Yaliyojiri Diamond Jubelee Tamko la Waislam - Video

Mohammed Hamad

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
3,988
1,301
Wadau ninavideo inayoonyesha yaliyojiri Diamond Jubelee kuhusu Tamko la waislam lakini nashindwa ku-upload msaada please.....

Note*

Video hii itasaidia kusikia kwa masikio sababu zilizopelekea kutoka kwa tamko ili kubalance mnapotoa comments zenu.



Ndugu zanguni nimeshindwa ku upload video clip ya yaliyojiri kwenye tamko la masheikh kujibu tamko la maaskofu kutokana na ukubwa wa file. Nimeona niwaleteeni summary na mwenye kutaka kujua zaidi atafute CD zinauzwa nje ya misikiti mikubwa kama mtoro, kiblateni na mingineo ni vizuri kwa mkristo na mwislam afahamu kilichojiri kuliko kusikiliza fitna. Sisi ni wamoja badi tudumishe umoja wetu kwa maneno na sio unafiki!


Summary:

Kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 CCM iliwaahidi waislam Mahakama ya kadhi na OIC. Waziri Benard Membe waziri wa mambo ya nje analihutubia bunge anasema "serikali imezuchunguza na imeona hakuna tataizo Tanzania kujiunga na OIC. Membe anaitwa na Polycap Membe anaambiwa njoo, Membe anaenda kwa Pengo walicho zungumza hakijulikani na alipotoka akarudi Dodoma akasema kama kuna jambo serikali halitaki kusikia basi ni OIC" Swali "msimamo wa serikali kutoitaka OIC ni wa Serikali au Pengo?"

Swali nani ana nguvu Serikali au Kanisa?"

Sikiliza, pengo kamwita Membe kamwambia njoo kiongozi wa dini amemwita kiongozi wa serikali kaitwa na kiongozi wa dini amekwenda viongozi wa kiislam kwa kujua nafasi yao wakaona sisi tumfate tusimwite wakaenda kwa membe wakaonana na PS wakamwambia Membe yupo? akasema yupo mwambie Masheikh wamekuja wanataka kuonana na wewe PS anarudi anawajibu hana nafasi ya kuonana na na Masheikh. Kiongozi wa kanisa akimwita kiongozi wa Serikali anaenda masheikh wakimfata hataki kuonana nao" Swali nchi hii nani ana nguvu? masheikh au kanisa?

Misamaha ya kodi.

Serikali imetaka kuopeleka mswada wa misamaha ya kodi Kanisa likachachamaa Srikali ilifuta mswada haikufuta mswada?"

Hatari ya pili ni ubaguzi wa kiuchumi.

Watz wote tunatoa kodi lakini sehemu kubwa ya pato la taifa linawanufaisha wakristo na taasisi zao zaidi kuliko waislam. Ubaguzi katika mambo ya uchumi.

Serikali kila siku inatuambia tunashukuru makanisa kwasababu yanasaidia serikali kuendesha huduma ya jamaii, mapadri na maaskofu tunawashukuru sana bila nyiyi hudama za jamii zingekuwa ngumu sana tunawashukuru kwa mashirika ya kiristo kwa kuisaidia serikali.

Swali hivi kweli Kanisa linaisadia serikali au serikali inaisadia kanisa? Inakuwaje? Serikali inakusanya kodi zikishakusanya wilayani haina hosp badala ya serikali kujenga hosp inachukua pesa inayapa kanisa kujenga hospital serikali yenyewe haijengi hospital hivi hapa nani kamsaidia nani?

Serikali katika kata hii haina shule badala ya kujenga inaipa kanisa pesa kujenga shule halafu baada ya kujenga Serikali inarudi kuishukuru kanisa yeye ndio anakusaidia wewe yaani yule uliempa mapesa ndio anakusaidia wewe sijui mnaelewa? hivi nani anamsaidia nani?

Kanisa inakuwa na uchumi wa aina tatu

1. Limepewa hela na serikali ikajenga kanisa
2. hosp ikijengwa vifaa vyote vya hosp havina kodi
3. Sio wanaotibiwa wanatibiwa bure (wanalipa)!

Nani anamsadia nani?

Shule:

Serikali katika bajeti yake lazma itenge pesa zitakazoenda kanisani kisa inaendesha shule. Serikali haijengi shule inategemea zinazojengwa na kanisa, mimi na wewe kama waislam tunakatwa kodi Serikali inaipa kanisa ili ijenge shule. zikishajenga shule kuna mfumo unaowazuia waislam wasizidi 10% kodi yetu inajenga shule waislam wanaambiwa wasizidi 10% kwa kodi yetu" Haya si maskhara madogo leo watoto wetu hawaendi shule lakini shule zinaendeshwa na kodi yetu. " mimi natoka mwanza sehemu kubwa ya mishahara ya hospital ya bugando inalipwa na serikali sehemu kubwa ya vivyaa vya hosp vimesamehewa kodi sehemu kubwa ya ukarabati wa hosp unasaidiwa na serikali na bado raia kujiandikisha tu ni 20,000 - 150,000 kujiandikisha tu baDO MAMBO MENGINE. oNA KANISA LINAVYOTENGENEZA PESA KWA KODI ZETU.

MoU

Mwaka 92' Kanisa limeitana na Serikali Wakatoliki wamemwita Josephat Lekulu askofu wa Arusha Serikali wakamwita Edward Lowasa na waprotestant wakamwita mwakilishi wao wakatengeneza makubaliano ya kugawana hela ya nchi....sheikh wa nchi hii hakutwa hata mmoja!!!!!Hawatuiti wanagawana kimyakimya Waislam hawamo.

Chini ya mfumo kristo, watajenga hiki kinafumuka kama uyoga wenzetu wanahela wenzao kutoka nje watawaletea zenu zikija magaidi hawa zimetoka uwarabuni kamata magaidi hawa! mnakaribia kukamuana mpaka uadui unazidi khaa sheikh jana elfu kumi na leo elfu kumi "posho"

Clip ni ndefu sana yameongelewa mengi sana ila hayo ni kwa uchache sana mwenye kuweza atafute CD mimi nimenunua jana baada ya sala ya ijumaa msikiti wa Vetenari.
 
Wadau inawezekaqna ku-upload video? nimejaribu nimeshindwa kama kuna mtu anajua nifahamisheni please.

Thanks.
 
Mkuu ka imeshindikana kabsaa, then try ku-upload kwa youtube then hapa tuwekee link, tutaiona tu.
Thnx for info kaka..)
 
Wadau ninavideo inayoonyesha yaliyojiri Diamond Jubelee kuhusu Tamko la waislam lakini nashindwa ku-upload msaada please.....

Note*

Video hii itasaidia kusikia kwa masikio sababu zilizopelekea kutoka kwa tamko ili kubalance mnapotoa comments zenu.


Ku-balance kitu gani?
 
Wazee hii clip itachukua takribani dakika 600 na kitu kuwa uploded
weka summary am sure there more important issues za kufatilia kuliko kukaa na kuangalia kitu ambacho sioni kama kinajenga....., source ya aliyesema haya maneno ni nani hadi yeye anajua uonevu wa watu kuliko watu wenyewe... au kuna evidence au ndio hizo connection za 1 + 1 ukapata 4 or its just hearsay and bla bla blah abra kadablah
 
Wazee hii clip itachukua takribani dakika 600 na kitu kuwa uploded


Mkubwauenda ukashindwa kabisa ku-upload hiyo clip
Kwanza hiyo clip ipo katika format gani na ina ukubwa upi?
Kama ni zaidi ya MB 100 haitaweza kuwa uploaded labda kwa muda mrefu sana
Cha kufanya kama ipo katika formart ya AVI badilisha katika formart ya FLV au MPG4 Kama huna hizo programe download kwenye inter
net any video conveter ili uchange fomart

kwani kwa file lenye MB 1000 Kama dk 15 hivi linaweza kuwa converted to 10-15MB by FLV

Byabato
 
maandishi tunayo, hiyo video haina msaada sana isikusumbue. Cha muhimu ni kwamba historia mbaya imewekwa kwamba waislamu walishapendekeza kuligawa taifa !!!
 
maandishi tunayo, hiyo video haina msaada sana isikusumbue. Cha muhimu ni kwamba historia mbaya imewekwa kwamba waislamu walishapendekeza kuligawa taifa !!!

Nitafurahi kama utanitoa uchafu wa masikio na tongotongo kivipi Waislam wanaiharibu nchi? Na swali dogo nini nafasi ya Kanisa kwenye nchi ambayo haina dini? Serikali na Kanisa ipi ina nguvu?
 
Mohammed Shossi said:
Shule:

Serikali katika bajeti yake lazma itenge pesa zitakazoenda kanisani kisa inaendesha shule. Serikali haijengi shule inategemea zinazojengwa na kanisa, mimi na wewe kama waislam tunakatwa kodi Serikali inaipa kanisa ili ijenge shule. zikishajenga shule kuna mfumo unaowazuia waislam wasizidi 10% kodi yetu inajenga shule waislam wanaambiwa wasizidi 10% kwa kodi yetu" Haya si maskhara madogo leo watoto wetu hawaendi shule lakini shule zinaendeshwa na kodi yetu. " mimi natoka mwanza sehemu kubwa ya mishahara ya hospital ya bugando inalipwa na serikali sehemu kubwa ya vivyaa vya hosp vimesamehewa kodi sehemu kubwa ya ukarabati wa hosp unasaidiwa na serikali na bado raia kujiandikisha tu ni 20,000 - 150,000 kujiandikisha tu baDO MAMBO MENGINE. oNA KANISA LINAVYOTENGENEZA PESA KWA KODI ZETU.

Mkuu wewe inaonekana ni Msomi, Kabla sijajadili Chochote nikuulize Swali kwamba Je Kwa Mtazamo wako Kuna Ukweli wowote katika haya Malalamiko?
 
Nitafurahi kama utanitoa uchafu wa masikio na tongotongo kivipi Waislam wanaiharibu nchi? Na swali dogo nini nafasi ya Kanisa kwenye nchi ambayo haina dini? Serikali na Kanisa ipi ina nguvu?

Ni Shule gani ya Kikristo Ambayo kuna Sharti kwamba Waislam wasizidi 10%
 
Nitafurahi kama utanitoa uchafu wa masikio na tongotongo kivipi Waislam wanaiharibu nchi? Na swali dogo nini nafasi ya Kanisa kwenye nchi ambayo haina dini? Serikali na Kanisa ipi ina nguvu?


Mkuu naheshimu sana michango yako mingi huwa ni constructive, usipoteze muda wako na mambo haya, udini ni mradi wa wajanja wachache wanaonufaika nao. tangu niwajuwe masheikh wao ndio wako front kuipinga serikali dharimu ya ccm bila kujari rais anatoka dini gani, Askofu Kilaini aliposema Kikwete ni chaguo la mungu sisi tunaoona mbali tulimpinga, na kumbuka kulikuwa na wagombea wa wakristo akiwemo mchungaji wa kanisa Mtikila, atimaye Kikwete akapata kura millioni 8+. mwaka jana kaambulia kura millioni 6, tatizo sio wakristo tatizo watanzania wameshamgunduwa kwamba ni kiongozi Dhaifu, sisi wapenda haki bila kujari vyama tulipenda upande wa ccm asimae kugombea Salim Ahmed Salim, lakini hakuna asiyejuwa fitina alizofanyiwa na kubdi la kikwete, ukila nyama ya mtu huwezi kuacha, kikwete aliingia madarakani kwa kutumia fitina basi ataendelea na fitina mpaka mwisho tuanze kuchinjana. kama swala ni udini mbona watu hawamtaki hata kumsikia Edward Lowasa lakini hujawi kumsikia mkristo amtete eti Edward Lowasa anachukiwa kisa ni mkristo! this is too low to me. sina imani na masheikh ubwabwa but I RESPECT MUSLIMS FAITH.
 
Nyie wakuu naona mnalishana sumu tu.....inaamana mapato yenu ya misikiti hayatoshi kugaramia mambo yenu sasa mmeanza kuigeukia serikali??
Nendeni shule mkuu maana hiyo misamaha ya kodi ipo kisheria kwa mtu yeyote anayejenga au kutoa huduma kwa jamii!! Mbona mengi hua anapewa hiyo misamaha sana!!! Je yeye ana kanisa??
Tengenezeni huduma za jamii hope nanyi mtapewa misamaha mingi tu
 
Nitafurahi kama utanitoa uchafu wa masikio na tongotongo kivipi Waislam wanaiharibu nchi? Na swali dogo nini nafasi ya Kanisa kwenye nchi ambayo haina dini? Serikali na Kanisa ipi ina nguvu?

Kama ni haya ndiyo mlioongea Diamond basi wala usijisumbue ku-upload hiyo video. Watu wanaposema serikali haina dini haina maana kuwa raia wake hawana dini. Maana yake ni kuwa dini haina kipaumbele katika maamuzi na utawala wa serikali. Machoni mwa serikali, Mohammed Shossi ni raia na uislamu wake ni sekondari.; Fundi Mchundo ni raia na ukristu wake ni sekondari. Vile katika utawala wa kidunia serikali ina nguvu kuliko dini yeyote ile ( ukristu, uislamu n.k.) lakini katika mambo ya imani, dini ina nguvu kuliko serikali. Bernard Membe mbele ya Polycarp ni muumini wa kawaida wa dhehebu lake ( mmoja kati ya kondoo alioagizwa kuwachunga). Bernard Membe, Benjamin Mkapa wote wanawaita mapadiri ambao wamewazidi umri na nafasi, baba. Kwa hali hiyo Polycarp anaweza kumuita muumini wake Bernard inapohusu mambo ya imani yake. Na Bernard anatakiwa achangamkie. Mfumo huo haupo katika uislamu kwa hiyo hamuwezi kujilinganisha na wakatoliki. Kila muislamu anasimama yeye binafsi mbele ya muumba wake. Ndiyo maana hao wanaojiita viongozi wa waislamu hawana mandate aliyonayo Polycarp kwa wakatoliki. Mohammed Shossi anaweza kuwatolea nje bila kuhofia athari zake kiroho wakati mkatoliki hawezi kumtolea nje Polycarp bila kuwa na wasi wasi wa hatma yake kiroho. Lakini wasiwasi huu hauhusiani kabisa na shughuli zake za kidunia. Ndiyo maana Julius Nyerere aliweza kutaifisha shule na hospitali za wakatoliki bila kuogopa kuwa ataadhibiwa na wakina Rugambwa. Wakristu tunatofautisha kati cha kaizari na cha Mungu. Lakini nyie sio hivyo. Ndiyo mana kwenu nyie Umma una umuhimu zaidi kuliko serikali yako. Uko tayari kufa kwa ajili ya muislamu mwenzako aliye Afghanistan wakati kifo cha mkristu mtanzania mwenzako unaona hakikuhusu! Ndiyo maana mnaona kujiunga na O.I.C. ambako mtakuwa na waislamu wenzenu ni zaidi kuliko umoja kati yenu na wale watanzania wenzenu wasiofuata imani yenu.

