Yaliyojiri Harambee ya CHADEMA live ITV - Oktoba 31, 2014

wajinga hawataisha. hivi chadema ni serikali?kama ccm imeshindwa kufanya hayo mambo wakiwa serikalini kwanini tuwape kura kama serikali wanazidiwa na chama kimoja cha upinzani tena kinachoendeshwa kwa ruzuku na michango ya wananchi ndo ujiulize kodi zetu zinaenda wapi.
Siku zote huyo Ifweero mimi huwa namuita kichwa maji,yeye anaongelea matsngazo ya cdm?mbona hasemi lichama lao linalo firisi watanzania kwa ktuibia kodi zetu?
 
Tatizo siyo kuchangia tatizo ni jinsi gani fedha hizo zitatumika! Maana hawa CDM ni wajanja wajanja sana maneno mengi kumbe wanalao jambo!

Tupeni mrejesho wa harambee za nyumba kwanza then tuanze kuchangia!
Wana cdm hatuhitaji fedha za majangili ccm
 
Chadema Yatikisa

- Yaja na mpango Changia Chadema
- Mbowe: Ukawa ni mpango wa Mungu
- Dr.Slaa : Mapambano yanaendelea.


Na Edger Yoram Mwankuga

Katika hali inayoonyesha Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema), kudhamiria kukiondoa Chama cha Mapinduzi (CCM) madarakani, jana chama hicho kimezindua mpango wa wanachama na wapenzi wa chama hicho na wapenda mageuzi kuchangia fedha chama hicho ili ziweze kuchangia harakati za kuleta mageuzi katika siasa za Tanzania. Huu ni mpango wa kwanza kufanywa na chama cha siasa Tanzania kwa kuwaunganisha wananachama na wapenzi wa chama hicho kupitia simu za mikononi. Hayo yalifanyika jana katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na chama hicho katika hotel ya Serena (zamani ikijulikana Kilimanjaro Hotel) jijini Dar es Salaam na kulushwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha ITV kuanzia muda wa saa 3 usiku hadi saa 5 usiku.

Programu zilizozinduliwa ni pamoja na e – membership ambayo inawawezesha wananchi na wapenzi wa chama hicho kujiunga na kuwa wananachama wa chama hicho kwa njia ya mtandao. Program ya pili ni ile inayojulikana kwa jina la e – media ambayo inawawezesha wanachama na wananchi wengine kupata taarifa za chama hicho kupitia simu zao za mkononi kama yanavyofanya makampuni ya simu. Program ya tatu na ya mwisho ni ile ya e – movement ambayo inaeleza namna ya kuwashirikisha wananchi katika kuleta mageuzi katika siasa za Tanzania.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mheshimiwa Freeman Mbowe akizindua program hizo, waliwaambia waliohudhuria hafla hiyo na wananchi wote kwa ujumla, kuchangia kwa hali na mali katika harakati za kulikomboa taifa na kuwaondoa CCM madarakani ambao wamekuwa wakitumia umasikini wa Watanzania kama nafasi ya kuendelea kubaki madarakani. Aidha Mbowe alisema "umasikini usiwe kikwazo kwa wanachama kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, bali uadilifu na uaminifu ndiyo viwe vigezo vya mtu kuomba nafasi za uongozi na kwamba fedha ambazo zitachangwa na wananchama na wapenda mageuzi zitatumika kama ilivyopangwa".

Utangulizi.

Kabla ya kuanza hafla hiyo, mcheleheshaji ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema upande wa Zanzibar, Salim Mwalimu, alianza kwa kuwakaribisha wageni na watu wote walioalikwa katika hafla hiyo. Miongoni mwa watu walioalikwa ni pamoja na viongozi wa vyama vya siasa vinavyounda Ukawa ambao ni Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi , James Mbatia, Emmanuel Makaidi, Mwenyekiti wa NLD, wakati Profesa Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa CUF hakuhudhuria. Pamoja na viongozi hao, baadhi ya wabunge wa vyama hivyo na madiwani walihudhuria, huku salaam ya "People's Power" na Ukawa vikitawala ukumbini hapo.
Aidha uzinduzi wa program hizo ulitanguliwa na sala zilizoongozwa na Isa Mohamed, Makamu Mwenyekiti Chadema upande wa Zanzibar kwa upande wa Uislamu wakati upande wa ukristo, sara iliongozwa na Mchungaji Peter Msigwa ambaye pia ni mbunge wa Iringa Mjini (Chadema).

