwa ktk site kama ambavyo mheshimiwa huyu amesema kwa udanganyifu!!.
Nifahamuvyo mimi ni kuwa, mwananchi wa kawaida (wapiga kura) wala hata haelewi nini maana ya upembuzi yakinifu na kwake yeye hiyo hata si sehemu ya ujenzi wa barabara. Kwa mwananchi wa kawaida kwake yeye ujenzi wa barabara ni kuona ma - greda na malori yakiwa site lami ikimwagwa na si kama ambavyo huyu mbunge wa CCM tena akiwa ni mkuu wa wilaya ya wananchi haohao anaowadanganya!.
Kwa wasiofahamu, ni kuwa, wilaya ya Maswa ina majimbo ya uchaguzi mawili; Maswa Magharibi mbunge wake ni JOHN MAGALLE SHIBUDA (CHADEMA) na Maswa mashariki ni SYLEVESTER KASULUMBAYI (CHADEMA). Sina hakika kama hawa jamaa walikuwepo au hawakuwepo bungeni leo, na kama walikuwepo sijui ni kwa nini walimwacha tu huyu mama akiwadanganya wananchi wao mchana kweupe!...Na nasikia huyu mama anataka kugombea ubunge katika moja ya majimbo haya na kwa uongo huu sidhani kama CCM watayarudisha tena haya majimbo, wamekosa kura tayari!!
Mimi nadhani mh. Rose Kirigini na mkuu wa wilaya ya Maswa hebu tu awaombe radhi wananchi wa wilaya yake kwa kuwaona wajinga, hawaoni na hawana ufahamu kwamba serikali haijaanza ujenzi wa barabara hii ya Mwigumbi - Maswa - Bariadi kwa kiwango cha lami!!