Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
NIRA DHIDI YA WAANDISHI IVUNJWE - UHURU WETU ULINDWE
(Dhidi ya Mpango wa Serikali kulifungia/kuliadhibu Gazeti la MwanaHalisi)
Na. M. M. Mwanakijiji
Kwa mara nyingine tena serikali ya Kikwete inakabiliwa na changamoto moja kubwa nayo ni kama itaweza kuzikunja kucha zake ambazo tayari zimenoloewa, kutolewa na kunyoshwa kama simba aliyeona mawindo. Bahati mbaya tumeshawahi kuwepo hapa huko nyuma.
Lakini safari hii inaonekana hakuna mtu mwenye uwezo wa kutuliza wale wenye vichwa vya "moto" ambao wamedhamiria kutoa funzo moja, la wazi ambalo litakuwa ni onyo kwa vyombo vingine vinavyodiriki kuvuka "mpaka" na kuvunja sheria ya magazeti ya mwaka 1976.
Vyanzo vya uhakika kabisa vimedokeza kuwa Serikali imrkusudia kulifungia gazeti la MwanaHalisi kutokana na habari yake ya Jumatano iliyopita kuwa na mambo ya kichochezi, kichonganishi na ambayo haina maslahi ya umma bali iliyokusudia kuleta wasiwasi na kutishia hali ya "amani na usalama". Mpango huu kwa hisia zangu (kutokana na matakwa ya kisheria) hauwezi kukamilika hadi Gazeti la Serikali litoke na sina uhakika toleo jipya linatakiwa kutoka lini.
Sheria hiyo inaeleza wazi katika Ibara ya 31 kuwa kuna makosa yanayohusu uchochezi na kwa tafrisiri hiyo mtu atakuwa ana nia ya uchochezi endapo atafanya kati haya haya (kitu ambacho Mwanahalisi itatuhumiwa)
(Dhidi ya Mpango wa Serikali kulifungia/kuliadhibu Gazeti la MwanaHalisi)
Na. M. M. Mwanakijiji
Kwa mara nyingine tena serikali ya Kikwete inakabiliwa na changamoto moja kubwa nayo ni kama itaweza kuzikunja kucha zake ambazo tayari zimenoloewa, kutolewa na kunyoshwa kama simba aliyeona mawindo. Bahati mbaya tumeshawahi kuwepo hapa huko nyuma.
Lakini safari hii inaonekana hakuna mtu mwenye uwezo wa kutuliza wale wenye vichwa vya "moto" ambao wamedhamiria kutoa funzo moja, la wazi ambalo litakuwa ni onyo kwa vyombo vingine vinavyodiriki kuvuka "mpaka" na kuvunja sheria ya magazeti ya mwaka 1976.
Vyanzo vya uhakika kabisa vimedokeza kuwa Serikali imrkusudia kulifungia gazeti la MwanaHalisi kutokana na habari yake ya Jumatano iliyopita kuwa na mambo ya kichochezi, kichonganishi na ambayo haina maslahi ya umma bali iliyokusudia kuleta wasiwasi na kutishia hali ya "amani na usalama". Mpango huu kwa hisia zangu (kutokana na matakwa ya kisheria) hauwezi kukamilika hadi Gazeti la Serikali litoke na sina uhakika toleo jipya linatakiwa kutoka lini.
Sheria hiyo inaeleza wazi katika Ibara ya 31 kuwa kuna makosa yanayohusu uchochezi na kwa tafrisiri hiyo mtu atakuwa ana nia ya uchochezi endapo atafanya kati haya haya (kitu ambacho Mwanahalisi itatuhumiwa)
31.-(l)
(a) kuchochea. chuki au ufidhuli au uasi dhidi ya Jamhuri ya Muungano
au Serikali yake; au
(b) kuchochea wakazi wowote wa Jamhuri ya Muungano kujaribu
kuleta mapinduzi ya kijambazi ya jambo lo lote katika Jamhuri
ya Muungano, lililowekwa kwa mujibu wa Sheria;
(c) kuchochea chuki au ufidhuli au uasi dhidi ya utekelezaji wa
haki katika Jamhuri ya Muungano;
(d) kuchochea manung'uniko na chuki au uasi miongoni mwa wakazi
wa Jamhuri ya Muungano;
(e) kuchochea chuki na uhasama baina ya vikundi mbali mbali vya
wakazi wa Jamhuri ya Muungano.QUOTE]
Lakini ndani ya sheria hiyo hiyo ibara inayofuatia inasema kuwa mtu hatakuwa na hatia ya kuwa na nia ya uchochezi endapo atafanya mambo yafuatayo (Ibara 31):
(a) kuonyesha kwamba Serikali imepotoshwa au imekosea, katika shu-
Auli yake yo yote-, au
(b) kuonyesha makosa au hitilafu katika Serikah au Katiba ya Jamhuri
ya Muungano, kadri mambo hayo yalivyo kwa mujibu wa
Sheria, au katika Sheria za nchi au katika utekelezaji wa haki,
kwa madhumuni ya kusahihisha au kurekebisha makosa hayo au
hitilafu hizo; au
(c) kuwashawishi wakazi wo wote wa Jamhuri ya Muungano kujaribu,
kwa njia zilizo halali kwa mujibu wa Sheria, kuleta mabadiliko
ya jambo lo lote lililowekwa kwa mujibu wa Sheria;
(d) kuonyesha, kwa madhumuni ya kutaka yaondolewe, mambo yo
yote yanayochochea au yanayoweza kuchochea chuki na uhasama
baina ya vikundi mbali mbali vya wakazi wa Jamhuri ya
Muungano.
