mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,310
- 6,548
Majadiliano kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ofisi ya waziri mkuu na Tamisemi yanaendelea.
Kwa asubuhi kulikuwa na kipindi cha maswali na majibu kama kawaida, Na ilipofika Saa nne Spika Makinda aliomba udhuru na kumuachia Mkt Zungu kuendelea na kikao.
Kwa sasa Mama Sita anachangia na hoja zake amezielekeza kwa walimu na masoko ya Tumbaku hasa katika jimbo la Urambo.
Karibuni
Kwa asubuhi kulikuwa na kipindi cha maswali na majibu kama kawaida, Na ilipofika Saa nne Spika Makinda aliomba udhuru na kumuachia Mkt Zungu kuendelea na kikao.
Kwa sasa Mama Sita anachangia na hoja zake amezielekeza kwa walimu na masoko ya Tumbaku hasa katika jimbo la Urambo.
Karibuni
ni hukweli usiopingika sera ya elimu nchini ni majanga na bomu linalosubiri kulipuka,haswa sera ya kutumia lugha ya kiswahili kufundishia,akichangia bajeti ya ofisi ya waziri mkuu,mapema leo asubui;
aliyekuwa waziri wa utamaduni kipindi cha mh mkapa,prof juma kapuya aliitaadharisha serikali juu ya sera ya kiswahili kutumiwa kufundishia mashuleni,kwamba ni janga ambalo litakuja kuliangamiza taifa hapo baadae,
akitoa sababu ambazo mimi niliziona zinamsingi sana kwa mstakabali wa baadae wa taifa hili,juu ya hajira,uchumi,na maendeleo,
ni kweli kabisa kiswahili ndio lugha ya taifa lakini ni vyema serikali ikawa makini na sera hambazo zitakuja kulifanya taifa liwe la watu mbumbumbu na wenye kushindwa na wageni,ni vyema serikali ikaandaa sera nzuri za helimu ili kuwaandaa watanzania na kuwapa elimu itakayo waletea tija hapo baadaye,
ni ukweli usiopingika kwamba serikali ya awamu ya kwanza kuondoa kiingereza kwenye sera ya elimu ya taifa,imeleta madhara makubwa sana kwa watanzania,na sasa inalazimika watanzania wenye uwezo kuwapeleka watoto wao kwenye shule za kulipia kutokana na kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadae ya lugha na teknolojia,
inashangaza kuona waziri au serikali wakitunga sera ya kiswahili halafu watoto wao wanawasomesha shule za kulipia! sasa hapa ni kutengeneza tabaka la watawala na watawaliwa,
hai hingii hakilini mnakataa lugha ya kingereza kufundishwa mashuleni halafu mnatunga sheria za nchi kwa lugha ya kiingereza!!!!! uhu ni uhuni kabisa yaani mnatoa fursa ya kuwafanya watanzania wazidi kuwa wajinga ili wasiwe na uhelewa wa kuzitambua haki zao kwa kutokujua tafsiri ya lugha za kigeni?
leo taifa kama china limejua hasara kama taifa lilivyopata kwa kukumbatia sera kama hizi kwa ukupiga marufuku lugha za kigeni mashuleni kwao,lakini sasa wamechukua hatua kwa kuwafundisha watu wao wajue lugha za kigeni kwa kuwa sasa taifa limepiga hatua kwenye uwekezaji na kibiashara nje ya nchi zao na wakagundua tatizo kubwa ni ukosefu wa ufahamu wa lugha.
leo ihi mtanzania wa darasa la saba au kidato cha sita aende maali na mkenya au mganda kuomba hajira mtanzania ataachwa,na mkenya na mganda wa darasa la saba kwa sababu ya lugha,
sasa serikali isijifanye mjamaa sana kwa kuwanyima watanzania haki yao ya kupata maarifa hambayo dunia nzima inajua nini maana ya lugha ya kingereza,au serikali inawaandaa watanzania kuzunguka hapa hapa nchini na sio kuwaandaa kwenda popote na kufanikiwa?
mimi katika maisha yangu nilishapiga marufuku watoto wangu kuwasomesha kwenye shule za serikali,kutokana na sera mbovu za kuwaandaa watoto vizuri kichwani,leo unamkuta mtanzania anaipenda na kuishabikia miziki ya nje lakini hajui ni nini kinaimbwa ndani ya ile miziki? ni ushetani kabisa na mimi siwalahumu watanzania hayo ni mazao ya sera mbovu za kuwanyima watanzania ufahamu wa lugha,
huku viongozi wakisomesha watoto wao kwenye shule za mapesa mengi?tuache siasa kwenye swala la helimu tusicheze na maisha ya watanzania tukiji nasibu na malugha ya ulaghai laghai ya [BRN] heti matokeo makubwa sasa mimi niseme hivi hiyo itakua ujinga mkubwa sasa
hembu tuwatendee haki hawa watanzania na tuache kucheza na maisha ya baadae ya watanzania,