DR. SLAA.

Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu wa chama hicho Dr.Slaa aliwaeleza waliohudhuria hafla hiyo lengo na madhumuni ya hafla hiyo, ambayo ni pamoja na wananchi kushiriki katika kuchangia fedha na mambo mengine katika harakati za kulikomboa Taifa katika makucha dhalimu ya CCM. Katibu Mkuu huyo alitumia nafasi hiyo kuwatupia vijembe wale wote wanaozusha kwamba mke wake "amechukuliwa" na wengine kwa kumsimamisha na kumtambulisha mbele ya kadamnasi.
Pamoja na mambo hayo, Dr.Slaa alitumia muda mwingi kueleza historia ya chama hicho ili kujibu mapigo kwa wale wote wanaosema Chadema ni chama cha Kaskazini/wachaga. Dr. Slaa alieleza kwamba Chadema kilisajiliwa rasmi mwaka 1992 na kwamba tangu hapo, chama kimekuwa kikikua kwa haraka sana. Aliwataja wanzilishi wa chama hicho pamoja na maeneo wanakotoka ambao ni Edwin Mtei (Kilimanjaro), Bob Makani (Shinyanga), Vitor Kimesela (Manyara), Brown Ngugwaulupi (Mbeya), Sarang'a (Singida), Masinde (Ukerewe), Merik (Pemba), Mary Kabigi (Rukwa), Wasira (Mara) na Philipo Silembi (Shinyanga).

Kwa mara ya kwanza, Chadema kilishinda kiti cha ubunge katika uchaguzi wa marudio Kigoma mwaka 1994 ambapo Dr. Kabolou aliibuka mshindi. Mwaka 1995 katika uchaguzi Mkuu, Chadema kilipata wabunge watatu ambao ni Sarakana (sasa marehemu), Dr.Slaa na mbunge wa viti maalum Mary Kabigi. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 Chadema kilipata wabunge wanne ambao ni Dr. Slaa (Karatu), Ndesamburo (Moshi Mjini), Dr.Kabolou (Kigoma Mjini) na mbunge wa viti maalum Grace Kihwelu na madiwani 72. Mwaka 2005, idadi ya wabunge iliongezeka hadi kufikia 11 na kwa mara ya kwanza chama hicho kilimsimamisha mgombea urais ngazi ya Taifa,Mhe.Freeman Mbowe ambaye alipata kura zaidi ya laki sita.

Katika uchaguzi wa mwaka 2010, Chadema kilipata wabunge 48 huku mgombea urais, Dr.Slaa akipata kura 26% ya kura zote zilizopigwa na hivyo kumanisha Chadema inakua kwa kasi kubwa sana.
Dr slaa alisema, Chadema ina agenda kuu mbili ambazo ni kusimamia uchumi utakaowafaidisha wananchi wote, na kukemea ufisadi ili rasimali za nchi ziweze kutumika kwa manufaa ya wananchi wote. Aidha Dr Slaa alisema Chadema imechangia katika kuleta mabadiliko katika nchi na kwa sasa wananchi hawaogopi kudai haki zao na kwamba kazi ndio imeanza.

Kuhusu mchakato wa katiba, Dr slaa alisema, haikuwa agenda ya CCM kuanzisha mchakato wa kutengeneza Katiba mpya na ndio maana mchakato umechakachuliwa. Hiyo ilikuwa sera ya Chadema ambayo ilikuwepo kwenye ilani ya uchaguzi mkuu mwaka 2010, ingawaje Rais Kikwete alipotosha kusema kwamba Chadema ingeweza kutengeneza Katiba mpya ndani ya siku 100. Na kwa kuwa mchakato huo umechakachuliwa aliwaomba wananchi kuipigia kura ya HAPANA katiba inayopendekezwa na kwamba harakati za kudai katiba mpya itakayozingatia masilahi ya wananchi wote ndiyo kwanza zimeanza.


JOSEPH MBILINYI (SUGU) NA JOSEPH HAULE (PROFESA J).


