Yanayojiri baada ya MNYIKA (MB) kufika Polisi Singida!

Scolari Ndenga

JF-Expert Member
Aug 4, 2008
271
43
Mwito wa Polisi, Singida: Yanayojiri!

Nimefika Singida kuitikia mwito wa Polisi kutoa maelezo kuhusu mkutano nilioalikwa Iramba kwa nafasi yangu ya Mkurugenzi wa Habari na Uenezi.

Nimekutana na RPC, amesema kwamba nisubiri mpaka saa 10:30 alasiri ndiyo nikutane nao kwa kuwa kwa sasa kuna kikosi cha upelelezi toka Dar Es Salaam kimekwenda eneo la tukio. Nimemuuliza RPC maswali mawili;

1. Wameniita kutoa maelezo kama mtuhumiwa au shahidi?
Amenijibu kuwa ni mahojiano ya kawaida.

2. Kwanini mpaka sasa watuhumiwa 12 waliofunguliwa jalada NDG/RB/190/2012 kwa kurusha mawe kwenye mwanzo wa mkutano wakati Bwana Waitara akitoa hotuba ya utangulizi huku polisi wakiachia hali hiyo. Baada ya kufungua jalada na polisi wa juu kupigiwa simu kuwa kuna njama kati ya Polisi na CCM hali ilitulia, Waitara akamaliza hotuba yake, Dkt Kitila akasalimia name nikahutubia kwa amani na kwenda kwenye mkutano mwingine. Mauaji yalitokea baadae mbali na tulipohutubia.

John John MNYIKA,
Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA)
18 Julai, 2012Mwito wa Polisi, Singida: Yanayojiri!

18 Julai, 2012

Chanzo: Status yake katika mtandao wa kijamii, Facebook

Mrejesho wa Mwisho/Update: Nimemaliza kutoa maelezo ya kurasa 12 pamoja na mambo mengine nimesema wazi kuwa kabla ya mkutano nilipewa taarifa kuwa kuna kikundi cha vijana wa CCM kimepangwa kuvuruga mkutano, hata baada ya kuwaambia Polisi wahakikishe ulinzi, Polisi waliwaachia vijana hao warushe mawe wakati Bwana Waitara akihutubia.

Taarifa za mauaji tulizipata usiku baada ya kurejea Singida Mjini na zilitolewa na RPC.

Hivyo sifahamu uhusiano wowote uliopo kati ya mauaji na mkutano wa CHADEMA uliomalizika kwa amani. Na nimewaambia sikutoa lugha yoyote ya matusi wala uchochezi bali nilieneza sera na wananchi wakataka turudi tena na tukawaahidi kuwa tulikwenda kwenye maandalizi ya Operesheni Sangara ya Singida nzima!

Nimewaambia, tuna ushahidi wa video na tutautoa mahakamani.

John John MNYIKA,
Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA),
18 Julai, 2012
 
Kwa hiyo wamekuita uache shughuli za bunge ili wakakuhoji?

Hawa polis vp jamani?.
 
Sasa wakumwita ni mwingine wa kumhoji katoka Dar amabaye hata mazingira ya mkoa wa singida hayajui isipokuwa posho ambayo atapewa kwa kusafiri na kufanya kazi nje ya kituo. What does it mean??? The misuse of finances of poor wananchi.
 
Mahojiano tu ya kawaida, wala asiwe na shaka.

Hata mie nadhani hivo,,wanataka pia kung'amua habari zilizotapakaa kwamba polisi walifumbia macho vitendo hivyo ili labda wawajibishane,maana ni mwendelezo wa lawama,matope kwa polisi yenyewe siku hadi siku
 
1. Wameniita kutoa maelezo kama mtuhumiwa au shahidi?
Amenijibu kuwa ni mahojiano ya kawaida.

John John MNYIKA
Ok, kwa hiyo hilo swali lake lilikuwa halina maana basi, manake nilidhani amejipanga kusimamia haki zake mbele ya polisi, nikajua na mimi leo nitajifunza kitu siku polisi wakiniita. Kumbe duh, sio lazima uambiwe aidha wewe shahidi au mtuhumiwa....! Maana kaja na swali dhabiti kweli kweli, halafu katulizwa na kijibu nyanyaaaaa... akakubali!

Mheshimiwa Mnyika anatafutwa kwa udi na uvumba tangu amtaje mkuu wa nchi kuwa ni dhaifu na wabunge wa ccm ni wazembe na Mwigulu alihusika kwenye EPA wanaitafuta roho yake kwa kila njia anatakiwa awe mwangalifu sana kwa anachokula,anachokunywa, akiendesha gari akiongea achague maneno, yaani kifupi awe makini kwa kila sekunde ya maisha yake yupo hatarini sana sana kuliko wakati wowote ule!
 
Back
Top Bottom