Ongezeko la wimbi ya kesi za Uhaini na Ugaidi nchini

Izato

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2019
Posts
5,378
Reaction score
11,545
Kutokana na ongezeko kubwa la wimbi la ufunguaji wa kesi nyingi sana za Uhaini na Ugaidi hivi sasa nchini katika utawala huu uliopo, kuna kila sababu ya kuwa na mashaka makubwa juu ya intelijensia ya Jeshi la Polisi.

Huenda polisi wana weledi unaotia shaka kwa kuzichukulia kwa wepesi mno tafsiri halisi ya kesi hizi. Ama kuna mashinikizo ya kisiasa kupitia ufunguaji kiholela wa kesi hizi ili kuweza kuwakomoa ama kuwathibiti mahasimu wa kisiasa ambao wanatishia maslahi ya watawala waliopo madarakani hivi sasa.

Ni vyema na haki Jeshi la Polisi kupitia maafisa wake waenende na kutenda kazi zao kimaadili, na zenye kuaminika mbele ya jamii, na wanapaswa kuwa waadilifu katika kuzifungua kesi hizi nzito. Ni vyema wakatambua kuwa kwenda kinyume na matakwa ya katiba na sheria, kila muhusika atakuja kuwajibika kipekee, na huu uchochoro wa kukwepa kuwajibika ipasavyo kwa kisingizio cha maagizo kutoka juu hautakuja kuwasaidia chochote katika siku za mbele, iwe hapa duniani ama mbinguni katika siku ya hukumu ya kiama.

Ni vyema jeshi letu hili likatambua kuwa matendo ya Ugaidi na Uhaini kwa mujibu wa sheria za Tanzania ni makosa mawili makubwa sana kwa kuwa yanahusu usalama wa Taifa na hivyo kustahili kwa kipekee kabisa kubeba adhabu kali kwa muhusika ama wahusika wa makosa haya. Ni lazimu wapate ufahamu wa kina kama vile ifuatavyo,

1. UHAINI - TREASON hili ni kosa la moja kwa moja dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na linatajwa katika Katiba ya Tanzania 1977 Ibara ya 28 na Kanuni ya Adhabu Sura ya 16, vifungu 39-41.

Vitendo vinavyohesabiwa ni uhaini ni;
1. Kufanya vita dhidi ya Jamhuri.
2. Kushikamana na adui wa Jamhuri au kumpa msaada katika kutekeleza nia ovu
3. Kuchochea uvamizi wa kigeni wenye silaha
4. Kushika silaha kwa nguvu kuilazimisha Serikali kubadili maamuzi yake, au kuitisha/kutisha Serikali
5. Kufanya kitendo kinachokusudia kumpa msaada adui, kuharibu utulivu wa umma, kuzuia majeshi au polisi, au kuhatarisha maisha
6. Kumuua au kujaribu kumuua Rais

Adhabu ya Uhaini ni
moja tu, yaani Kifo

Makosa yanayofanana, yaani Treasonable offences. Kifungu 40: mtu asiye chini ya uaminifu akifanya kitendo kama cha uhaini kama vile,
kuficha uhaini - Misprision of treason yanatajwa katika kifungu 41. Kujua mtu anapanga kufanya uhaini na kutotoa taarifa kwa mamlaka husika. Adhabu yake ni kifungo cha maisha.

2. UGAIDI - TERRORISM
Unasimamiwa na Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002 - Prevention of Terrorism Act.
Sheria hii inatoa adhabu kwa:
1. Kufanya kitendo cha kigaidi. Kifungu 5, 7, 8: Adhabu ni kifungo kisichopungua miaka 30
2. Kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi: Adhabu ni kifungo kisichopungua miaka 18.
3. Kuficha ama kuhifadhi magaidi. Adhabu ni kati ya miaka 18 hadi 30
4. Kukusanya au kutoa fedha kwa kundi la kigaidi: Adhabu ni Kati ya miaka 15 hadi 20

Polisi wetu wanapaswa kutambua kuwa uhaini ni kushambulia moja kwa moja Serikali, Taifa, au Rais. Na Ugaidi ni kujenga hofu na vurugu dhidi ya raia kwa lengo ovu la kisiasa/kiitikadi.

Uchochezi mitandaoni kwa sasa unatumika kama kisingizio pekee cha ufunguaji wa kesi hizi. Kimbilio la eti watuhumiwa kutuma ujumbe unaochochea, kudhalilisha, au kuleta hofu inayoweza kusababisha mashtaka ya uhaini. Na hii ndiyo imebakia kuwa "mens rea" inatotumika sana na maafisa wa polisi hivi sasa.
 
Kutokana na ongezeko kubwa la wimbi la ufunguaji wa kesi nyingi sana za Uhani na Ugaidi hivi sasa nchini katika utawala huu uliopo, kuna kila sababu ya kuwa na mashaka makubwa juu ya intelijensia ya Jeshi la Polisi.

Huenda polisi wana weledi unaotia shaka kwa kuzichukulia kwa wepesi mno tafsiri halisi ya kesi hizi. Ama kuna mashinikizo ya kisiasa kupitia ufunguaji holela wa kesi hizi ili kuweza kuwakomoa ama kuwathibiti mahasimu wa kisiasa ambao wanatishia maslahi ya watawala waliopo madarakani hivi sasa.

Ni vyema na haki Jeshi la Polisi kupitia maafisa wake waenende na kutenda kazi zao kimaadili yenye kuaminika na jamii, na kuwa waadilifu katika kuzifungua kesi hizi nzito. Ni vyema kutambua kwenda kinyume na matakwa ya katiba na sheria, kila muhusika atakuja kuwajibika kipekee, uchochoro wa kukwepa kuwajibika ipasavyo kwa kisingizio cha maagizo kutoka juu haitakuja kuwasaidia chochote katika siku za mbele, iwe hapa duniani ama mbinguni katika siku ya hukumu ya kiama.

Ni vyema Jeshi letu likatambua kuwa Ugaidi na Uhaini kwa mujibu wa sheria za Tanzania ni makosa mawili makubwa sana ya kisheria kwa kuwa yanahusu usalama wa Taifa na hivyo kustahili kwa kipekee kabisa kubeba adhabu kali kwa muhusika ama wahusika wa makosa haya.

Tanzania ni nchi ya kigaidi, full stop.
 
Yani DPP kwa miaka yake minne kazink amefungua kesi za ugaidi nyingi kuliko kesi zote za ugaidi zilizowahi kufunguliwa dunia nzima
 
Watawala, wapambe wao, pamoja na machawa wao, hawatambui kuwa Jeshi la Polisi kila linavyo fungua kesi hizi, mbele ya jumuiya ya kimataifa inaleta athari hasi za kiuchumi na kidiplomasia.

Wao wanadhani wanawakomoa viongozi wa CDM na wanaharakati, hawatambui wanaoathirika ni umma wa Watanganyika. Kinasosubiriwa sasa ni "time bomb" kulipuka kutokana na chuki ya wananchi waliokuwa wengi dhidi ya watawala waovu, wezi, na wasioaminika.

Maafisa wa Jeshi la Polisi ambao wanafahamika mbele ya jamii kwa kushiriki uovu na ukandamizaji huu wa watawala lazima watambue hawako salama. Wajifunze kwa kile kilochomtokea Bwana Jela wa Gereza la Ukonga mbele ya macho na matakwa ya sheria.
 
Wasimamizi wa Mijadala, tafadhali naomba kichwa cha habari katika uzi huu kisomeke kama ifuatavyo,

Ongezeko la wimbi la ufunguaji wa kesi za Uhaini na Ugaidi nchini

Natanguliza shukrani zangu kwenu.
 
Back
Top Bottom