Yanayojiri baada ya MNYIKA (MB) kufika Polisi Singida!

Nadhani Chadema wanabidi wasiwe wanafanya tena chochote kwa kuamini Jeshi letu la Polisi. Wanabidi waajiri waandishi wa habari waiobobea kwenye fani ya upelelezi pia. Vitumike vifaa madhubuti vya kunasa sauti na picha na kuvisafirisha mara tu vinaponasa. Nahisi mpango wa kumwaga fisi na simba wengi huko mabwepande! Ili wasaidie kazi. Mambo haya yanajiweka wazi kila kukicha!
Mungu ibariki Tanzania na wale wote wenye nia nzuri na Taifa letu!

Nakuunga mkono Mkuu! Hili litasaidia hata pale Mahakama zinapoibeba serikali,hatimaye haki iweze kupatikana hata kama na baada ya muda mrefu kiasi gani!
 
Hata Mahakama zetu hapa nchini, hatuna imani nazo tena. Hii ipelekwe kwenye mahakama za kimataifa zinazosimamia haki za binadmu.
 
Kwa mahakama zipi za kupokea ushahidi wa video? polisi na mahakama niwalewale
 
Mrejesho wa Mwisho/Update: Nimemaliza kutoa maelezo ya kurasa 12 pamoja na mambo mengine nimesema wazi kuwa kabla ya mkutano nilipewa taarifa kuwa kuna kikundi cha vijana wa CCM kimepangwa kuvuruga mkutano, hata baada ya kuwaambia Polisi wahakikishe ulinzi, Polisi waliwaachia vijana hao warushe mawe wakati Bwana Waitara akihutubia.

Taarifa za mauaji tulizipata usiku baada ya kurejea Singida Mjini na zilitolewa na RPC.

Hivyo sifahamu uhusiano wowote uliopo kati ya mauaji na mkutano wa CHADEMA uliomalizika kwa amani. Na nimewaambia sikutoa lugha yoyote ya matusi wala uchochezi bali nilieneza sera na wananchi wakataka turudi tena na tukawaahidi kuwa tulikwenda kwenye maandalizi ya Operesheni Sangara ya Singida nzima!

Nimewaambia, tuna ushahidi wa video na tutautoa mahakamani.

John John MNYIKA,
Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA),
18 Julai, 2012

That is why i like CHADEMA hawabahatishi hata siku moja magamba mpooooooooooooooooooo?
 
members, hebu fikirieni ingekuwa ni mkutano wa CCM halafu wakatokea wanachama wa CHADEMA wakafanya fujo na hatimaye wakauwawa baadhi yao na washabiki wa CCM! Je kesi bado ingekuwa ina sura hii ya sasa? Nadhani CHADEMA wangeshutumiwa kwa kuingilia mikutano ya chama kingine na kufanya fujo. Tena wangeulizwa mbona CCM haijawahi kuwavurugia mkutano wenu kwa kutuma vijana waanzishe fujo? Tena ingesemwa hadi Bungeni kwamba waliouwawa wamejitakia kwa kuingilia mikutano ya wenzao kwa kujaribu kuondoa amani!!!

Tutafakari hayo!!
 
Kesi za kutungwa! Wamkamate aliyewatuma hao wahuni kurusha mawe ktk mikutano - yaani huyo Mbunge Mchemba!! Anyway, Walishakosea, wangemkabidhi Kova 'aigize' uongo mwingine...Polisi hawana la kukuhoji!

Ikiwakwama sio ajabu wapeleke Mahakamani kama jadi yao halafu wakataze isihojiwe maana ipo mahakamani kama wanavyozuga katika kila hujuma zao na failure yoyote pale Govt inayosutwa wakakosa immediate fikra!!

Nchi hii tunayo kazi...!

waliomrushia mawe kikwete kule mbeya hivyo walifanywaje?
 
waliomrushia mawe kikwete kule mbeya hivyo walifanywaje?
Walikua na haki kumrushia mawe kiongoz dhaifu kwan maisha yanazidi kuwa magumu miundombinu hakuna yeye anaenda kuwa sanifu na msafara waliolipana maposho ya mamilioni inauma sana nyie MAGAMBA mnavyowafanyia watanzania na mkomboz wao CHADEMA
 
Mheshimiwa Mnyika anatafutwa kwa udi na uvumba tangu amtaje mkuu wa nchi kuwa ni dhaifu na wabunge wa ccm ni wazembe na Mwigulu alihusika kwenye EPA wanaitafuta roho yake kwa kila njia anatakiwa awe mwangalifu sana kwa anachokula,anachokunywa, akiendesha gari akiongea achague maneno, yaani kifupi awe makini kwa kila sekunde ya maisha yake yupo hatarini sana sana kuliko wakati wowote ule!

Hata yeye amekuwa na kiburi sana tokea kashinda ile kesi yake ya Ubunge dhidi ya Ghumbi. Mnyika kabadilika sana, sio yule wa siku zote.
 
Vyombo vya usalama bila kujijua vinajengea wakati mugumu na chama tawala kwa kuvichonganisha na vyama vya upinzani.
Mpango huu unalengo la kutumika baadaye kuwatisha wanausalama kuhusu mstakabari wa ajira zao baada ya upinzani kuingia madarkani kwani watakuwa wamefanya mambo machafu mengi kwa kushirikiana na chama tawala.Wawe makini sana upepo sio shwari kama wanyoupima kwa bendera.Wajue nchi sio ya chama ni Watu.watu wakisema itawaliwe na nani itakuwa hivyo.
 
mnyika anajua anachokifanya! magamba bwana mtu akiwa str8 mnataka kumpoteza,yana mwisho hayo na ndio ss
 
Thursday, 19 July 2012 07:56
0digg

mnyika-top.jpg
Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika

Neville Meena, Dodoma na
Gasper Andrew, Singida
MBUNGE wa Ubungo (Chadema), John Mnyika jana alihojiwa na polisi kutokana na vurugu zilizosababisha kifo cha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kata ya Ndago, wilayani Iramba, Yohana Mpinga (30).Mnyika ni mmoja wa viongozi wa Chadema ambao walihutubia mkutano huo uliofanyika katika Jimbo la Singida Magharibi.Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi (DCI), Robert Manumba alieleza nia ya jeshi hilo kutaka kumhoji Mnyika kuhusu tukio hilo, lakini hakutaka kuzungumzia kwa undani suala hili akishauri aulizwe Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida.

Mnyika aliyekwenda Singida kuitikia wito wa polisi, alihojiwa na kikosi maalumu cha maofisa wa jeshi hilo kutoka Makao Makuu, Dar es Salaam, ambao wako mkoani humo kuchunguza matukio ya vurugu zilizotokea mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mkutano wa Chadema na kusababisha kifo cha kada huyo wa CCM.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Singida jana, Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema kuwa, Mnyika alifika ofisini kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida jana saa 7.45 mchana kuitikia wito uliotumwa kupitia Ofisi za Bunge.

Makene alimnukuu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Linus Sinzumwa akisema, Mnyika anapaswa kuhojiwa na kikosi maalumu cha maofisa wa Polisi kutoka Dar es Salaam ambacho kwa wakati huo, kilikuwa Ndago kufanya upelelezi wa kitaalamu zaidi kuhusiana na mauaji ya Yohana.
“Kutokana na kauli hiyo, hivi sasa Mbunge Mnyika amepumzika hadi hapo saa kumi jioni, atakapohojiwa na hicho kikosi maalumu, anahojiwa kuhusu nini, hiyo ni siri hakuna anayefahamu,” alisema Makene.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mnyika alisema akiwa katika Ofisi ya RPC Sinzumwa alihoji iwapo alitakiwa kuhojiwa kama mtuhumiwa au shahidi.“Jibu la RPC ni kwamba ni mahojiano ni ya kawaida tu, nilihoji sababu Mwita (Mwikwabe) aliambiwa kwamba ni mahojiano ya kawaida, lakini baadaye aliwekwa ndani na kupandishwa kizimbani,” alisema Mnyika.

Gazeti hili lilipowasiliana na Makene jana saa 11.30 jioni, alisema walikuwa bado hawajaitwa kwenda kuhojiwa na badala yake polisi waliwataka kuendelea kusubiri kwa kuwa maofisa waliokwenda Ndago walikuwa wamekwama njiani.

Bungeni Dodoma
Mapema jana asubuhi kulikuwa na habari kwamba Mnyika amekamatwa na polisi akiwa mjini Dodoma anakohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti, lakini ikabainika kwamba alikwenda mwenyewe Singida kuitikia wito wa polisi.
Mkurugenzi wa masuala ya Bunge wa Chadema, John Mrema alisema jana mjini Dodoma kuwa, Mnyika alikwenda Singida kuitikia wito wa polisi ambao walimwita kupitia Ofisi ya Spika wa Bunge.

Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema kuwa, juzi Bunge lilipokea barua kutoka polisi mkoani Singida ikitoa wito kwa Mnyika kwenda kufanyiwa mahojiano kuhusiana na vurugu zilizotokea katika mkutano mwishoni mwa wiki iliyopita.

“Kweli polisi walifika hapa wakawasilisha barua wakiomba kwamba Mnyika afike Singida kwa ajili ya kuhojiwa na sisi baada ya kuwasiliana na Spika tulimwarifu na ninaamini leo (jana) atakuwa amekwenda huko,” alisema Joel jana.

Chadema walalama
Wakati Mnyika akiendelea kusubiri kuhojiwa, Chadema jana kililalamikia polisi kutochukua hatua dhidi ya watu waliowafanyia fujo kwenye mkutano wao.

“Kaimu Katibu wa Chadema Mkoa wa Singida alifungua kesi dhidi ya baadhi ya watu waliokuwa wakiongoza vurugu za kuvuruga mkutano, lakini mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa, tumeuliza RPC anasema eti analifuatilia,” alisema Makene.

