Yaliyojiri Bungeni: Usomaji Bajeti ya Serikali 2015/16

Yaliyojiri Bungeni: Usomaji Bajeti ya Serikali 2015/16

Hapo tu umeme utapanda, japo nasikia tetesi Units zimeshaanza kupunguzwa.
Sasa sijui zitafika ngapi!

We acha tu nifah, maisha ndo yatazidi kuwa magumu sana

Ila kwa nchi yetu ambayo tunajitegemea kwa 60% tu, halafu tunapeana madaraka kwa kujuana pasipo kuzingalia uwezo wa mhusika, sishangai kuona focus ya serikali ktk kuongeza mapato inakuwa kwenye mafuta, vinywaji na magari
 
waziri wa fedha Saada mkuya salum yuko hewani hivi sasa anaendelea kuwasilisha. ameanza kwa kusema kwamba huu ni mwaka wa uchaguzi na masuala kadhaa ya mipango ya maendeleo ya nchi. endelea kufuatilia uzi huu kwa updates'

vipaumbele
1.uchaguzi mkuu
2.msukumo kwenye miradi ya maendeleo
3.mipango ya maendeleo vijijini.

kwamba serikali itaendelea kuondoa misamaha ya kodi isiyo ya lazima na itaendelea kuondoa kodi kwenye bidhaa zenye umuhimu maalum kwa wananchi ie zinazomlenga mwananchi moja kwa moja mfano kwenye pembejeo za kilimo.

hatua za kuthibiti mianya ya upotevu wa fedha
1.kupiga marufuku wakala wote wa serikali ambao hawatumii mfumo wa kielektroniki

===PAYE ITASHUKA HADI 11%
mafao kwa wazee////wataanza kulipwa baada ya kukamilisha takwimu na kuwatambua

kwenye PAYE ni changa la macho. Lazima tukumbuke PAYE inategemea kiwango cha mshahara nikimaanisha siyo fixed kama wanavyotaka kutuaminisha.
 
Waziri anamalizia kwa kusisitiza kuwa bajeti ya serikali itatekelezwa endapo tu kutakuwepo na amani na utulivu nchini ikiwa ni pamoja na kufanya uchaguzi mkuu hapo oktoba kwa amani na utulivu.

anaisema sisiem sasa!
 
Sigara na pombe mpaka sasa kimia nadhani wameona aibu kwa sababu tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu
Ni njia ya kuadaa wananchi ili wapate kura Ccm wanasima za kitoto sana
 
We acha tu nifah, maisha ndo yatazidi kuwa magumu sana

Ila kwa nchi yetu ambayo tunajitegemea kwa 60% tu, halafu tunapeana madaraka kwa kujuana pasipo kuzingalia uwezo wa mhusika, sishangai kuona focus ya serikali ktk kuongeza mapato inakuwa kwenye mafuta, vinywaji na magari

Kwakweli hali inazidi kuwa mbaya.Hivi ni kwanini wameongeza tozo katika mambo hayo?
 
nanaga tu ule uzi wa kubet naaupitia mbali,kumbe kuna hela za bure huko?
 
Habari wakuu,
Leo ni usomaji wa bajeti ya nchi kwa mwaka 2015/16 ambayo ni bajeti ya mwisho kwa kipindi cha awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, pia bajeti hii itasomwa sambamba na nchi zote zilizomo kwenye jumuiya ya Afrika mashariki kasoro nchi ya Burundi ambayo mwaka wake wa fedha ni tofauti. Sasa ni Samia Suluhu akishukuru wote waliomsaidia kufisha lengo la utengenezaji wa bajeti.
=========

Misamaha ya kodi: Serikali imekuwa ikipunguza misamaha ya ridhaa kupitia kwa waziri, sasa itapunguza kodi kwenye bidhaa muhimu kama tiba na bidhaa za mitaji na haitahitaji ridhaa ya waziri. Lengo kuu ni kupunguza mianya ya upendeleo hata rushwa kwenye misamaha ya ridhaa. Wizara ya fedha inaendelea kutangaza misamaha yote inayotolewa ili kuweka uwazi na taarifa zinapatikana katika tovuti ya wizara ya fedha.

Dhamira ya kuongeza mapato ya kodi: Kwa sasa makusanyo ya kodi ni takribani 12% ya mapato yote, utendaji wa TRA utapimwa, tutajitahidi kuziba mianya ya kukwepa kodi, matumizi ya mifumo itapunguza mianya ya kukwepa kodi na itabidi kasi ya kusambaza mifumo hii iongezwe.

Serikali haitafanya biashara na wafanyabiashara wasiotumia EFD, lazima sasa mfumo wa kielectroniki utumike kwa ajili ya malipo yote ya serikali ikiwemo faini mahakamani, viingilio mbuga za wanyama na nk na lazima maafisa maduhuli wasimamie hili. Tunaongeza kasi ya kufanya tathmini ya majengo mijini ili kupata tozo sahihi.

Itapitia upya viwango vya posho za safari katika mashirika ya umma, mikataba ya ukusanyaji kodi pia itapitiwa upya.

Kuimarisha usimamizi wa matumizi, serikali itaendelea kusimamia zabuni na utoaji wa fedha za mafungu kulingana na mapato.

Madeni ya mifuko ya hifadhi ya jamii: Serikali inayatambua na katika mwaka huu wa fedha serikali imedhamiria kulipa madeni, serikali itauza hati fungani kutambua madeni na kuimarisha hali ya fedha ya mifuko.

Sera za bajeti kwa mwaka 2014/15 zilijikita katika kukuza uchumi, kudhibiti mfumuko ya bei, kupunguza misamaha ya kodi na kujikita kuongeza mapato. Jumla ya trilioni 8.6 zilikusanywa sawa na asilimia 86 ya makadirio, tunakadiria kufikia asilimia 91 ya malengo ya jumla mpaka mwaka huu wa fedha kwisha. Mapato yasiyo ya kodi yatafikia asilimia 74.

Kwa ujumla anazungumzia bajeti inayoisha ikiwemo malengo waliyoyaweka, walipofikia hadi sasa na wanapotarajia kufika mpaka ukomo wa bajeti husika utapofika rasmi. Anasema sera za matumizi zimefikiwa ikiwemo mgao wa matumizi kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti.

Ubia kati ya serikali na sekta binafsi Miradi kadhaa ilitambuliwa ikiwemo Mabasi kasi, upanuzi bandari ya Dar es Salaam

Deni la taifa: Msisitizo umewekwa kukopa mikopo yenye masharti nafuu na deni la taifa limefikia 19.5. Ongezeko limesababishwa na uhitaji na kushuka kwa shilingi dhidi ya dola ya kimarekani. Kati ya hizo Deni la nje ni 73% na la ndani ni 26.8%.

Changamoto tulizokabiliana nazo ni mahitaji makubwa ya fedha kuboresha miundombinu, utegemezi wa mashirika ya umma ikiwemo TANESCO, TRL na mengineyo ambayo yalitakiwa yazalishe, mabadiliko ya tabia nchi, kuimarika kwa dola ya Marekani na kadhalika.

Utekelezaji wa bajeti kwa miaka mitano: Tumejenga vinu vya gesi, usambazaji umeme vijijini umeongezeka, tumeboresha miundombinu na uchukuzi, maboresho ya uchukuzi wa anga ikiwemo kuboresha viwanja na reli. Kuboresha sekta ya kilimo, kuboresha huduma za jamii ikiwemo afya, elimu kwa kuongeza mikopo elimu ya juu, kuongeza walimu shule za msingi.

Usimamizi wa uchumi, kiwango cha ongezeko kimepanda na tumefanikiwa kupunguza mfumuko wa bei pia tumeweza kuongeza ajira ikienda sambamba na ongezeko kwa pato la taifa. Uwekezaji kutoka nje umeongezeka.

Thamani ya shilingi ilipungua kwa kasi zaidi mwishoni mwa mwaka 2014, ilisababishwa na kuimarika dola ya marekani, kushuka kwa bei ya dhahabu katika siko la dola, kuongezeka kwa mahitaji ya matumizi ya dola, mauzo madogo nje, serikali inajizatiti kuimarisha thamani ya shilingi. Watu waupuke kuagiza bidhaa ambazo zinaweza kupatikana ndani pia tunaimarisha uuzaji wa bidhaa nje.

BAJETI YA MWAKA 2015/16
Huu ni mwaka wa kukamilisha mipango tuliyojiwekea na kujiwekea malengo ya miaka mitano ijayo tutajikita katika uchaguzi mkuu, umeme vijijini, maji vijijini na kukamilisha miradi ya kimkakati inayoendelea pamoja na kuwekeza kwa rasilimali watu.

Sekta ya gesi inategemea kiliingizia taifa pato miaka ijayo na ajira kwa wananchi, hata hivyo sekta hio inakabiliwa na changamoto nyingi na serikali imeandaa sera kuhakikisha kila mtanzania ananufaika na gesi kwa kuanzisha mfuko wa gesi na maandalizi ya kutunga sheria kuhakikisha usimamizi yataletwa bungeni. Sasa anaomba marekebisho wa baadhi ya sheria za kodi.

  • Kwa ufupi sijapenda vipaumbele vya misamha ya kodi kama vile pipi? sasa pipi ina tija gani kwa taifa
  • halafu yale magari ya mkataka wa kifisadi wa uda yameshushiwa kiwango cha kodi kuyaingiza.
  • ile deal ya magari ya semi trailer imenuka tena wameshusha ushuru wake, wakati uozo umejaa huko, wanaua reli kijinga jinga tuu.
  • eti vijiti vya vibiriti no ushuru wakati kiwanda chetu moshi kinakufa, are u kidding?
  • pasta na spaghetti no ushuru, deal ya yule muhindi hiyo, yaani wanahongwa tuu.
  • mabomba ya pvc no msamaha eti kuna kiwanda tayari, cha nani!!
  • nyavu hakuna ushuru, deal ya kijana wake hii.
  • hiri ri bajeti linapindishwa kuwanufaisha watu wao. wizi mtupu
 
Sigara na pombe mpaka sasa kimia nadhani wameona aibu kwa sababu tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu
Ni njia ya kuadaa wananchi ili wapate kura Ccm wanasima za kitoto sana

madhara ya sigara na pombe yamewatia aibu.
 
MKUYA: Serikali inalenga kukusanya mapato ya kodi na yasiyo ya kodi ya shilingi 13.4 trilioni sawa na asilimia 14.3 ya Pato la Taifa.
 
Ha ha ha! Wazee wa mikeka, nina wasi wasi jamaa atashusha odds.

Mkuuu hata ashushe tutamkamata tu.
Nina kamtaji ka 950,000 leo nampa huyu Spain ili kafike 1ml hivi afu tuanze kumchapa vizuri kuanzia kesho kwenye qualofication za europa
 
Back
Top Bottom