Yaliyojiri Bungeni: Usomaji Bajeti ya Serikali 2015/16

Yaliyojiri Bungeni: Usomaji Bajeti ya Serikali 2015/16

MKUYA: Serikali itaongeza kima cha chini cha Pensheni kwa wastaafu wa Serikali kwa mwezi kutoka TSH 50,000 hadi TSH 85,000
 
Mkuya: "Napendekeza kuongeza tozo kwenye mafuta ya Petrol na Disel kutoka shilingi 50 hadi 100 kwa lita

Yale yale, kwa hiyo hajui kuwa mafuta yakipanda ndo kila kitu kimepanda!
Ndo shida ya mawaziri wetu wa fedha ,wao wanajuaga kuongeza kodi ya mafuta, magari na vinywaji
 
inaitwa kujitegemea,kwa kuchangia maendeleo,serikali haina hela,watu ndo wenye hela
Kweli kabisa Mkuu. Hawa jamaa wanashangaza sana. Wanataka maendeleo lakini hawataki kulipa kodi
 
Zile porojo kwamba zitafungwa sasa hazipo tena.. Tuendelee kuwekeza huko mkuu

Yeah maana wameibariki kabisa kama watapata 12 bilioni kwa mwaka ina maana mhindi huwa anabeba zaidi ya 200 bilioni hivi kwa mwaka. Sisi tu ndio wazembe. Wacha ligi ianze
 
Kwa anayejua tafadhali. Hivi hiki kifaa anachotumia Bi Sada kusoma Bajeti kinaitwaje? Maana naona kashika kama kalamu vile ambayo anatumia kuscrow kwa juu. Ila ukikiangalia kwa mbali kinaonekana kama karatasi vile
Tablet mkuu yenye kalamu kama hii ya kwangu
20150611_171900.jpg
 
Yale yale, kwa hiyo hajui kuwa mafuta yakipanda ndo kila kitu kimepanda!
Ndo shida ya mawaziri wetu wa fedha ,wao wanajuaga kuongeza kodi ya mafuta, magari na vinywaji

sasa hivi nauli juu, chakula juu.
 
Yeah maana wameibariki kabisa kama watapata 12 bilioni kwa mwaka ina maana mhindi huwa anabeba zaidi ya 200 bilioni hivi kwa mwaka. Sisi tu ndio wazembe. Wacha ligi ianze
Aisee leo ndio nimejua kumbe kwa muhindi kuna pesa mingi hivi.. Nami nitaongeza mtaji wangu maradufu..
 
Mkuya: "Kuongezeka kwa tozo na ushuru katika mafuta ni kwa ajili ya umeme vijijini na mfuko wa barabara
 
Aisee leo ndio nimejua kumbe kwa muhindi kuna pesa mingi hivi.. Nami nitaongeza mtaji wangu maradufu..

Mi sikujua kama wangeiweka kama source ya kupata hela. Ila sababu wameibariki wacha sisi tuendelee kuzichanga tu. Kule kwenye jukwaa letu tujitajidi tumchape hata 100,000,000 kwa mwaka
 
Back
Top Bottom