Sasa hapa unakabiliwa na tatizo. Kama mtu anafanya mambo ya ibara ya 31 ambayo yanatajwa kuwa ni halali lakini matokeo yake (kwa ni njema kabisa) yakasababisha hisia za chuki dhidi ya serikali au dharau kama ilivyo ibara ya 30 itakuwaje? Tutajuaje kuwa mtu anayefanya jambo hilo hana lengo baya hata kama analofanya ni halali? Sheria yetu mbovu ya magazeti inajichanganya kwa kujaribu kutoa jibu hapa (31:3)
(3) Katika kufikiria kama jambo lo lote lilitendwa, maneno yo yote
yalitamkwa au hati yo yote ilichapishwa na kutangazwa, kwa nia ya
kuchochea uasi, kila mtu atahesabika kuwa. ana jukumu kamili juu ya
matokeo yote ya vitendo vyake vyote vya makusud[/U]
hilo la kusema maneno hayo ni kupanua wigo wa uwezo wa serikali kufahamu nia ya mtu kiasi kwamba hakuna mazingira yoyote yale ambayo mtu anaweza kusema au kufanya kitu ambayo hayataangukia kwenye "vitendo vyake ya makusudi". Ni wangapi kati yetu wanafanya vitendo vya makusudi (visivyo vya bahati mbaya)?
Lakini kwenye suala la Mwanahalisi madai yatakayotolewa yataangukia katika vipengele hivyo lakini ni Ibara ya 36 ndiyo naamini itatumiwa kulifungia gazeti hilo au hata kuchukua hatua zaidi za kisheria. Ibara hiyo inasema hivi:
Mtu ye yote atakayetangaza au kueneza habarl yo yote
ya uwongo, Uzushi au taarifa ambayo yaweza kuwatia watu woga na
wasi wasi au kuchafua amani katika nchi atakuwa ametenda kosa na
akipatikana na hatia mbele ya mahakama atapaswa kuadhibiwa kwa
kutozwa faini isiyozidi shilingi elfu kumi na tano au kufungwa gerezani
kwa muda usiozidi miaka mitatu au kupewa adhabu zote mbili
(2) lwapo mtu ye yote atashtakiwa kwa kosa chini ya kifungu cha
(1) mahakama itabidi ikubali kuwa kuna utetezi wa kutosha ikiwa
mshtakiwa atathibitisha kwamba kabla ya kutangaza au kueneza habari
au taarifa ya aina iliyoelezwa katika kifungu cha (1) alichukua hatua
madhubuti za kuhakikisha ukweli wa mambo na kwamba matokeo
yake yalimfanya asadiki kwamba habari au taarifa hiyo ilikuwa ya kweli
Katika hilo la ibara ya 36 inaonekana suala hapa ni kwenda mahakamani. Lakini serikali haitaenda mahakamani kufungua mashtaka ya uchochezi. Wao watatumia kipengele cha sheria ambacho kinampa madaraka makubwa Waziri wa Habari.
Lakini kinachotisha zaidi siyo tu ukali wa sheria hiyo lakini zaidi uwezo wa Waziri mwenye dhamana ya Habari kufungua magazeti. Hebu tuangalie sheria hii inatoa nguvu za namna gani basi? Nitaweka ibara yote hapa:
25.-(l) Waziri akiona kwamba kwa ajili ya manufaa ya umma au
kwa ajili ya kudumisha amani na usalama inafaa afanye hivyo
aweza kutoa amri na kuitangaza kwenye Gazeti la Serikali ambayo itaeleza
kwamba gazeti lililotajwa katika amri hiyo litakoma kutolewa
tangu siku (ambayo katika fungu hili itaitwa ''tarehe ya kuanza kutumika'')
itakayotajwa katika amri hiyo.
