Kanina
JF-Expert Member
- May 26, 2013
- 277
- 81
Katika kipindi cha maswali kwa waziri mkuu leo bungeni, Kafulila amemuuliza Mh. Pinda juu ya Serikali kuendelea kumlipa Seti wa IPTL zaidi ya shilingi Bilioni 5 kila mwezi kama capacity Charges, wakati umiliki wake ni feki, pamoja na mahakama kudhibitisha hivyo!
Pinda hakujibu hilo baada ya Madame Spika, kumzuia kutoa majibu ya suala hilo kwa sababu 'eti' ni swali jipya.!
=============
Lissu: Niwashukuru wapiga kura wangu na watanzania kwa ujumla kwa kunipa fursa hii na hii itakuwa hotuba yangu ya mwisho kama msemaji mkuu kambi ya upinzani juu ya katiba na sheria, naomba kwa ruhusa yako nifanye rejea katika misha ya miaka mitano ya bunge la kumi.
Rais aliahidi kuwa 26/4/2014 Tanzania itakuwa na katiba mpya, leo ni wiki ya tatu tangu ahadi mpya ya April 30 kupita. Uhakika pekee tulionao ni rais kuondoka bila katiba mpya alioahidi, hii ni serikali iliyoshindwa. Sisi tuliweka mpira kwapani na kuondoka, hivyo waliobaki ni chama kilichoshindwa. Swali analotakiwa waziri mkuu kulijibu ni lini kura ya maoni itapigwa na kwa sheria ipi.
Kibona: Kuna mama mmoja Ileje, peke yake anaenda kilomota 90 anapanda pikipiki eti hakimu mfawidhi kashilia magari mawili, nataka gari liende Ileje. Naomba mheshimiwa waziri aliengalie suala la nyumba ya hakimu wa wilaya.
Rashid Ali: Wananchi wa Tanzania wamepoteza imani na vyombo hivi kutokana na kutotendewa haki sawa kwa wote, nimeshangazwa mwezi uliopita mahakama ya Kisutu. Prof Lipumba alifika mahakamani saa mbili asubuhi, tumekaa mahakamani hadi saa tisa jioni hakimu haonekani, katika utawala bora ni kuwatesa wananchi, watu wako nje hawaitwi na mahakama ndio msimamizi mkuu wa haki za wananchi.
Nirejee kusema, kuna wananchi kutoka ZNZ wamekamatwa kutokana na pembe za ndovu, wamewekwa ndani mwaka mmoja na nusu, wamefutiwa mashtaka halafu wamekatwa tena na polisi. Haki sawa kwa wote na kwa wakati, wizara hii imeshindwa kuendesha shughuli za kesi, hakuna mtu aliefikishwa mahakamani kesi za ufisadi.
Matiku: Nianze na matatizo yaliyopo Rolya, hakuna mahakama ya wilaya hivyo watu wanafata mahakama Tarime na kwa Jiografia ya kule ni usumbufu mkubwa kwa wananchi. Watu hawalazimishwi kuchangia maabara lakini kwa nini mahakama inatumika kulazimisha, iliwapaka kifungo cha miezi mitatu au faini laki mbili.