Yanayojiri Bungeni Dodoma: Alhamisi, January 29, 2015

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Alhamisi, January 29, 2015

Kwahiyo huo mjadala umeazimia maamuzi gani?
Ndiyo tayari hoja imeshajadiliwa?
 
Kwahiyo kiongozi wajuu aliyetoa maelekezo ili prof Lipumba apigwe tu kajulikana?
 
Duuu Lusinde noma sana...eti lazima watu wajue kachumbari ina pilipili na watu lazima wajue siasa zina gharama zake....duuu huyu jamaa ni kiboko
 
Ni aibu kwa mtu aliyepita Law School of Tanzania asijue nini maana ya Reasonable Force ilhali First Year wa LL.B anaifahamu.Namwomba Principal,Hon.Ndika J. Kumnyang'anya Bw.Sadifa Cheti cha Kuhitimu,na pia kufukuzwa kwenye Uwakili Kama ni Wakili!
Naona Aibu
 
Hapa tu ndipo huwa nashangaa uumbaji Wa Mungu. Yaani namtafakarigi Lusinde nabaki nacheka tu maana hata yeye hajielewi.

Sijui wapigakura wake wakoje kichwani Kama walimchagua Lusunde Kama chaguo bora kuliko Malecela....

Walimchoka babaye LeMutuzi,bahati ya mtende ikamwangukia Lusinde
 
Husika na kichwa hapo juu,

Ni dhahiri kwamba umakini wa viongozi wa serikali katika kutoa kauli bungeni juu ya maswala magumu kwa mustakabali wa nchi yetu,kauli zao zimekua na ututa kama sio upotoshaji na udanganyifu mkubwa:

Nirejee kauli za mh. Chikawe juu ya tuhuma za jeshi la polisi kutumia nguvu kubwa juu ya chama cha wananchi CUF,kwamba prof. Ibrahim Haruna Lipumba hakutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ndio chanzo cha polisi kutembeza kipigo:

Jamani hivi kweli mh waziri hata vyombo vya habari hutazami? Na kama hutazami kwanini usifanye hata kautafiti kabla ya kuja kutoa kauli zinazo idhalilisha serikali? Maana kila mtu anajua kilichotokea juu ya unyama wa jeshi la polisi juu ya viongozi wa CUF.

Mimi napata mashaka kwenu ninyi mnaomzunguka baba mheshimiwa rais,kwamba hivi jinsi mambo yalivyo nchini ugumu wa maisha ukiukwaji wa misingi ya sheria na ukandamizwaji wa maskini kunyimwa haki zao unatokana na ninyi kumwangoza mh rais vibaya kwa kumpotosha.

Baba mheshimiwa rais wangu,waangalie sana hawa wanaokuzunguka,juu ya ushauri wao kwako na utendaji wao kazi hawa ndio wanakiangamiza chama kwa utendaji wao usio na weledi,haiwezekani waziri kukurupuka na kutoa kauli za reja reja katika mambo yanayogusa amani ya nchi yetu.

Mwisho:

Nivyema wewe kama rais ukapitisha fagio ndani ya jeshi la polisi na kuwaondoa wale watendaji wasiotimiza wajibu wao kwa kukubali kutumiwa na kikundi kidogo kisichohitakia amani nchi yetu,na kukifanya chama kionekane kwamba ndio kimelituma jeshi kufanya mambo kinyume na haki za binadamu:

Nb: Tanzania ni nchi ya watu wa vyama vyote ila nchi yetu haina dini kabila wala chama ila watu wake wana dini,kabila,na vyama,ilituijenge nchi yetu tanzania ni vyema haki na usawa vikapewa kipaumbele juu ya makundi yote,bila kubagua na haki kutolewa upande mmoja. Mungu ibarika Tanzania.
 
Wadau, natumai kuwa mnaendelea kufuatilia mjadala wa bunge linaloendelea mjini Dodoma.

Katika maswali ya papo kwa papo, Freeman Mbowe alionesha wasiwasi juu ya muda wa siku 90 uliotengwa na Tume ya Uchaguzi wa kuwaandikisha wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015. Katika maelezo yake, Mbowe amesema kuwa Kit moja ya BVR ina uwezo wa kuandikisha watu 22 tu kwa siku hali ambayo anasema kuwa itakuwa vigumu kuandikisha takriban watu milioni 24 wanaotarajiwa kuandikishwa. Hivyo alipendekeza Tume ipate fedha na muda wa kutosha ili iweze kuandikisha watu wote.

