Yaliyojiri Club na Erickb52

Yaliyojiri Club na Erickb52

Kiuno changu kina matatizo kidogo nilitenguka juzi usiku usiniulize nilikuwa nafanya nini maana hamkawii...



Huyo mkaka alokuwa anabinua kiuno ndo Chimbuvu kama unamskia, si unajua tena wakongo kwa ndombolo na kibinda nkoi
 
Last edited by a moderator:
Halafu Erickb52 kwa kudanganya
Yule uliyeondoka nae kwenye tax tena ukafanya kumbeba na alikuwa anakuegemea begani alikuwa nani
Au kwa kuwa ndyofu zilichanganya hukujua
 
Last edited by a moderator:
Yaani ndugu yangu erickb52 mshukuru Mungu kwa kuwahi kuondoka huko club na ungechlewa kidogo ungekuwa mweupe kotekote yaelekea wewe ni mtoto wa kuja yaani club kunakupa ushamba namna hii unashangaa nini dada kubandika kope zake kwani hujawahi ona mitaani kwenu hapo?
Kweli club kuna maajabu sana na vituko vingi!
Jana nilikuwa zangu counter na DJ alikuwa vizuri sana yan bandika bandua bila kuchange beat wala kuharibu step za wateja wake! Nilistaajabu mdada mmoja alipokuja counter na mkaka kuchukua kinywaji,kope zake zilikuwa ndefu kama nusu nchi hivi nkamwangalia kwa makini nikaona zimeongezewa urefu yan zimemfanya amekuwa katuni hasaaa ila yeye alijiona katokelezea mbaya na mashauzi kibaoooo!
Then kuna binti mmoja aliletwa kupata toti mbili za godons alipokosa glass akazitwanga kavukavu hapohapo counter....nilifeel maumivu yake kooni lol wadada mko juu siku hizi.
Baadae kidogo nilimuona mkaka kajibebea juice kubwa ya Azam kwapani na mkononi kabeba Castle Lager na yuko anazunguka kila kona na anazinywa zote...sikujua flavor alokuwa anapata.
Baadae wakaingia Mmama na kasharobaro kamoja wakiwa wanaonyeshana mahaba kweli kweli lol Walikuwa wakibusiana na kukumbatiana mara kwa mara bila aibu na kuvuta hisia za watu!Kwa umri walipishana zaidi ya miaka 20 (Watu noma)
Wanaume nao hawakuwa mbali kuleta raha ya macho lol kuna mkaka alikuwa anacheza kwa style ya binua kiuno kama mdada yan alikuwa anajiachia utadhani sio ridhiki ila nilihisi ni pombe zilimkolea tu(Pombe zisizidi jamani)
Kimavazi kuna waliokuja wamevaa magauni marefu(Hawa nilihisi walokole wanaouacha ulokole taratibu au mahausigel) na wapo walokuwa wamepiga vimin haswaa na kifua nje lol mitego tupu wengine kawaida!
Kuna wanaocheza kwa step hadi raha lol huchoki kuwaangalia hata kidogo!

Kilichokuja kuniudhi nikaondoka ni mdada alipokuja na kuanza kujisogeza sogeza nilipokaa na kunigusagusa nikimuangalia anasema samahani kaka mh kila mara lol nikaona hapa hapafai tena nikaamua kuepusha msongamano nikaenda zangu kulala!

Je ni haya ndio yanayotokeaga club ?? Mbona yanastaajabisha?
Anyway mi sio mzee Mtambuzi mzee wa story

I remain
Erickb52
 
amalizie nini na wakati ameshajieleza kuwa alitoka nakwenda kulala kwani hujamuelewa wewe? acha kumdadisi mwenzio na tena usimdadisi kaka yangu hivyo weee acha nasema acha kabisa
 
my kaka erickb52 wanakuonea gele walitaka ubaki pale ili nawe ujumuike na hao hasa arushaone na watu8
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom