Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Nakumbuka katika kuteua wakuu wa mikoa muda fulani uliopita, Raisi Magufuli alisema kwamba alikuwa akiteua wakuu wa mikoa ya mipakani wengi wakiwa wanajeshi ili kusaidia katika suala la ulinzi mipakani. Lakini sasa, migongano na nchi jirani za Kenya, Zambia, Rwanda na hata Uganda zimetufundisha na kutupa onyo juu ya umuhimu wa kuhakikisha kwamba wakuu wa mikoa ya mipakani wanapaswa kuwa watu wenye uwezo mkubwa wa kidiplomasia.
Ukichukulia Tanga na Kilimanjaro kwa mfano, tumeshuhudia wakuu wa mikoa wakichochea badala ya kuzima moto wa jazba uliojitokeza kati yetu na Kenya, hadi kufikia hatua ya kuwakejeli viongozi wakuu wa nchi jirani! Sasa hii ni hatari sana, na tusipoangalia inaweza kuleta machafuko kufikia wananchi wa mipakani kuanza kupigana na watu wa nchi jirani na hata kuuana. Na mazingira kama hayo yanaweza kufikia hatua ya polisi au jeshi kuingilia kati, na hata risasi kupigwa dhidi ya nchi jirani na kuzua mpambano wa askari wenye silaha.
Sio vibaya kuweka wanajeshi kama wakuu wa mikoa ya mpakani, kwa kuwa wapo wanajeshi wanaojulikana kuwa mahili katika masuala ya diplomasia. Hata hivyo, kama ni suala la ulinzi mipakani ni vema kuwa na kambi za jeshi katika kila mkoa wa mpakani, na wakuu wa kambi hizi wakawa sehemu ya kamati za ulinzi za mkoa ambazo zinasimamiwa na wakuu wa mikoa.
Hata hivyo, kipaombele kiwe kuteua wakuu wa mikoa ya mipakani ambao ni raia na watu wenye uwezo mkubwa katika masuala ya diplomasia. Na ikibidi, wakuu wa mikoa ya mipakani wawe wanapitia mafunzo maalumu ya diplomasia kabla ya kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi.
Ningependa kushauri kwamba mabadiliko haya yafanyiwe kazi haraka iwezekanavyo.