Katika hafla hiyo pia alikuwepo Joseph Mbilinyi (Sugu) ambaye ni mwanamuziki na mbunge wa Mbeya Mjini – Chadema na mwanahiphop Joseph Haule (Profesa J) ambao walipata nafasi ya kutumbuiza. Mbilinyi aliwaeleza waliohudhuria hafla hiyo kwamba watatumia muziki katika kuleta mabadiliko katika taifa, ambapo watazunguka nchi nzima kuwahimiza wananchi kuikataa Katiba Inayopendekezwa, kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kushiriki kimamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao utafanyika tarehe 14 Desemba, 2014. Pamoja na kwamba vyombo vya muziki havikuwa vinatoa sauti kwa ukamilifu, Sugu na Profesa J waliwainua vitini waliohudhuria hafla hiyo huku wengine wakisimama na kupunga mikono juu huku wakionyesha alama ya vidole viwili. Baada ya kumaliza kutumbuiza, wasanii hao waliwagawia CD za nyimbo viongozi wa chama.


MHE.FREEMAN MBOWE.


Kabla Mwenyekiti hajazindua programu hizo, alitumia muda wa zaidi ya dakika 20 kuhutubia umati wa watu waliohudhuria hafla hiyo na wananchi kwa ujumla waliokuwa wanafuatilia shughuli hiyo kupitia luninga na mitandao ya kijamii, huku Ukawa ikichukua nafasi zaidi.


UKAWA.


Mbowe alianza kwa kuwashukuru sana viongozi wa vyama vinavyounda Ukawa kwa kuweza kuhudhuria hafla hiyo na kuonyesha maana halisi ya ushirikiano. Viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Taifa, na mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Emmanuel Makaidi, Mwenyekiti wa chama cha NLD na mwenyekiti mweza wa Ukawa, huku Profesa Lipumba akitoa udhuru wa kutohudhuria kikao hicho, lakini viongozi kadhaa wa CUF walihudhutria hafla hiyo.
Lengo la muungano wa Ukawa ni kupeleka ujumbe na kilio kwa watanzania na kuwakumbusha kwamba watanzania wanaweza kuligeuza Taifa kuwa la neema na wala Mungu hakuwaumba Watanzania kuwa wa kulialia tu .

Aidha alieleza kwamba, Ukawa ni mpango wa Mungu na hivyo hautavunjuka kama wengine wanavyosema. Ukawa imedhamilia kuufanya ushirika kuwa wa kweli na upendo ambao utaondoa kilio cha watanzania, na kwamba wataenzi kila fursa na uwezo wao kuhakikisha umoja huo unadumu na kujibu kiu ya watanzania, na aliwabeza wale wote wanaoonyesha hofu ya kuvunjika kwa ushirika huo.
Baada ya kusema hayo Mwenyekiti alizindua program tatu ambazo ni e – membership, e – media na e – movement. Wakati huduma zingine zikitarajia kuanza mapema wiki ijayo, programU ya kuchangia ilianza mara moja ambapo Mwenyekiti aliwaeleza waliohudhuria hafla hiyo na wananchi kwa ujumla namna ambavyo wanaweza kuchangia fedha chama kupitia simu zao za mikononi kwa njia ya Mpesa ,Airtel Money na Tigo Pesa.

Hata hivyo ni MPESA tu ambayo ilikuwa tayari kutumika wakati huduma zingine zikitarajia kuanza jumatatu ijayo. Aliwaongoza watu wanaopenda kuchangia fedha chama hicho hatua za kufuata katika kutumia fedha. Hatua hizo ni kama ifuatavyo:
MPESA. · *150*00 · LIPA KWA MPESA- CHAGUA NAMBA 4 · INGIZA NAMBA YA KAMPUNI AMBAYO NI 213040 · INGIZA KUMBUKUMBU YA MALIPO UTAANDIKA M4C(ikifuatiwa na jina ila sio lazima) · WEKA KIASI · NAMBA YA SIRI · THIBITISHA. Hadi matangazo ya moja kwa moja yalipokuwa yanasitishwa tayari kiasi cha Tshs milioni sita kilikuwa kimepokelewa ambapo upokeaji wa fedha hizo ulikuwa unaonekana wazi katika screen kubwa iliyokuwapo ukumbini hapo, huku watu wengine wakiahidi kukichangia fedha taslimu chama hicho.

