Ni USD 2500 tu, story ya rafiki aliyeona kabahatisha, kumbe kabahatishwa

Ismoo

JF-Expert Member
Apr 18, 2018
1,039
1,460
Hii Nimeitoa kwa Mdau Mmoja Huko Kariakoo, Mitaa ya Msimbazi, Jijini Dar Es Salaam, Alikutana na Mtu Huyu, Nae Akaona Hii ni Fursa Adhwim ya Kujiongezea Kipato.

Mazungumzo Yalikuwa Kama Hivi:

"Kaka samahani ndugu yangu"
Haya maneno yalimfanya apunguze mwendo na ageuke ili aone ni nani aliyemsemesha, mwenye rafudhi ya watu wa Mwanza.

Alikuwa ni jamaa mmoja hivi wa makamo umri kuanzia miaka 40 - 45. Alikuwa amevaa rafu sana watoto wa mjini husema kavaa Kinyasa, "Za sahizi Kaka"

"Salama"
Akajibu kisha akamuuliza "Unasemaje?"

"Kwanza unaitwa nani?" Akamtajia jina lake

Akamwambia...
"Ooh kumbe ni Mkristo mwenzangu basi nakuamini, mimi naitwa......" Akataja jina lake, alafu akaendelea kuongea....

"Ndugu yangu naomba unisaidie"
Alisema huku akitoa kijibahasha kilichotuna mikononi mwake na kukifungua.

"Ndugu yangu mimi nilikua nafanya kazi kwa wazungu mwaka mzima, sasa ndiyo wamenilipa haya mahela ya kikwao"
Alikuwa anaongea hivi huku tayari ameshatoa kibunda cha hela kutoka kwenye kile kijibahasha.

Kwa haraka haraka aliweza kutambua zile zilikua ni dola za kimarekani, japo akuweza kujua zilikua ni dola ngapi?!

Jamaa aliendelea kumwambia...
"Mimi sijui pa kuyatumia, mimi nataka hela nilizozizoeya ili nirudi kwetu Maswa, Wewe unayajua?"
Jamaa akamjibu "Ndiyo, na ili uweze kupata pesa za kitanzania itabidi zibadilishwe"

"Zikibadilishwa napata shingapi? Boss wangu nilimuuliza hizi ni shingapi akaniandikia kwenye bahasha"
Aliongea huku akimpa kijibahasha asome, yalikua ni maandishi ya wino wa blue yalisomeka "Dollars 2500"

"Ngoja nipige hesabu"
Jamaa akwambia huku anaingiza mkono mfukoni na kuchukua simu yake, haraka haraka kwenye Kikokotozi (Calculator).

Kiukweli jamaa alianza kupagawa baada ya kuona madolali, akutaka kujua alikua anafanya kazi wapi, kazi gani na kwa nani?
Alichokumbuka mara ya mwisho kufatilia dola 1 ilikua sawa na shilingi 2300. Chapchap akafanya hesabu rahisi tu 2300 ×2500 jibu likaja 5,750,000/-

Akazidi kupagawa akaona huyu boya hela zote hizi asimpige!? Alikua anawaza kumuibia kiujanja ujanja tu, basi akamwambia hizo pesa ni sawa na milioni tano tu.

"Milioni tano!?"
Jamaa akapayuka kwa mshangao kisha akasema
"Ukinisaidia tukazipata nitakupa milioni moja si itakutosha?"

Akamjibu "Ndiyo"

Sasa hapo kichwani akawa anapiga hesabu za kwamba atapata faida ya 1,750,000 bila kuitolea jasho

Basi bwana akamwambia twende nikupeleke pakubadilishia pesa.

Ghafla wakasikia sauti ya mtu mwingine, ikiwashtua: "Oya vipi jamani, kuna nini hapa...!?"
Jamaa mwingine akaja mbele yao na kuwauliza "...mimi nilikua nawaangalia kitambo"

Yule jamaa aliyewasimamisha akaongea kwa mkazo akitaka kujua kinachoendelea.

Sasa jamaa yangu akaona dili lake kama litakwama hivi, hivyo hakumjibu kitu akamwambia yule Msukuma twende zetu.
Lakini cha ajabu yule Msukuma hakutaka kwenda na kuanza kumuelezea yule jamaa kila kitu kuanzia mwanzo hadi mwisho mpaka walivyokubaliana. Jamaa yangu ndani ya moyo Anakereka kwelikweli...

"Sasa sikilizeni...." Yule jamaa akasema
"...Mimi nina boss wangu tunaweza kumfata na kumpa dola yeye atupe pesa za kitanzania ana ofisi yake si mbali na hapa twendeni atatupa pesa, Benki watawasumbua"

Baada ya jamaa kusema vile yule "Msukuma" akamhaidi jamaa kuwa wakifanikiwa atatoa milioni moja wagawane na jamaa yangu. Basi wakaanza safari kwenda kwa huyo Boss wake, wakafika kwenye ofisi moja kwa nje kulikuwa na magari kadhaa yameegeshwa Kwenye yale magari kulikua na gari moja Toyota Mark X nyeusi, jamaa akawapeleka mpaka kwenye hiyo Mark X.

Kulikua na wanaume wawili, mmoja alikua mnene mweusi ana kitambi kavalia suti kijivu na tai, jamaa akawasalimia na kumuita pembeni yule Bonge mwenye suti na kuanza kuongea naye... Kumbuka jamaa yangu alishamtonya yule jamaa na suala la kula ganji, akasema atulie atamseti Boss wake...



SEHEMU YA PILI NA YA MWISHO. SHUKA CHINI YA COMENT UTAIKUTA:
 
Kwa kuwa "main caractor" naye alikuwa na nia ovu, ninapenda akalizwe.

Katika movie za wanyama, roho yangu huridhika sana nikiona kwa mfano simba akizingirwa na mbwa mwitu na kisha kuliwa mpaka anaisha.

Nikiona fisi kakamatwa na simba na kufanywa mlo huwa ninajisikia faraja.

Nikiona nyoka anayekula panya akikamatwa na kenge na kumezwa mazima, hapo roho yangu burdaaaan!

Tukija kwa upande wa binadamu mi ninapenda sana mwizi akiibiwa, dhulmati akidhulumiwa, tapeli akitapeliwa na muuaji akiuawa!

Ninapenda sana kuona mbaya akitendewa mabaya yale yale anayowafanyia wenziye ili ayahisi maumivu wanayoyapata kwa ufedhuli wake.
Embu songesha simulizi hii tuuone mwisho wake.
 
Walipagawishaga kipindi fulani nikaja kushtuka mwishoni kabisa na pesa mkononi tayari wanile kichwa! Hawakuamini kilichotokea! Wanatumiaga dawa hawa mbwa!

- kuna wengine wana trick ya kutengeneza pesa wajinga sana
Mkuu mbona una kisa mujarabu sana, embu tusimulie ilikuwaje kuingizwa kingi na kisha ukasevu?
 
Mkuu movie zile zina uharisia wa Maisha yetu japo huku ni hakili sio action
Kwa kuwa "main caractor" naye alikuwa na nia ovu, ninapenda akalizwe.

Katika movie za wanyama, roho yangu huridhika sana nikiona kwa mfano simba akizingirwa na mbwa mwitu na kisha kuliwa mpaka anaisha.

Nikiona fisi kakamatwa na simba na kufanywa mlo huwa ninajisikia faraja.

Nikiona nyoka anayekula panya akikamatwa na kenge na kumezwa mazima, hapo roho yangu burdaaaan!

Tukija kwa upande wa binadamu mi ninapenda sana mwizi akiibiwa, dhulmati akidhulumiwa, tapeli akitapeliwa na muuaji akiuawa!

Ninapenda sana kuona mbaya akitendewa mabaya yale yale anayowafanyia wenziye ili ayahisi maumivu wanayoyapata kwa ufedhuli wake.
Embu songesha simulizi hii tuuone mwisho wake.
 
Back
Top Bottom