Yaliyojiri Jangwani, Dar: Mkutano wa kuhitimisha Kampeni za mgombea Urais wa CCM, Dr. Magufuli

Democracy
 

Attachments

  • 1445613062845.jpg
    1445613062845.jpg
    41.4 KB · Views: 333
Magufuli:
Ninafahamu Dar es Salaam mna tatizo la Maji. Kuna mradi wa maji haujamalizika kwa sababu kuna baadhi ya watu wamepeleka zuio mahakamani. Kesi mpaka sasa inasua sua mahakamani wakati tunapoteza watu kwa sababu ya magonjwa kama kipindupindu. Swali la kujiuliza, Kwa nini kesi haimaliziki Mahakamani ili mradi wa maji umalizike kuepusha maafa ambayo tunaweza kuyazuia. Nikiwa Rais siwezi kuingia kazi za Mahakama lakini nitajenga mazingira ya kuwezesha kesi kuisha haraka na kwa ufanisi.
 
Katika hali niliyoitafusiri kama kuchanganyikiwa leo magufuli katoa tena mpya jangwani baada ya kumwambia Rais Kikwete.Nasema wazi, Mheshimiwa Rais Kikwete unisamehe. Uliweka watu madarakani ambao walituchelewesha kwenda mbele
Nimejiuliza huyu mtu naweza kuwa Rais kweli.Huku akijisibu serekali ya JK imefanya makubwa,Huku anakiri maendeleo yamecheleweshwa kwa uteuzi mbovu wa JK
Huyu mtu ni wa kuangalia mara mbili mbili,La sivyo tutazamisha taifa

Watu hao ni Lowasa, Masha, Medeye, Mahanga na mafisadi mengine ambayo yameambiwa yaondoke
 
Mkutano wa kampeni wa Chama chaapinduzi umeisha pale Jangwani mengi yameongewa lakini Mimi nataka nililete hili tu moja kwenu wana Jamvi.
Kwanini JPM hakumtambulisha mkewe kwamba leo nimekuja na mama watoto wangu jamani napenda nimtambulishe kwenu jambo hilo likafanywa na Mheshimiwa rais je kuna nini ndani yaakeee???
 
Dharau zako kwa Rais Kikwete na Serikali yake,mwisho wake Jumapili. Dharau zako dhidi ya watanzania wafanyakazi,wakulima na wafanyakazi zitakoma Jumapili.

Dharau zako za kujiona wewe ndiye mchapakazi na msafi pekee chamani,zinafikia tamati Jumapili. Dharau zako za kupania kutumia mabavu hata kwa mambo ya kisheria,zinagota Jumapili. Utajuta kuwafahamu watanzania!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Mkuu vipi JPM anakuja kuwanyima ulaji nini?? Mlizoea nalenale eeeh,, mfanye kazi sasa na kuishi kwa kufuata sheria... Mwisho wa wazembe sasa!!! Kumbe wewe ndio yale masalia unategemea kuishi kwa huruma,, pole sana...
 
Angekuwa hwara yake yule aliyempa nyumba ya serikali angemt
ambulisha. This is the type of president you want?
 
Hivyo huyo Kikwete anaondoka madarakani kwa lipi? Rais aliyewafahamu wauza madawa ya kulevya, majangiri wa wanyama wetu, wezi wa EPA, raisi aliyeasisi Escrow, Richmond na mafisadi. Na wote hao hakuwachukulia hatua au kuwajibika mwenyewe. Aende zake tumemchoka.
 
Kwanza ashukuru hata mungu kwamba tulikuwa wajinga kiasi cha kumchagua yeye kama Rais.

Mafuriko leo yameshindikana. Imebdi watu wakae ili uwanja uonekane umejaa. watu wangesimama ule uwanja hata nusu uisngefika. Watu wamejitawanya kwa kukaa!
 
Magufuli:
Wana Dar es Salaam nadhani mmesikia kuna watu ambao waliwahi kuwa katika nafasi za juu serikalini, wengine waliwahi kuwa Mawaziri Wakuu na washauri wa karibu wa Rais, lakini bila aibu na kumwogopa Mungu wanasimama kwenye makujukwaa na kusema CCM haijafanya lolote. Swali la kujiuliza, kama CCM haijafanya lolote, wao walikuwa wanafanya nini kwa miaka zaidi ya 12 wakiwa Mawaziri wakuu au washauri wa Rais. Kwa nini walibaki ndani ya serikali wakilipwa mishahara wakati walikuwa hawafanyi chochote. Kulipwa mishahara bila kufanya chochote serikalini ni kuwaibia Watanzania. Hawa watu wanasimama kwenye majukwaa wakiwaambia watanzania kimantiki waliwaibia pesa yao kwa miaka zaidi ya 12 kwa sababu hawakufanya lolote wakati tukiwa Mawaziri Wakuu.
 
Kuna tatizo tena kubwa, hii ni mara ya pili Kikwete analazimisha kumtambulisha mke wa Magufuli mara ya kwanza ilikuwa siku ya uzinduzi.

Hata alipoletwa Magufuli aliondoka akabaki Janeth na Kikwete, alipopewa nafasi ya kuomba kura akasema tumpe mheshimiwa Magufuli badala ya Mme wangu Magufuli, kuna kitu hakiko sawa.
 
Tumeona mmeweka viti ili vichukue sehemu kubwa ya uwanja, tumeona.
Tumeona pia wanafunzi wa secondary(Zanaki secna shule nygine) walivyolazimishwa kuuzuria, Tumeona.
 
Sasa akapumzike na tutaona kama tunaweza kumfikiria kumpa hata wenyekiti wa kijiji maana hata Taaluma yake aliyosomea tunaitilia mashaka mashaka kutokana na uwezo mdogo wa kujieleza na kutoa hoja katika kampeni zake za miezi miwili. # VIVA, VIVA a UKAWA.
 
Watu hao ni Lowasa, Masha, Medeye, Mahanga na mafisadi mengine ambayo yameambiwa yaondoke

Nyani haoni kundule.,nani asieyemjua Andrew chenge.,,anna tibaijuka.,ngeleja.,nyalandu..na wengine kibao tu waliopo kwa mafisiem???au ukiondoka ndo ufisadi unapianzia??!!
 
Magufuli:
Ninafahamu Dar es Salaam mna tatizo la Maji. Kuna mradi wa maji haujamalizika kwa sababu kuna baadhi ya watu wamepeleka zuio mahakamani. Kesi mpaka sasa inasua sua mahakamani wakati tunapoteza watu kwa sababu ya magonjwa kama kipindupindu. Swali la kujiuliza, Kwa nini kesi haimaliziki Mahakamani ili mradi wa maji umalizike kuepusha maafa ambayo tunaweza kuyazuia. Nikiwa Rais siwezi kuingia kazi za Mahakama lakini nitajenga mazingira ya kuwezesha kesi kuisha haraka na kwa ufanisi.
Uongo Uongo Uongo!!!!!
 
Back
Top Bottom