Amandla.....
 
Summary:

Kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 CCM iliwaahidi waislam Mahakama ya kadhi na OIC. Waziri Benard Membe waziri wa mambo ya nje analihutubia bunge anasema "serikali imezuchunguza na imeona hakuna tataizo Tanzania kujiunga na OIC. Membe anaitwa na Polycap Membe anaambiwa njoo, Membe anaenda kwa Pengo walicho zungumza hakijulikani na alipotoka akarudi Dodoma akasema kama kuna jambo serikali halitaki kusikia basi ni OIC" Swali "msimamo wa serikali kutoitaka OIC ni wa Serikali au Pengo?".
Nimeishia kwenye Summary tu sikutaka kupoteza muda wangu..... Mytake Hawa watu ni wakuogopa kama ukoma wanajenga chuki na segregation ambazo hazima maana MAHAKAMA YA KAZI NA OIC..., HIVI NI SERIKALI NDIO INAYOAMUA HAYO AU SISI WANANCHI...., DAMN... HUKO NCHI YETU DOWANS WANAIBA HUKU SO CALLED WATANZANIA WANATUGAWA NA KUTEMBEZA CHUKI :A S angry:
 
Halafu mkuu kati ya yote uliyoandika hapo sijaona hata mmoja likimtaja kiongozi mkuu wa nchi kwa sasa ambaye ni muislamu.
Mbona membe siyo spika wa bunge kwa hizo tuhuma mlizo mpa?? Mbona wala hajawahi kua waziri wa sheria na katiba wala fedha??
Maamuzi makubwa hua yanafanywa na rais lakini kwenye tamko lenu sijaona mahali ambapo mmeonyesha kukerwa na ufanisi wake wa kazi!!
Mkuu kama wewe unaona mbali mi nakushauri achana na haya mambo pia ukiona mtu yeyote anapandikiza chuki kama hizi kemea milele.
 
...mtakuwa mnalalama kila siku tuu badala ya kuwa creative kwenye masuala yanayohusu maendeleo? maendeleo hayaletwi mdomoni wala kwa mihadhara, fanyeni kazi!
 
kinachonishangaza ni mashekhe kulishupalia kanisa kwa kipindi hiki, sijui maskini wa Mungu limewakosea nini? Mie ninavyoona kukata mzizi wa fitna basi na nyie fungueni hospitali zenu na hizo huduma nyingine za jamii ili mfaidike na hiyo migawo, ila tu mkumbuke wenzenu hata shule wameenda hivyo hata miradi yao inakuwa endelevu haiwezi kufa. Hebu fikiria kusingekuwa na Bugando, KCMC Na nyinginezo nyingi sijui nchi ingekuwaje? Ungeniambia serikali itajenga, nikuulize mbona serikali imeshindwa kujenga ndani ya hii miaka 50 tangu uhuru hizi huduma za jamii?
Kwanza wanaolalamika ni genge la watu wachache tu na wanaoishi Dar, ungetuuliza sie tunaoishi huku mikoani makanisa yanavyotusaidia hasa mahospitali
Serikali imeshindwa kuboresha tu shule za kata za secondari, itakuwa mambo yote itaweza?
hata hivyo nchi inajengwa na watu wote ikiwamo na taasisi binafsi, kwa hiyo mie nawashangaa hawa ndugu zangu kukaa na hizi chuki ambazo hazina msingi. Haf kwenye hizo huduma za jamii wakristo kwa waislam, budha, wapagani wote tunachangia kwa hiyo si kwamba wakristo wanatibiwa bure!
Kwa upande wangu naona madai ya hawa ndugu hayana mshiko kabisa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom