Clemence Baraka
JF-Expert Member
- Sep 4, 2012
- 1,693
- 652
Wakati mwingine nachelea kuamini kuwa hawa ndugu zetu wa kutoka kaskazini yaani wakina MANGI wana ukabila fulani kama wakikuyu wa Kenya vile na hili limenisononesha sana pale lilipofanywa na watu ambao ni wasomi wa wakiwa wanahisa wa AKIBA COMMERCIAL BANK!!! Mimi ni mwanahisa wa hii benki na huko nyuma ilikubalika kuwa mwenyekiti wa hiyo benki atatokana na wawakilishi wa wanahisa wadogo wazalendo katika bodi; sasa cha kushangaza ni kwamba safairi hii tumewachagua wawakilishi wawili ambao sio wachaga na matokeo yake ni kwamba mkurugenzi mchaga ambae ni mzalendo lakini anawakilisha corporate shareholders ameweza kuwashawishi wanahisa wazungu wakubali kuwa utaratibu sio kuwa mwenyekiti atokane na wawakilishi wa wanahisa wadogo bali wanahisa wote wazawa kitu ambacho kilimuhalalisha yeye kupewa huo uenyekiti na hao wazungu wanaoshirikiana nae kuihujumu hiyo benki; ukweli ni kwamba nyuma ya pazia, mbinu hii ilitumika ili kuhakikisha kuwa MCHAGGA ndio anakuwa mwenyekiti wa hii benki na sio vinginevyo!!! Ukabila wa namna hii lazima tuupige vita kama tunavyowapiga vita magamba!!
Ndugu yangu huyo unayemsema ndie mwanzilishi wa hiyo benki. Yaani kupewa uenyekiti tena kwa kura za wajumbe inakutia simanzi? Kwa kweli roho zetu nyeusi kama tulivyo na ndio maana hata kupata riziki kwa Mungu inakuwa ni kazi.