Yaliyojiri kesi inayomkabili Mbowe na wenzake leo Februari 4, 2022. Kesi imeahirishwa. Shahidi wa 13 kuendelea kutoa ushahidi Februari 7, 2022

Shahidi: Ni Simu aina ya Techno Yenye Rangi Nyeusi, ambayo Nimeitambua Kupitia Exhibit Lebel Ambayo Inaonyesha Namba ya Jalada la CD/IR /2097 /2020 Pia imeandikwa aina ya simu, Na inaonyesha Simu hiyo imepatikana kwa Mtuhumiwa ambaye ni Mohammed Abdilah Ling'wenya

Wakili wa Serikali: VIpi Kuhusu IMEI namba Shahidi: IMEI namba imeandikwa IMEFUTIKA

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Naona ametambua P 35

Wakili wa Serikali: Twende Kwenye Simu za Tarehe 09 August 2020

Shahidi: Simu nilizo pokea Tarehe 09 August 2020 ni Mbili ambazo ni Za Khalfani Bwire Simu aina ya Bundy, Nimeitambua Kupitia Lebel namba ambayo Inaonyesha Namba ya Jalada ambayo ni CD/IR /2097 /2020

Na Simu hii inaonyesha ni aina ya Bundy IMEI namba 359440075933775 Na Simu hii ilipatikama Maungoni Mwa Khalfani Bwire

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ametambua Exhibit P 30

Wakili wa Serikali: Simu Nyingine kwa hiyo Tarehe 09

Shahidi: Simu Nyingine ni simu aina ya Tecno Yenye IMEI namba 355019115930845 Simu hii nayo ilipatikana Maungoni Mwa Khalfani Bwire Inaonyesha Namba ya Kesi ambayo ni CD/IR /2097 /2020

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ametambua Exhibit P 32

Wakili wa Serikali: Twende Simu uliyokabidhiwa Tarehe 11 August 2020

Shahidi: Naitambua Simu aina ya Techno Yenye IMEI namba 358721101132040

Wakili wa Serikali: Imetoka Kwa nani

Shahidi: Imetoka Kwa Denis Leo Urio ambaye ni Mmiliki ambayo Inaonyesha Namba ya Kesi CD /IR /2097 /2020

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ametambua Exhibit P 34

Wakili wa Serikali: Nani ambaye ameandaa PF 145 kwenye simu hii

Shahidi: Simu hii nimeandaa Mimi na Nimeandika kwa Mkono Wangu

Wakili wa Serikali: Twende simu za Tarehe 12 August 2020

Shahidi: Simu hiyo ni Techno Yenye IMEI Namba 358073079115221

Wakili wa Serikali: Ulipokea Simu hiyo Kutoka Kwa nani

Shahidi: Kutoka Kwa Luteni Deni Leo Urio, Inaonyesha Namba ya Jalada CD /IR/ 2097/2020
Hivi kwa mfano simu ikiwa ya laini mbili inakuwa na IMEI moja au mbili?
 
Shahidi: Leo anaongea taratibu Kuliko Mashahidi wote ambao waliwahi Kufika Katika kesi hii, Kila Muda Jaji na Mawakili wa Serikali Wanamkemea na Kuomba aongeze Sauti
 
Juzi

Kibatala; hiyo simu ina line?

Urio; Hakuna

Kibatala; ulimpa swila simu na line hau bila line?

Urio; nilimpa na line.

Kibatala; hiyo line ipo wapi?

Urio; sijui

Leo

Ws: baada ya kukutana na urio nini kiliendelea baada ya kutoa maelezo?

Swila: nilimuomba simu kwa ajili ya upelelezi.

Ws: baada ya kukukabidhi simu nini kiliendelea?

Swila: aliniomba nimpe line ya Vodacom kwa sababu nilijua Kama anawasiliana na mbowe kwa telegram taarifa zitabaki kwenye simu.

Hawa watu hawakujipanga kufremu hii kesi ya michongo.

Sent from my Lenovo TB-7305X using JamiiForums mobile app
 
Kesi ya michongo shaidi bila kumpiga tution ya nguvu (maswali na majibu) sijui huko mahakani kungekuwaje. Swila anaonekana ana kichwa kigumu sana yahani mpelelezi mzima anachukuwa msasa wa siku mbili. Huku unatililika vizuri kwa sababu amelala na mtihani. Ngoja sasa akutane na mtiani usiokuwa na chabo tumuone atakavyo weweseka
 
Juzi

Kibatala; hiyo simu ina line?

Urio; Hakuna

Kibatala; ulimpa swila simu na line hau bila line?

Urio; nilimpa na line.

Kibatala; hiyo line ipo wapi?

Urio; sijui

Leo

Ws: baada ya kukutana na urio nini kiliendelea baada ya kutoa maelezo?

Swila: nilimuomba simu kwa ajili ya upelelezi.

Ws: baada ya kukukabidhi simu nini kiliendelea?

Swila: aliniomba nimpe line ya Vodacom kwa sababu nilijua Kama anawasiliana na mbowe kwa telegram taarifa zitabaki kwenye simu.

Hawa watu hawakujipanga kufremu hii kesi ya michongo.

Sent from my Lenovo TB-7305X using JamiiForums mobile app
NDO KWA NINI RE-EXAMINATION YA LT URIO ILISITISHWA GHAFLA.
 
Back
Top Bottom