hata mimi
JF-Expert Member
- Oct 17, 2017
- 1,356
- 1,437
Mjumbe BOQ inaandaliwa tu (kwa kupendekeza vifaa tu) halafu inakabidhiwa shuleni moja kwa moja habari ya bei manunuzi sijui takataka gani zote itajua kamati yenyewe (ambapo kamati yenyewe ni Mwl Mkuu kama mwenyekiti, Mwalimu wa ujenzi kama katibu na wajumbe wengine kutoka kwenye kamati ya shule)Huyu mleta mada ndio wale watu waliokubuhu kwenye majungu na huenda ni Mwalimu. Mnyororo wa Ujenzi unahusisha MAHANDISI ambae huandaa BOQ, PMU Kufanya manunuzi kadri mhandisi alivyoelekeza, Wakuu wa Shule na Wenyeviti wa Kamati za Ujenzi, Watendaji wa Kata na Vijiji vyenye mradi husika woooote wanakaa meza moja kupokea mgao wa manunuzi kama yalivyofanywa na PMU. Sasa hapo REO au DEO anaingia wapi? Tuache kutumia JF kuchafua wenzetu na Members wa JF wa aina hiii mngekuwa mnapigwa LIFE BAN ili muendekeze majungu kwenye familia zenu tu.
Mwalimu mkuu na Mwalimu wake wa ujenzi ndo watafanya quotation za bei madukani, kwa mafundi seremala na kila kitu mfano mawe mchanga kokoto nk kwa kusaidiana na wajumbe wao
Kichekesho zaidi viongozi wa serikali ya kijiji au kata wanaingia kama wadau tu kwenye kamati hizo lakini kuna 20% ya nguvu ya jamii ambayo Mwalimu Mkuu analazimika kumfuata boss wa kijiji ili aipate wakati huo huyo boss hajapewa mamlaka yoyote kwenye kamati za shule (kamati ya ujenzi ya manunuzi na ya mapokezi)
Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app