Steven mushi mushi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2016
- 533
- 741
Kuna rafiki yangu mmoja alipendana na binti mmoja sasa kutokana na mapenzi yao kuwa matamu na kuendelea kuimarika kila siku waliamua kula kiapo cha damu (yamini) ili wasijetengana wala kusalitiana. Baada ya kama mwaka mmoja tangu wale kiapo penzi likaanza kuyumba kwa kile jamaa anachodai binti kamwambia anataka waachane kila mmoja aendelee na maisha yake. Sasa rafiki yangu kachanganyikiwa juu ya kile kiapo cha yamini walichokula, yeye anasema ni lazima kwanza watengue kile kiapo maana wakiachana hvhv kinaweza kikawaletea madhara makubwa. Eti wana JF ni kweli kwamba mkila kiapo cha yamini ya damu kuwa hamtaachana ikitokea mmeachana bila kutengua kiapo kitakuwa na madhara kweli maana rafiki yangu anadai kinaweza kikasababisha hata kupoteza maisha. Ni kweli au ni uoga tu warafiki yangu maana kuna watu wengi ameongea nao ikiwemo ndugu zake ila wao wamemwambia hakina madhara.