Majadiliano kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ofisi ya waziri mkuu na Tamisemi yanaendelea.
Kwa asubuhi kulikuwa na kipindi cha maswali na majibu kama kawaida, Na ilipofika Saa nne Spika Makinda aliomba udhuru na kumuachia Mkt Zungu kuendelea na kikao.
Kwa sasa Mama Sita anachangia na hoja zake amezielekeza kwa walimu na masoko ya Tumbaku hasa katika jimbo la Urambo.
Karibuni
samahani wakuu nimeingia kati ya mada hii kwa hoja ambayo imetokana na kichwa cha mada halafu imewekwa nukuu ya
PRINCE CROWN sielewi kama ni kushabihisha na mada yenyewe au kitu gani.
Swala la ELIMU tumeshalizungumzia sana humu na isitoshe ELIMU ni kuelimika sio kujua Lugha. Mtu anayejua 2+2=4 kwa kiswahili hawezi kutoa jibu tofauti akiuliza kwa kiingereza, kinachotakiwa hapo ni kujifunza lugha tu ya kiingereza hapatakuwa na haja ya kunfundisha tena 2+2. Na huwezi kuhoji ati kwa nini waziri kapitisha lugha ya Kiswahili iwe ya kufundishia wakati watoto wake wanapelekwa shule ya Kulipia?. kwani shule za kulipia ndio Kiingereza? ama tunatakiwa kusisitiza somo la lugha ya Kiingereza litumiwe shule zote!.
Watu wengi wanakosea sana na wanashindwa kutofautisha kati ya lugha ya kufundishia na somo la Kiingereza. Unaweza kufundishia lugha ya Kiswahili na ukaweka mkazo wa somo la Kiingereza kwa kila shule ili wanafunzi waijue lugha. Hivyo unapofundisha Lugha lazima utumie lugha hiyo hata iwe Kifaransa tofauti na lugha ya kufundishia masomo mengine. Leo zipo shule nyingine China, Uingereza na Canada zinafundisha lugha ya Kiswahili unafikiri kwa nini? iweje hawa wafundishe lugha yetu mashuleni kwao wakati kiswahili sio lugha ya kufundishia kwao? na wasiseme kwa nini wasitumie kiswahili kuwa lugha ya kufundishia..
Kuna watu wanasema sana juu ya China kama mfano bora, lakini wakumbuke tu kwamba nchi za magharibi wamelazimika kufanya biashara nao kwa sababu zamani nchi hizo ziliweka vikwazo kwa nchi zote za kijamaa zisinunuliwe mali zao. bado nchi kama Korea, Cuba zimewekewa vikwazo sasa unategemea vipi nchi hizo ziweze kuendelea maana UJAMAA haukatazi kuuza nje ama kununua nje isipokuwa kuwa na uwezo wa kujitosheleza (kujitegemea). Sisiw wenyewe tulikuwa waathirika wa mpango wa kuwekeana vikwazo kwa sababu za kimrengo.
Na China baada ya kufunguliwa milango wafanye biashara nje ndipo walipochukua nafasi hiyo na kufundisha Kiingereza na vipo vyuo maalum vinavyotumia lugha ya kiingereza kufundishia. Nchi nyingine za Ulaya zimeweza tenganisha shule hiz na kuziita International school lakini hakuna nchi yoyote Ulaya inatumia Kiingereza kama lugha ya kufundishia watoto wa shule za msingi kwa sababu Kiingereza sio lugha yao. Utamfundishaje mtoto somo lolote la elimu kwa lugha asoijua?
leo hii mtoto wa darasa la kwaza ukamwambie one plus one equals what? utamtupa nje kabisa ni lazima kwanza ajifunze lugha kisha ndio umfundishe kwa lugha hiyo. lakini kuna urahisi mkubwa kumfundisha mtoto - Moja kujumlisha moja ni sawa sawa na Mbili, kesho akakumbuka kuliko neno One or Two asolijua maana yake.
Kuiga kwingine jamani kuweni na pride na lugha yenu kwanza, mnaposhindwa kujiamini wenyewe mtaendelea kuwa watumwa wa fikra..