(2) Kila amri iliyotolewa kwa mujibu wa kifungu cha (1) itataia-
(a) jina la gazeti linalohusika na amri hiyo;
(b) majina ya mwenye gazeti, mchapishaji na mtoaji wa gazeti hilo:
Isipokuwa kwamba hakuna amri kama hiyo iliyolewa kwa
mujibu wa kifungu cha (1) itakayokuwa batu kwa sababu ya
kukosa kutoa maelezo au kutoa maelezo yasiyo sahihi kuhusu mwenye
gazeti, mchapishaji au mtoaji wa gazeti au ye yote kati yao.
(3) Iwapo amri imetolewa kwa mujibu wa kifungu cha (1) kuhusu
gazeti lo lote-
(a) mtu ye yote ambaye, tangu tarehe ya kuanza kutumika. atachapisha
au kutoa au kuagiza lichapishwe au litolewe gazeti lo
lote lililotajwa katika amri hiyo, atakuwa ametenda kosa na
akipatikana na hatia mbele ya mahakama atapaswa - kuadhibiwa
kwa kutozwa faini isiyo,zidi shilingi elfu ishirini au kufungwa
gerezani kwa muda usiozidi miaka minne au kupewa
adhabu zote mbili pamoja;
(b) mtu ye yote ambaye, tangu tarehe ya kuanza kutumika, atauza,
atachuuza, atagawa, kuweka au kuagiza iwekwe hadhara ya
watu nakala yo yote au sebemu ya nakala ya gazeti lililotajwa
katika amri hiyo, iwe nakala hiyo au sehemu yake ilichapishwa
au kutolewa kabla ya tarehe ya kuanza kutumika au
sivyo, atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia mbele
ya mahakama atapaswa kuadhibiwa kwa kutozwa faini isiyozidi
shilingi elfu kumi au kutungwa gerezani kwa muda usiozidi
miaka miwili au kupewa adhabu zote mbili pamoja.
(4) Kwa madhumuni ya fungu hili ''hadhara ya watu'' ina maana
ya kawaida ya maneno hayo na pia ifahamike kuwa ni pamoja na
njia yo yote ambayo watu wana haki ya kupita, jengo, mahali au
chombo ambacho watu wana haki ya kukitumia ama bila masharti
au kwa malipo, na jengo lo lote au mahali po pote panapotumiwa
na watu kwa ajili ya ibada au mikutano au mahakama ambayo
watu wote wanakuwa huru kuhudhuria.
Katika ibara hiyo kuna mambo matatu ya kuangalia kwa ukaribu.
Kwanza, katika kufungia gazeti Waziri haitajiki kwenda mahakamani kupata amri ya mahakama kufanya hivyo. Yeye kutokana na wadhifa wake na kwa mujibu wa sheria hiyo ana uwezo wa kulifungia gazeti lolote alimradi kwamba "akiona kwamba kwa ajili ya manufaa ya umma au kwa ajili ya kudumisha amani na usalama inafaa afanye hivyo"
Hii ina maana kuwa katika suala la MwanaHalisi manufaa ya Umma ni nini? Tunapata kupata jibu kidogo katika majibu ya serikali (kupitia ndugu yetu Salva) kuwa Rais Kikwete anapendwa sana na anafanya mambo mazuri yanayosifiwa ndani na nje ya nchi yetu. Ina maana ya kuwa kama Mwanahalisi wameandika kitu ambacho kitamharibia sifa Rais na kumfanya asionekane bora au anayefaa au aliye makini basi "manufaa ya umma" yanadhurika! Yawezekana kitu kama hicho hicho ambacho ni wao wanajua manufaa ya umma ni nini hasa. Na katika hili wanaweza kuleta sheria za Usalama wa Taifa ya 1970, ya Taasisi ya Kijasusi ya 1996, Uhujumu uchumi na hata wakajaribu ile ya Madaraka ya Rais wakati wa Dharura ya 1986.
Kimsingi "manufaa ya umma" kinaweza kuwa kitu chochote cha kuwafurahisha watawala!
Jambo la pili la kuona katika ibara hiyo ya 25 ni kuwa ili wafikishane mahakamani ni mpaka pale ambapo Gazeti (Mwanahalisi katika mjadala wetu huu) iamue kukaidi agizo hilo la Waziri na kuchapisha gazeti hilo licha ya kufungiwa baada ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali (kitu ambacho nadhani wanakisubiri na sina uhakika linatoka lini). Endapo watatangaza (kumbuka kuwa Waziri hawezi kutangaza simamisho hilo hadi pale litangazwe kwanza kwenye gazeti la serikali vinginevyo litakuwa ni agizo batili) basi Mwanahalisi watakabiliwa na kukubali au kukaidi.
Kwa maneno mengine MwanaHalisi haliwezi kwenda mahakamani kupinga agizo la Waziri wa habari kwani Sheria haitoi nafasi hiyo (wanaweza kujaribu) kwani uwezo wa kulifungia gazeti uko mikononi mwa Waziri. Na zaidi ya yote Ibara ya 52 inasema hivi.
Hapana mtu ye yote anayeweza;kufungua mahakamani shauri lo
lote ]a madai dhidi ya mtumishi wa Serikali ye yote kwa ajili ya
jambo lo lote ambalo mtumishi huyo ametenda au ameacha kutenda
katika kutekeleza madaraka yake chini ya Sheria hii.
Wakikaidi serikali itavamia jengo la Mwanahalisi kuchukua vitu mbalimbali (kama ushahidi) na kuwapeleka mahakamani au kuwasumbua tu kama walivyofanya mapema mwaka huu.
Hili naamini ndilo linalopaswa kutokea kwani wakienda mahakamani ni serikali itatakiwa ithibitishe kuwa kilichoandikwa ni uchochezi, uchonganishi au kwa namna yoyote ile inavunja sheria ya 1976. Lakini uzuri wa kufikishana mahakamani ni kuwa kwa mara ya kwanza (katika kumbukumbu yangu) katika miaka ya karibuni sheria hii itawekwa kizimbani na uhalali wake Kikatiba utakuwa matatani hasa ukizingatia hili jambo la tatu nitakalolisema. Hivyo njia pekee ni kwa MwanaHalisi kukaidi agizo la kufungiwa litakalotangazwa kwenye Gazeti la Serikali.
Jambo la tatu ni kipengele cha mwisho kinachojadili "hadhara ya watu". Maana ya neno hilo kwa mujibu wa sheria hii ni mahali popote pale ikiwemo "jengo lo lote au mahali po pote panapotumiwa na watu kwa ajili ya ibada au mikutano au mahakama ambayo watu wote wanakuwa huru kuhudhuria" Hii ina maana gani?
Kwa kifupi baada ya Mwanahalisi kufungiwa ukikutwa na gazeti hilo (toleo la ukaidi) mahali popote iwe msikitini, kanisani, mahakamani au mahali popote pale ambapo panakidhi maana yao ya hadhara basi utakuwa na makosa na utatakiwa kulipa faini au kutumikia miaka 2 jela au vyote viwili.
Ninachosema ni kuwa endapo Serikali itakunjua kucha zake na kuwaparua mwanaHalisi, itakuwa ni wakati mbaya zaidi katika historia yetu ambapo vyombo vya habari kwa mara nyingine vinalazimika kufungiwa. Magazeti yamefungiwa huko nyuma mara nyingi tu na MwanaHalisi halitakuwa la kwanza.
Lakini magazeti hayo yote huko nyuma yamekuwa yakikubali amri hiyo bila kufanya civil disobedience. Ni matumaini yangu kuwa vyovyote wanavyotaka kufanya serikali wafanye, lakini MwanaHalisi litatoka hata kama itabidi litoke kwa njia nyingine kabisa lakini toleo hilo litatoka pamoja na hilo kufungiwa na kama kuna kwenda mahakamani basi wataenda mahakamani. Lakini hatuwezi kamwe kuacha sheria hii iendelee kuwepo na kuwa kama nira dhidi ya vyombo vya habari. Siyo sheria hii tu bali pia ya madaraka ya Rais wakati wa dharura ambayo sitoshangaa kama itatumiwa Tarime Jumapili , kama walivyoitumia Pemba 2001.
Tunatoa wito kwa serikali kuzikunja kucha zake, kukaa chini na kuzungumza vinginevyo badala ya kumuacha Waziri alifungie gazeti basi waende kwanza mahakamani kutoa shitaka dhidi ya MwanaHalisi kwa kutumia sheria hiyo au yoyote waliyonayo.
Hatuwezi kukaa kama watumwa ambao dakika yeyote nira ya mabwana zetu itashushwa kwenye shingo zetu. Endapo gazeti hilo litafungiwa kwa sababu Waziri kasema hivyo, ninaahidi kukaidi amri hiyo kwa njia ninazojua mimi.