Yaliyojiri Jangwani, Dar: Mkutano wa kuhitimisha Kampeni za mgombea Urais wa CCM, Dr. Magufuli

pmoses95 kwa akili yako finyu unaona huu ni uchochezi kisa tu unapingana na kauli za kibabe. ushauri wako wapelekee ccm
huu ni uchochezi. uwe makini na post zako mwisho wa siku jamii forum haitakuja kukuchomoa lupango, nimetoa ushauri tu lkn
 
ImageUploadedByJamiiForums1445687000.703222.jpg
 
Kama mtanzania wa kawaida tena ninaekabiliwa na umaskini mkubwa ninatamani sana kuona nchi yangu ikipata uongozi imara utakaoleta mabadiliko yatakayozaa huduma bora za jamii kama Elimu,Maji Safi na Salama,Miundombinu bora,AFYA nk.Kufupisha hadithi licha ya baadhi ya watu wengi wakiwemo ndugu,jamaa,marafiki na wengine mashuhuri kwelikweli ktk siasa za nchi hii kuamini kuwa upinzani unastahili kupewa dhamana ya kuongoza Taifa letu nimekua nikisita na kushindwa kuungana nao nikiamini UPINZANI bado haujakomaa vizuri,haujajipanga vizuri na jambo hili liko wazi hata katika maamuzi,sera,aina ya viongozi wanaokumbatiwa na HATA umakini katika mambo madogo madogo lakini muhimu.Kwa mfano siku ya uzinduzi wa kampeni za UKAWA mgombea Mh Edward Lowassa alituelekeza mahali pa kwenda kuisoma HOTUBA aliyoshindwa kuisoma,SASA naomba tuitembelee TOVUTI ya CHADEMA kisha tulinganishe na ya CHAMA CHA MAPINDUZI na kisha tumalizie na ya IKULU.

*SEE ATTACHED PHOTOS*
Na ndio nalazimika kuhitimisha kwa kusema "ukishindwa kuwa makini katika mambo madogo hakika makubwa hutayaweza"na Wa mbili havai moja!
 

Attachments

  • chadema na slaa.jpg
    chadema na slaa.jpg
    17.7 KB · Views: 119
  • rais na mgeni.jpg
    rais na mgeni.jpg
    26.3 KB · Views: 117
  • ccm.jpg
    ccm.jpg
    34.8 KB · Views: 122
  • rais na mof.jpg
    rais na mof.jpg
    26.4 KB · Views: 112
  • ametangazwa.jpg
    ametangazwa.jpg
    16.3 KB · Views: 111
UPDATES JANGWANI
Baadhi ya picha za wananchi Jang'wani.

12107871_903630526385510_1008124874376697407_n.jpg

Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi

Mgombea Urais kupitia chama cha mapinduzi ameingia viwanja vya Jangwani akiongozana mkewe pia ameongozana na watu wengine kadhaa.

Anaeingia sasa ni mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.

Anaehutubia kwa sasa ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi, Dr. Jakaya Kikwete na anaongelea kukosekana kwa Samia ambae leo yupo Zanzibar kuhitimisha kampeni Visiwani.

Kikwete: Nampongeza sana kwa kuizunguka nchi hii kwa gari, hakupanda helicopter, wengine wamepanda helicopter na wameshindwa kuhutubia, anasema watu wakasome kwenye website, wananchi wa kawaida wanauliza huko website ndio wapi?

Magufuli bado una nguvu, nakuombea afya njema, leo na kesho ili kesho kutwa tufanye uamuzi wetu kukuthibitisha kuwa Rais wetu na mama Samia kuwa makamu wa kwanza mwanamke. CCM haikukosea kukuteua, umekamilika na watu wetu tunawajua. Wanaoifaa Tanzania tunawajua.

Mchakato umeendeshwa vibaya! Mzee yule hataki kusema kweli kwamba aliemtaka hakupata! Utaratibu uliotumika na chama mwaka huu ulianza kutumika kwa mara ya kwanza 1995, haujafanyiwa mabadiliko, mwaka 1995 nilikuwepo na tulikuwa wagombea 17, halmashauri kuu ya taifa ilileta majina 5.

Mzee yule mjumbe wa kamati kuu, 2005 hapakuwa na mabadiliko yoyote, tulikuwa wagombea 11, kamati kuu ilileta majina matano, mzee Msuya, Kigoda, Sumaye na mimi na mzee alikuwa halmashauri kuu, taratibu hazijaharibika. 2005 alikuwepo kwa utaratibu ulele, mzee Mkapa alikuja na majina yake mfukoni? Kwenye NEC alikuwa yeye wa mwisho kwa kupata kura 30 tu.

Mzee yeye alimpenda mtu na chama kwa vigezo vyake mtu wake hakukidhi sifa na kusema chama kinaendeshwa vibaya si kweli, tumeona naye anajaribu kuzungusha mikono imemshinda. Ndugu Magufuli mimi sina wasiwasi kwamba watanzania tarehe 25 watakupigia kura nyingi sana.

Magufuli
Nanawasukuru sana wana Dar es Salaam kwa kunipa makaribisho haya makubwa. Katika ziara yangu hapa Dar es Salaam nimekutana na bendera za vyama mbali mbali. Hii imenipa faraja na ujumbe unaoniambia nikichaguliwa kuwa Rais lazima nikawatumikie wananchi wote.

Nimetembea kwa gari Kilometa 46,221 nchini . Nimefanya hivyo kwa maksudi kwa sababu nilikuwa ninataka kukutana pia na adha za kimaisha kama wananchi wengine wanavyokumbana nazo. Nilitaka kukutana ana kwa ana na watanzania wengi .

Ujumbe wangu kwa wana Dar es Salaam na watanzania wote ni kupambana na rushwa na ufisadi. Nitahakikisha kwa nguvu zangu zote na kwa kumtanguliza Mungu, ninapambana na rushwa na ufisadi kwa sababu hii ni kansa kitaifa.

Wala rushwa na mafisadi sehemu yao ya kuishi ni gerezani.

Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere aliwahi kusema, katika nchi yenye amani, tatizo kubwa huwa ni rushwa. Tanzania ya Magufuli lazima tuhakikishe wala rushwa na ufisadi maisha yao yanakuwa ndani ya gereza.

Nilipochaguliwa kuwa mgombea Urais wa Tanzania, kuna mafisadi wamekimbia CCM. Nasema kama kuna ambao wamebaki waondoke. Tunataka nchi hii isonge mbele. Watu wengi wamechoka na rushwa, Ufisadi na blabla. Mimi kwangu ni Kazi tu. Nitaunda mahakama maalum ya kushughulika na mafisadi.

Nitaunda Baraza la Mawaziri lenye Mawaziri wachache, waadilifu na wachapakazi.

Nitapambana na adha za wafanyakazi wa kipato cha chini. Nitaboresha maslahi yao kuanzia walimu, manesi, madaktari, polisi, wanajeshi. Nitaweka mazingira mazuri ya sehemu zao za kazi. Ninafahamu wafanyakazi kwa sasa wanakatwa 11% PAYE. Nitahakikisha ninaishusha chini ili wafanyakazi waweze kuwa na kipato kinachowawezesha kuishi kwa furaha.

Mimi ni rafiki wa wafanyakazi, ninayatambua matatizo ya wafanyakazi. Nimewahi kuwa mwalimu na Mke wangu ni Mwalimu wa shule. Tumeyaishi matatizo ya wafanyakazi.

Naomba pia nisema, lazima wafanyakazi wafanye kazi na wale wachache ambao hata kama utawapa mamilioni lakini hawawezi kuacha kupokea rushwa, lazima wajiandae au watubu. Mfanyakazi akiharibu kwangu hakuna kuhamishwa. Kazi yake inakuwa imeisha. Sitaki kuwa mnafiki. Hata vitabu vya Mwenyezi Mungu vinasema, na asiyefanya kazi asile.

Serikali yangu hakuna kuwasumbua Mama Lishe. Nitahakikisha ninaboresha maeneo yao ya kazi.

Hakuna kusumbua waendesha bodaboda. Nitahakikisha ninaboresha kazi zao.

Nitahakikisha waendesha Bajaj na pikipiki wanatengenezewa njia yao maalum ili nao pia waruhusiwe kuingia hata katikati ya Jiji. Jiji nila watu wote na hata waendesha pikipiki lazima wafanye kazi zao sehemu yoyote kwa furaha bila kubughudhiwa na mtu yoyote.



Nitawapatia Watanzania Mabadiliko bora na siyo bora mabadiliko.

Nitakuwa mtumishi wa Watanzania ambaye nitafanya maamuzi sahihi na siyo maamuzi magumu kwa sababu hata mafisadi, majambazi na vibaka wanafanya maamuzi magumu.

Ninafahamu Dar es Salaam mna tatizo la Maji. Kuna mradi wa maji haujamalizika kwa sababu kuna baadhi ya watu wamepeleka zuio mahakamani. Kesi mpaka sasa inasua sua mahakamani wakati tunapoteza watu kwa sababu ya magonjwa kama kipindupindu. Swali la kujiuliza, Kwa nini kesi haimaliziki Mahakamani ili mradi wa maji umalizike kuepusha maafa ambayo tunaweza kuyazuia. Nikiwa Rais siwezi kuingilia kazi za Mahakama lakini nitajenga mazingira ya kuwezesha kesi kuisha haraka na kwa ufanisi. Ninaheshimu sana mihimili ya nchi ambayo ni Dola, Bunge na Mahakama.

Suala la tatizo la umeme linashughulikiwa na ninawakikishia katika utawala wangu, nitaliondoa tatizo la umeme.

Katika kuondoa au kupunguza msongamano wa magari, serikali ya awamu ya tano , itajenga barabara za juu katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam huku akieleza kutaanzishwa mfuko maalumu kwa ajili ya kuboresha barabara za Jiji hilo.Barabara ya juu eneo la Tazara itaanza kujengwa kwani tayari mkandarasi amepatikana.

Kama mkinichagua kuwa Rais, kuanzia mwaka ujao kutakuwa hakuna kulipa karo kwa wanafunzi kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne.

Serikali yangu itatoa milioni 50 kwa kila vikundi vya vijana na kina mama kwa kila mtaa/kijiji ili waweze kutumia kama mtaji.

Wana Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla nadhani mmesikia kuna watu ambao waliwahi kuwa katika nafasi za juu serikalini, wengine waliwahi kuwa Mawaziri Wakuu na washauri wa karibu wa Rais, lakini bila aibu na kumwogopa Mungu wanasimama kwenye makujukwaa na kusema CCM haijafanya lolote. Swali la kujiuliza, kama CCM haijafanya lolote, wao walikuwa wanafanya nini kwa miaka zaidi ya 12 wakiwa Mawaziri wakuu au washauri wa Rais. Kwa nini walibaki ndani ya serikali wakilipwa mishahara wakati walikuwa hawafanyi chochote. Kulipwa mishahara bila kufanya chochote serikalini ni kuwaibia Watanzania. Hawa watu wanasimama kwenye majukwaa wakiwaambia watanzania kimantiki waliwaibia pesa yao kwa miaka zaidi ya 12 kwa sababu hawakufanya lolote wakati tukiwa Mawaziri Wakuu. Hii ni dharau kwa Watanzania.

Hawakufanya lolote kwa Miaka zaidi ya 12 wakiwa Mawaziri Wakuu lakini leo wanatuomba tena tuwape nafasi nyingine waende tena kupokea Mishahara bila kufanya chochote. Watu wa aina hii lazima tuwakatae.

Mtu ambaye hafahamu Taifa limetoka wapi na liko wapi, hawezi kufahamu linakwenda wapi. Ninaifahamu vizuri Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla ya wakati wa utawala wa Awamu ya Kwanza, Awamu ya Pili, Awamu ya Tatu, na pia utawala huu wa Rais Kikwete. Ninafahamu Dar es Salaam inakotaka kwenda kimaendeleo. Nawaomba mnichague kwa kura nyingi ili nikamilishe malengo yenu kimaendeleo.


Haya baba kanyaga twende
 
Back
Top Bottom