Alidai kwamba vurugu hizo zilifanywa na watu wachache na kwamba majina yao yaliwasilishwa polisi, lakini hakuna hatua zozote zilizochukukiwa.
“Kutoka eneo ambalo tulikuwa tukifanyia mkutano mpaka hapo kituo cha polisi kilipo ni kama hatua 25 au 30 hivi na jalada tulifungua na majina ya watu 12 waliotufanyia fujo tuliyawasilisha,” alisema na kuongeza:

“Lakini tulipowauliza polisi kama kuna hatua zozote walizowachukulia watuhumiwa hao, tumejibiwa kwamba hakuna hata mtu mmoja ambaye ameshakamatwa mpaka sasa.”
 
[h=2]Nukuu ya maandishi ya jumbe za simu za kutishwa kuuawa alizotumiwa Mwigulu Nchemba [/h] 18/07/2012
0 Comments


Baadhi ya wabunge wa CHADEMA, wamehusishwa na mauaji ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa Kata ya Ndago wilayani Iramba mkoani Singida, Yohana Mpinga (30).

Akizungumza bungeni jana, Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba alisema kabla ya mauaji hayo anayoona yalipangwa, alitishiwa kuuawa kwa kutumiwa ujumbe mfupi wa simu na wabunge hao kutokana na mijadala yake bungeni.

Nchemba alitoa madai hayo alipoomba Mwongozo wa Spika akitumia Kanuni ya Bunge ya 47 inayohusu kusitishwa kwa shughuli za Bunge ili kujadili jambo la dharura la Taifa.

Sehemu ya ujumbe huo ambao Spika wa Bunge, Anne Makinda alimzuia kuusoma, unamtaka Mwigulu asijifanye anajua, kwani mwenzake Chacha Wangwe (Marehemu Mbunge wa Tarime) alijifanya anajua na “sasa yuko wapi?” Ujumbe mwingine ulimwambia kuwa skafu ya Bendera ya Taifa anayovaa shingoni, itageuka sanda yake.

Akiomba Mwongozo huo, Nchemba alisema kutokana na tukio la kinyama lililotokea jimboni mwake juzi la kuuawa kwa Mpinga na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA, aliomba Bunge liahirishwe ili suala hilo lijadiliwe kwa kina.

“Naomba tuahirishe Bunge tujadili suala hili, kwa kuwa inaonesha kilichotokea kilipangwa, nilipokea SMS (ujumbe mfupi) katika simu yangu za kunitishia kuuawa kutokana na mijadala ninayochangia bungeni na namba za walionitumia SMS zimebainika kuwa ni za wabunge wa CHADEMA,” alisema Mwigulu.

Alisema namba za simu zilizokuwa zikitumika kumtumia ujumbe huo mfupi alizipeleka Polisi na tayari wabunge hao waliomtishia maisha wamebainika majina yao na hatua zaidi zitachukuliwa.

Pamoja na kukataa kutaja majina ya wabunge hao, Nchemba nje ya Bunge alionesha ujumbe mfupi aliotumiwa ambao unasema:


  1. “Hivi wewe unajiamini nini? Kwa nini unatusonga hivyo? Unadhani nchi hii ni ya CCM milele? “Utajutia kimbele mbele chako. Unadhani ni wewe tu unayejua sana? Ukabila kwenye chama chetu unakuhusu nini, hata kama ni kweli, kwa nini kututia aibu?”
  2. “Hata ufanyeje, 2015 tunaingia Ikulu na mjengoni tutajaa, Wangwe alijifanya kujua kama wewe leo yuko wapi?”
  3. “Bendera unayovaa kila siku shingoni itageuka sanda yako. Kila mtu ana haki ya kuvutia kwake, lakini wewe umezidi. Hatuwezi kuitema keki tuliyokwishaionja”.
  4. “Fahari yako leo, itageuka kilio kwako. Utatutambua.”

Hata hivyo, Spika Anne Makinda alimkatisha Nchemba asiwataje kwa majina wabunge hao waliomtumia ujumbe mfupi wa kutishia kumwua na kumtaka aiachie Polisi ishughulike na jambo hilo, ambapo pia aliukataa Mwongozo wa kuahirisha kikao.
 
Mungu yupi atakayesimama na wauaji?
Gamba mkubwa wewe. Ndo maana umefunguliwa ID mwezi July wkt wa Bunge na Mwigulu ili upost ***** wako sio? Tangu trh 08 July 2012 unapost 176 na zote ni pumba tupu. Aibu yako itakukuta wewe na boss wako 2015. Chama chenu kimeuwa watu wangapi na hakuna aliyekamatwa? Operation ya M4C imezunguka sehemu ngapi iweje hapo kwa Mwigulu ndo zitokee vurugu? Inaonyesha huyu jamaa ni zero brain ndo maana akaandaa vijana wake wafanye fujo. Kuna watu wenye nguvu km Lowassa, Rostam, Chenge, etc na wanakashfa kibao ila hawakuandaa vijana wa kupambana bali walikaa kimya na kuyapokea maneno ambayo yamepita na maisha yanaendelea. Mwambieni Mwigulu ajifunze siasa kwani huo ni utoto, kuandaa watu wafanye vurugu ili kuonyesha vijana wanampenda sana na wana uchungu nae.
 
Back
Top Bottom