Hata hivyo, pamoja na Waziri Mkuu kukubaliana na Mbowe juu ya umuhimu wa Serikali kuipatia Tume fedha za kutosha ili iweze kukamilisha kazi yake kwa wakati, Waziri Mkuu anasema kuwa hawezi kubishana na Mbowe juu ya uwezo wa mashine hizo ila taarifa anazotoa juu ya uwezo wa mashine hizo yawezekana kuwa zisiwe za kweli. Waziri Mkuu anasema kuwa kwa taarifa alizopata na Tume ni kwamba, awali walijua kuwa mashine hizo zilikuwa na uwezo wa kuandikisha watu 70. Hata hivyo, uzoefu waliopata kwenye wilaya za majaribio za Mlele, Kinondoni na Kilombero ni kwamba imebainika kuwa mashine moja ina uwezo wa kuandikisha mara mbili ya makadirio ya awali.

Kwa maelezo haya ya Waziri Mkuu, ni wazi kuwa Mbowe alikusudia kulidanganya taifa kwa malengo anayoyajua

Nawasilisha



Yaani mkuu nimerudia mara sita kusoma hii thread lakini nashindwa kuelewa una maanisha nini!!!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
kwa kweli chikawe pale aliteleza,hata sura yake ilikuwa inaonyesha kwamba anasemaje uongo.
ni jambo LA kushangaza waziri anafanganya huku wabunge wengine wakimpigia makofi.
pia inasikitisha mbunge kusimama na kusema kwamba for the first time police wamefanya kazi nzuri ya kumpiga kiongozi Wa upinzani.
hii inadhiirisha wazi kwamba chama tawala IPO taabani kisiasa kiasi cha kuanza kutumia polisi kuwadhibiti wapinzani.
ccm jiandaeni ki saikolojia kuwa wapinzani, kwa hali hii mnabomoa daraja Kati ya police na jamii.
 
ifike sehemu polisi wakipiga watu na mabomu nasi wananchi tukawanyonge familia zao zinazo ishi mitaani. Hii itakuwa ni dawa kwa hawa polisiccm

mkuu punguza hasira ni kweli mambo haya yanachochea chuki kwa wananchi,cha msingi ni kupaza sauti zetu viongozi wasikie na dunia isikie bila kuumizana na kulipizana visasi,kutumia njia za udugu na upendo hili hata hawa wanaotumiwa kuwapiga ndugu zao nafsi zao ziwasute na kubadilika,
 
Inaelekea mheshimiwa waziri wetu anaulemavu wa kusikia au hakielewi kishwahili alichokuwa anaongea Mwenyekiti wa CUF akiwaambia wana CUF kuwa maandamano na mkutano haupo. Nadhani apelekwe kwa daktari.
 
kwa kweli chikawe pale aliteleza,hata sura yake ilikuwa inaonyesha kwamba anasemaje uongo.
Ni jambo la kushangaza waziri anafanganya huku wabunge wengine wakimpigia makofi.
Pia inasikitisha mbunge kusimama na kusema kwamba for the first time police wamefanya kazi nzuri ya kumpiga kiongozi wa upinzani.
Hii inadhiirisha wazi kwamba chama tawala ipo taabani kisiasa kiasi cha kuanza kutumia polisi kuwadhibiti wapinzani.
Ccm jiandaeni ki saikolojia kuwa wapinzani, kwa hali hii mnabomoa daraja kati ya police na jamii.

nikweli kabisa ndugu ifike maali hawa mawaziri wakawajibika kwa kauli zao za uongo uongo,pili huyu kibajaji tumsamehe bure kwani hali ngumu za maisha ndizo zilizo mwasiri kiakili,

huyu ali hishi mitaani kwa hiyo husitegemee lugha zake zikawa na ustaharabu,hili ni tatizo la mfumo wake wa kifikra ndipo uwezo wake wa kufikiri ulipo hishia,angetafuta hata kukaa na wazee wenye busara ili anyonye busara zao,
 
inaelekea mheshimiwa waziri wetu anaulemavu wa kusikia au hakielewi kishwahili alichokuwa anaongea mwenyekiti wa cuf akiwaambia wana cuf kuwa maandamano na mkutano haupo. Nadhani apelekwe kwa daktari.

hawa mawaziri mkuu wamzoea kuhandikiwa hotuba,hawa ni kulatu,na kusinzia bungeni, sasa hao wanao waandikia hotuba wanalenga kuwa dhalilisha,

bila wao kujijua,wewe ukiwa waziri ni kujitafutia semina na visafari safari ili upige hela, ni dilitu na udalali wa 10 pacent ndio unawafanya wapigane vikumbo kungangania uwaziri:
 
inadhihirisha ni mawaziri wa namna gani tulionao, wanaongea kabla ya utafiti, sijui hata vyomb vya habari haangalii
 
Back
Top Bottom