Kangosha
Senior Member
- Sep 18, 2023
- 139
- 266
Kwa wale tunaofuatilia habari za kimataifa tumeona jinsi raia wa Nepal hasa vijana walivyoiangusha Serikali Yao kutokana na ugumu wa maisha. Hali kama hio naiona ikija kutokea Tanzania. Nasemea hivi kwa sababu zifuatazo:-
1. Vijana wengi wanamaliza vyuo,shule za secondary na hata msingi ila ajira hawana. Viongozi wengi hili jambo wanalichukulia poa kwa kuwa watoto wao na ndugu zao wa karibu wamewatafutia na kuwapa kazi kwa vimemo. Hakuna Kiongozi hata mmoja ambaye mtoto ama ndugu yake atakaa mwaka nyumbani bila kuunganishiwa kazi. Kwa wale maofisa wa utumishi watakubaliana na mimi kuhusu vimemo vinavyotokaga kwa wakubwa wakielekeza wawape ajira watoto na ndugu zao.
2. Swala la rushwa limeanza kuja kwa Kasi Sana. Kuna ofisi moja ya Serikali nilienda kwa ajili ya kupata huduma mtoa huduma akataka nimpe ela ili anisaidie. Akasema la sivyo niende nije siku nyingine. Rushwa huwa inakera, rushwa hujenga chuki. Bahati mbaya hata tuliowapa jukumu la kuzuia rushwa nao wanakula rushwa. Hakuna kitu kinakera kama mtu unapambana upate kitu flani halafu mtu anataka umpe rushwa ilihali ela ya kumpa rushwa hauna.
3. Viongozi wamekuwa wabinafsi na kujilimbikizia Mali. Sasa hivi viongozi waliopewa dhamana wanajilimbikizia mali hatari. Unakuta mtu ana majumba,lodge,magari, viwanja ambavyo haviendani na kipato chake. Nna mfano wa viongozi kadhaa nnaowajua. Viongozi hawajali shida za watu. Tena akitokea mtu akaisemea shida za watu anaonekana mbaya. Mfano mtu kama mchengerwa alikataa matumizi ya barabara ya mwendokasi ya Mbagala wakati tukisubiri mabasi yaje akatoa sababu za kuzuia za ajabu sana. Angeweza kusema yapite tu hata magari madogo ili kupunguza foleni.Alikataza kwa kuwa anajua yeye akiwa anaenda kwake Rufiji barabara inasafishwa na Polisi ama huyo huyo anapita kwenye mwendokasi. Wakati viongozi wa nchi za wenzetu wanatafuta kila namna kutatua kero za raia wao, hawa wakwetu ni kama vile hawajali kwa kuwa wanaona hakuna wa kuwawajibisha. Kadhalika watu hawaridhiki. Yaani familia nzima inakuwa inataka kujazana Serikalini. Bora hata ingekuwa ni kwa uwezo binafsi. Jitu linapewa nafasi kwa influence ya .......
4. Baadhi ya taasisi kutokuwajibika. Sasa hivi ukienda baadhi ya taasisi ni kama vile wamelazimishwa kufanya kazi. Kuna hospital moja nilienda wahudumu wapo busy kuchat na simu. Mtu unaenda hospital saa2 asubuhi na unatoka saa11 jioni. Haya yote yanalimbukiza chuki katika mioyo ya watu. Baadhi ya barabara zimeharibika balaa. Ndio tunajua kuwa budget ya kutengeneza haipo, ila kuna mashimo mengine ni makubwa hatari ambayo yangeweza hata kufukiwa na udongo wa moramu kwa kutumia vibarua.
3. Kutokuwa na mkakati madhubuti wa nchi katika kutengeneza ajira na kushukilia ajira zilizopo. Ishu ya kutengeneza ajira na kushukilia ajira zilizopo kupitia viwanda n.k ilitakiwa iwe Sera ya nchi na kila taasisi. Leo hii mtu anaweza kutengeneza ajira ama kujiajiri ila akakumbana na changamoto kutoka sehemu nyingine unayofanya aache. Mfano Leo hii ukisema ujiajiri kwa kuwa daladala ambalo utamuajiri dereva na kondokta utatamani uache mara moja maana Polisi wataku- harass balaa. Ila laiti wangejua kuwa daladala husika ni ajira kwa watu basi badala ya ku- harass kitengo cha traffic kingekuwa kinatoa somo kuhusu swala zima la daladala. Kitendo cha kuambiwa kuwa biashara kadhaa zimefungwa ilitakiwa Serikali iunde tume kujua sababu zilzosababisha kufungwa Kwa hizo biashara na kurekibisha ili kuzuia ufungwaji wa biashara zaidi.
Nnayo mengi ya kueleza ila niishie hapa.
Kwa wale tunaoitakia mema nchi yetu tutiririke zaidi. Maana nchi ikichafuka kila mtu atakuwa mhanga. Mbaya zaidi unakuta umejitafutia Mali zako kwa njia halali ila zinaharibiwa ukihisiwa kuwa na wewe ni Jizi.