Peter Msigwa ambaye ni mbunge wa Iringa Mjini na mjumbe wa kamati ya kuchangisha fedha, aliwashukuru wananchi wote waliokichangia chama hicho, na kwamba wafanyabiashara wasiogope kukichangia chama hicho kwani hiyo ndio njia pekee ya kuwaondoa CCM madarakani .Kwa upande wa kamati hiyo inayoundwa na wengi wa wabunge wa chama hicho, ilikuwa imekusanya zaidi ya shilingi milioni mia hadi kufikia siku ya jana.


Chadema ni chama cha kwanza nchini kutumia njia ya teknolojia kuwafikia wananchi na wanachama wake na kufanya iwe rahisi kwa wanachama kukichangia fedha chama hicho. Katika dunia ya Sayansi na Teknolojia, ni vema kutumia fursa zinazojitokeza ili kuongeza ufanisi. Kwa sasa wananchi wengi wana simu za mkononi na hivyo kama programu hizo zitakuwa endelevu ni wazi kwamba zitakisaidia sana chama hicho kuliko kutegemea ruzuku ya serikali.

Katika wakati huu ambapo kuna manunguniko ya chini kwa chini ya matumizi mabaya ya fedha za ruzuku ni vema chama kikawa na mfumo wa uwazi katika matumizi ya fedha hizo ili kutowakatisha tamaa wananchi katika kuchangia chama hicho.


Katika uchaguzi mkuu huko India, uliofanyika mapema mwaka huu, kulijitokeza chama kidogo cha Aam Aadmi Party (Common Man's Party) kikiongozwa na Arvind Kerjriwal ambacho kimeanzishwa miaka miwili iliyopita. Kutokana na udogo wake isingekuwa rahisi kwa chama hicho kufurukuta mbele ya vyama vikubwa vya Indian Congress Party na BJP. Kwa kuona hivyo chama hicho kilizindua kampeni ya mtandao ili wananchi waweze kukichangia ili kuweza kujiendesha. Katika hali ambayo haikutarajiwa , chama hicho kilipata fedha nyingi ambazo zilisaidia chama hicho kuwasimamisha wagombea karibu sehemu zote za nchi hiyo.Hata kama chama hicho hakikushinda uchaguzi huo, lakini nguvu ya sayansi na technolojia ilionekana. Hivyo programu zilizozinduliwa na chadema ni ubunifu mzuri na kama mambo yatakwenda kama walivyopanga basi watanzania wanaweza kushuhudia mabadiliko makubwa sana katika siasa za Tanzania.
 
CCM inachangiwa na wezi kama IPTL, Dowans, makampuni ya mafuta, wahindi ndo maana wafanyabishara hawataki kulipa kodi kisa wanasubiri uchagizi ukifika wachangie chama chakavu hafj wao wanasamehewa kodi.

CCM wanaongoza hii nchi nzima na hao wote uliowataja, pamoja na wewe na baba'ko na chama chako. Kumbuka hilo.
 
aweke wazi iyo mikataba kama anasadifu sera yake ya utawala bora uone madudu aliokubaliana nayo mpaka kupata icho anachosaini utahama leo icho chama


Mikataba ya kibiashara si lazima iwe wazi. Unataka competitors wapige bao la kisigino?

Hivi hizi shule huwa mnasomea kuwa wajinga?
 
CHADEMA au UKAWA sio suluhisho ya mlalahoi kama mimi hapa Tanzania.

Usidhani watakulipia mahali,watakuungia bundle wala kukupatia pesa ya kununua bia au vocha.

Watu mjiongeze kwa kujituma wenyewe kijasiriamali na kadhalika.
 
Kutakuwa na harambee
ya CHADEMA itakayofanyika kesho tarehe 31/10/2014 katika ukimbu wa
Serena Hotel na kurushwa live na ITV kuanzia saa 3 usiku mpaka 5 usiku.

Katika harambee hiyo,CHADEMA watazindua matumizi ya teknolojia katika
siasa.

CHANZO:ITV

Tahadhari:TANESCO msitukatie umeme kwa kisingizio
chochote kile.


UPDATE:

JINSI YA KUCHANGIA;

MPESA
1.*150*00#
2.LIPA KWA MPESA-CHAGUA NAMBA 4
3.INGIZA NAMBA YA KAMPUNI AMBAYO NI 213040
4.INGIZA KUMBUKUMBU YA MALIPO UTAANDIKA M4C(ikifuatiwa na jina ila sio
lazima)
5.WEKA KIASI
6.NAMBA YA SIRI
7.THIBITISHA

NOTE:Kama hutaki jina lako lionekane,andika M4C tu.Ila kama unataka jina
lako lionekane andika M4C kisha ikifuatiwa na jina lako bila kuacha
nafasi,mfano M4CMbowe.
=====

umemnukuu vibaya dr slaa. marehemu ni mhe mama kabigi na sio salakana.
 
Upinzani mnawachangia akina Slaa kujegea mahekalu, mabwepande. Mbowe kununuwa majumba UK, Dubai.

Au huyajui hayo?

Dada FaizaFoxy nadhani waujua vyema usemi usemao..."Hiyari yashindwa Utumwa"Kama nimetoa kwa hiari yangu sioni shida.Hivi wakumbuka ni mara ngapi chini ya CCM tumechangia MABASI kwa ajili ya WANAFUNZI wa jiji la Dar es Salaam,yameishia wapi?Je hayakuishia mikononi mwawachache?

Hawajaomba pesa/michango kwa ajili ya kununua mabasi bali kwaajili ya kutoa elimu ya uraia kwa wale tusiokuwa na uelewa.

Sioni shida mtu wa kawaida akamchagua kiongozi bora bila kujali chama atokacho bali uelewa wake umemfanya amchague kiongozi sababu amepata uelewa.

Sitaona shida kuchangia kabisa kama nikiona wale akina mama wapewao rushwa ya shilingi elfu mbili au tano wanakataa kumchagua kiongozi mtoa rushwa sababu wamepata elimu.Hainipi shida kama wakikuchagua wewe Dada FaizaFoxy kwa sababu wamekuona ni kiongozi bora bila kutoa rushwa au khanga,tshir,skafu au sukari,lakini wameuona umuhimu wako kama kiongozi bora na wakakuchagua bila kujali chama utokacho,basi kwa elimu hii basi nitaendelea kuchangia kila siku.

Elimu ya uraia ni muhimu sana sasa kwa watanzania wasiojua wajue namna ya kuwawajibisha viongozi wezi,wala rushwa,mafisadi nk,siyo sababu wanatoka ukanda,kabila au dini fulani.
 
....Tena wabwia unga na punda ndo wanaochangisha michango kwa magamba !!!

Umeona eh,ndiyo maana hata kesi zao zinaishia pale zilipoanza tu.Hawajui hata ubaya wa hii kitu kwa Taifa letu,wanachojali wao mradi pesa za kuhonga wakati uchaguzi zimeingia basi
 
Wewe ndio hamnazo na kesho hazitakuwepo.

Hivi unajuwa mikataba mingapi ya maendeleo kasaini Kikwete China? nnauhakika hujui na wala hutaki kujuwa.

Hivi kwenu wapi? hakuna mabasi ya Yutong na ma lorry ya Howo yanayokwenda huko? au hujawahi kupita barabara mpya inatengenezwa na ukaona Wachina wako busy? unafikiri vinakuja au wanakuja tu bila kwanza kuwa na uhusiano?

Huyu unamjuwa? na hapa unajuwa ni wapi? na unajuwa katumia gharama ngapi kufika hapo?:




Punguani wahed.

FaizaFoxy hivi huwa muda mwingine akili yako unaipeleka wapi? au hiyo hijabu sio kwa ajili ya kujisitiri bali ni kuficha akili zako fupi? hiyo mikataba unayo isifia umesha wahi kuisoma? au ndio kujikomba tu kisa rais ni muumini mwenzetu?
 
Last edited by a moderator:
FaizaFoxy hivi huwa muda mwingine akili yako unaipeleka wapi? au hiyo hijabu sio kwa ajili ya kujisitiri bali ni kuficha akili zako fupi? hiyo mikataba unayo isifia umesha wahi kuisoma? au ndio kujikomba tu kisa rais ni muumini mwenzetu?

Funguwa akili yako iliyo finyu. Hakuna mkataba wa kibiashara hususan kubwa zenye ushindani wa Kimataifa ukawekewa wewe wazi uisome.

Hivi hizi shule huwa mnaenda kufundishwa ujinga?
 
Back
Top Bottom