demigod
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 8,250
- 15,116
Natumai kila mtu alishawahi kuingizwa mjini kwa namna ambayo hatokuja kuisahau.
Pia nina amini hata uwe mjanja vipi wapo watu watakao kuzidi ujanja katika eneo ambalo huna ufahamu nalo vya kutosha.
Kisa Changu:
Kipindi kile simu zinatoka toka. Bi mdashi alininunulia simu flani hivi, sifa kubwa ya ile simu ilikuwa na mp3 (mpTHREE) ndani yake.
Kipindi iko vocha ya buku tu.Nayo ilikuwa inaitwa Dola moja. Hakukua kujiunga wala nini.
Unaweza kuplay muziki na wale wenye Nokia za tochi wakabaki wanakishangaa.
Siku moja nilikuwa nafanya safari kwenda kariakoo kununua mzigo wa familia. Tukashuka na basi katika mtaa ambayo una msongamano mkubwa sana watu. Sijatembea hatua 10 mbele, Jamaa akanishika bega uku akisema kwa sauti ya chini "Najua hunifahamu lakini tutembee kwa haraka kidogo ili nikushirikishe jambo". Nami nikatii.
Kufika mbele kidogo akaniambia noitazame nyuma ili nione kama kuna mtu yeyote anayetufuata kwa shauku. Ni kweli bhana kutazama nikaona kama kuna jamaa ambaye alikuwa alitufuata kana kwamba hana uhakika na watu anao wafuatilia.
Kumjibu ndio, akasema huyo jamaa ameibiwa pesa kwenye gari lakini hana uhakika na mtu aliye muibia. hivyo basi anatufuatilia sisi kwa nyuma ili kutaka kufahamu kama kuna muhusika kati yetu.
Nikamuuliza kwa hiyo shida yako nini, Akasema "Ni kweli nimezichukua ila hana uhakika kama ndimi ndiye niliyezichukua". Hivyo basi jamaa akatoa bahasha (Ile ya barua) ikiwa imejaa mithili ya vibunda vya pesa ndani yake. Jamaa akachana ile bahasha kwa juu nami nikaona noti moja ya buku 10 hivyo kupelekea kuamini kuwa zilizomo mule ndani zote ni noti.
Tukiwa tunaendelea kutembea huku yule wa nyuma akiendelea kutufuata kwa shauku, jamaa akashauri anipe ile bahasha yenye pesa ili tuachane kwa mbele llengo kuu ni kumpoteza maboya yule anayetufuatilia. Ila aliponikabidhi ile bahasha alisema kuwa ninaweza kukimbia na pesa la sivyo nimuachie kitu chochote cha thamani.
NDANI YA AKILI YANGU:- Yakiwa yote yanaendelea nami pia ubongo wangu ukanishauri nimpige tukio huyo jamaa. Akili ilisema jamaa akikupa kibunda na mkaachana njia basi wewe tokomea mbali na hilo eneo linaloitwa kariakoo.
Kitu cha thamani pekee ambacho nilikuwa nacho ni ile simu. Sikusita kumpatia simu kwa sababu niliona uwingi wa zile pesa ndano ya bahasha nimgeweza kununua hata simu kama zile 10. Basi nikampa huku akinisisitiza kuwa tuachane pale mbele na tukakutane roung about karibu na maduka ya kuuza simu.
Nimeisahau kidogo mitaa ya Kariakoo, kwakuwa niko nje ya mkoa kwa kipindi sasa. Lengo la kuachana ni kumpoteza maboya jamaa aliyekuwa akitufuatilia, na kweli baada ya kuachana njia jamaa wa nyuma alianza kumfuatilia jamaa niliyempa simu yangu, nami nikadhani mpango wetu umefanikiwa.
Kufika mbele kidogo nikachepuka njia tofauti na ile niliyoelewana na jamaa lengo lilikuwa kutoroka na pesa. Nikafika pahala ambapo nikaona choo cha kulipia nami nikalipa na kuingia. Humo nilikusudia kuanza kuhesabu pesa ili kufahamu ni kiasi gani.
NILIPIGWA NA BUMBUWAZI:-
Baada ya kufika nikatoa bahasha ile na kuichana, Loooooh Bahasha ilikuwa na noti moja ka Elfu KUMI na zingine zote hazikuwa noti bali ni magazeti yaliyochanwa kufuata size ya noti za buku kumi kumi. Hapo ndipo nikagundua kuwa NIMEKWISHA TAPELIWA.
Baada ya hapo nilianza kuchanganyikiwa na kuanza kukimbialia uelekeo ambao wale jamaa walielekea. Kuchanganyikiwa kwangu kulinipelekea hata kuanza kuuliza watu kuwa "WALE JAMAA WAWILI WAMEELEKEA WAPI?"
Nilihaha kama Mbwa aliye kosa maziwa ya mama yake. kariakoo nzima nilizunguka huku nikiwa na amatumaini kuwa huenda nikakutana nao kwa bahati mbaya.
Ikumbukwe kuwa Niliingia Kariakoo majira ya saa 3:45 asubuhi. lakini nilirudi home saa 12 jioni. Jambo zuri nilirudi na mzigo ambao niliagizwa ila nikakuta malalamiko kuwa kwanini nimechelewa kurudi na ilikuwaje sikuwa napatikana kwenye simu.
Nilimdanganya Bi mdashi kuwa tuliibiwa kila kitu simu pamoja na pesa za kufanya manunuzi ila kwa msaada wa Polisi tuliweza kupata pesa kutoka kwa mmoja kati ya wezi wawili walio dhaniwa, Ila yule mwizi mmoja alifanikiwa kuondoka na simu.
Mpaka leo hii sijawahi kumwambia ukweli Bi mdashi ila natumai kumwambia ukweli siku nikirudi kuonana naye. Jambo ambalo nina uhakika nalo ni kwamba hatokuwa na kumbukumbu ya kukumbuka kama aliwahi hata kuninunulia simu ambayo nimeielezea.
TUPE KISA CHAKO.