Lissu anasema kuwa wameletewa jedwali la marekebisho ya kanuni ya bunge maalum. Kwamba marekebisho kuhusu kanuni za 14, 32,33,35,37,38,58,61(1),64(1),85(4). Anasema kuwa mabadiliko haya yanaletwa na Katibu wa Kamati ya Uongozi. Alisema kuwa hiyo si sahihi kwa vile kanuni inaeleza bayana. Anasema kuwa kanuni hazina hata wiki tatu na bado zinaanza kuchakachuliwa. Anasema kuwa viporo vya 37 na 38 ndivyo vinavyotakiwa viwasilishwe. Alisema kuwa hayo marekebisho hayatakiwi kuwasilishwa. Pia anasema kuwa kamati ya uongozi haina mamlaka ya kuleta mabadiliko ya kanuni. Anasema kuwa hii takataka, uchafu nk hataki iingizwe kwenye bunge hili. Mwenyekiti anasema kuwa tuhuma za Tundu Lissu ni nzito na amezitoa bila yamkuwa na karatasi ya marekebisho hayo. Anasema kuwa Kamati ya Uongozi imefanya kazi ya kuandaa kazi za kila siku. Anasema kuwa kamati ya kanuni ndiyo inapaswa kuwasilisha marekebisho ya kanuni. Anasema kuwa tusubiri hicho kinachopaswa kuwasilishwa na kikionekana ndipo bunge litaamua.