Mbunge Gulamali Atoa Mifuko 700 ya Simenti Ujenzi wa Shule na Zahanati

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

MBUNGE GULAMALI ATOA MIFUKO 700 YA SIMENTI UJENZI WA SHULE NA ZAHANATI JIMBO LA MANONGA

Mbunge wa Jimbo Manonga Wilaya ya Igunga, Mhe. Seif Khamis Gulamali ameendelea na ziara yake katika Vijiji vya Kata ya Uswaya na kutoa Mifuko 700 ya Simenti kwaajili ya kusaidia ujenzi wa Shule za Msingi na Sekondari na Zahanati.

Ziara ya Kikazi aliyofanya katika Kata ya Uswaya kwa Vijiji vya Chalamo, Utuja, Uswaya na Mwakadele ambapo ameweza kukagua Miradi, Kuzungumza na Wananchi na Kupokea Zawadi kutoka kwa wananchi

Mbunge Gulamali pia amegawa Vifaa vya Michezo kwa Vijiji vyote na Shule zote 3 za Msingi na Sekondari lakini Pia nimetoa mifuko 700 ya Simenti kwa Miradi mbalimbali kwenye Kata ya Uswaya inayohusu Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi, Ujenzi wa Zahanti na Ujenzi wa nyumba za Watumishi wa Afya

Akizungumza na wananchi waliohudhuria na kushuhudia michezo mbalimbali, Mhe. Gulamali amewashukuru sana wananchi na viongozi wa Vijiji kwa Mapokezi Mazuri na Upendo waliouonyesha kwake na kusema kwamba "Nasema Asanteni sana Wana Uswaya"
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-07-08 at 00.14.01(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-08 at 00.14.01(1).jpeg
    68.6 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-07-08 at 00.14.03.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-08 at 00.14.03.jpeg
    63.6 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-07-08 at 00.14.00.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-08 at 00.14.00.jpeg
    37.2 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-07-08 at 00.13.59.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-08 at 00.13.59.jpeg
    32 KB · Views: 2
Ni vyema ukatueleza pia pesa za mfuko wa jimbo zimetumika vipi?

Maana kusema mbunge katowa wakati ni pesa za mfuko wa jimbo kutoka serikali kuu ni Utapeli wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom