Yaliyonikuta January 1 2012

Yaliyonikuta January 1 2012

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,292
Reaction score
6,773
Nilikuwa maeneo ya upanga karibu na kituo cha polisi cha zamani ambacho kimehamishwa Ghafla ikasimama gari mbele yangu. Mtu mmoja mwenye mvi na kitambi kikubwa akateremka na kuanza kunifokea. Akaniambia "Fundi umefuata nini huku mi nakuitia kazi we unazurura tu!" Akanipatia bahasha huku akifoka akaniambia haraka sana kaanze kazi. Akaingia kwenye gari na kuondoka nilipofungua ile bahasha nimekuta kibunda cha noti za shilingi 10,000 1.milion. na kile cha shilingi 5000 laki tano. Kwa jinsi alivyoondoka haraka nimeshindwa kukanusha kuwa sio mimi.
 
dah afadhali umejitangaza humu
sasa tunakuja kudai chetu ....kumbe ni wewe????lol
 
Hela za magumashi hizo..polisi wako nyuma yako!
 
Iwapo nitamfahamu mwenyewe nitamrejeshea kile kilichosalia
 
Hela za David Cameroon hizo, jiandae kuwaga wiyo tumbwinya yako.
Amesema fundi na ndani ya Bahasha kuna kikaratasi kidogo kimeandikwa mwambie mke wangu akuopatie funguo za stoo utoe mifuko 15 ya cement na nondo zitakazotosheleza tutawasiliana nikirudi Kibaha.
 
Pesa za majini hizo!
Alitabiri sheh yahya kabla ya kifo chake kuwa hiyo itatokea mwaka huu.
 
duh, ningekuwa mie nimepata bahati hiyo.
Ningeongeza mke wa pili
 
Sipati picha ulivyofungua hiyo bahasha na kukuta ni pesa,ulikuwa matumatu niaje!
 
yakweli hayo? maisha yenyewe yalivyo magumu!!
 
Duh..hii kitu imekaa ki Freemason 100%

Huyo shrti lake litakuwa yeye awe anatoa fungu kama hilo akikutana na mtu yeyote barabarani. Wapo wengine wamepewa masharti kuwa inapogonga saa 6.01 tu, wanachomoa hela mfukoni na kuanza kuhesabu kwa tumaini la kushika hela nyingi mwaka huo. Wengine wanazimwaga chini njia panda....
 
namuhurumia fundi,atapata msala wa kuambiwa keshalipwa kazi hajafanya
 
Back
Top Bottom