Yajue mambo 10 ya kuvutia kwa Nyoka Anaconda

simba ni wa kawaida tu lazima cmba amezwe
Ni kweli, kinachomsaidia chui na duma kuwaua chatu na anaconda ni kwamba Chui anatumia akili sana na ananyambulika mwili wake, tofauti na simba anatumia nguvu nyingi tu na akili kidogo wakati chatu na wao wana nguvu nyingi pia. Chui wanavinzia na kuwapiga meno ambayo yana ncha kali sana.
 
Mbona mbuzi wa bibi alibanwa na chatu akavunjika kiuno na mguu..
[emoji2] [emoji1] lazima avunjike aisee, kuna video moja niliicheck chatu akimbana mbwa ni hatari, mbwa alitoa matapishi yenye spidi ya hatar sana
 
Nilikuwa naangalia Animal planet jamaa wanawakamata kilaiini sana ilikuwa Venezuela mto Amazon unakoanzia
 
Habari wanaJF,
Leo nataka tujuzane kuhusu Jijoka aina ya Anaconda ambalo hupatikana sana Amerika ya kusini haswa katika misitu ya Amazoni.

1- Anaconda inaweza kuwa urefu wa futi zaidi ya 30 yaani kama basi la shule na uzitowake waweza kufikia Kg 550 . Anaconda jike huwa mkubwa zaidi ya dume na katika maisha yeka nyoka huyu huendelea kukua kila umri wake unpoongezeka.

View attachment 344631

2- Kwa kawaida joka hili kwa asilimia kubwa huwa na rangi ya kijani iliyokolea sana mfano wa kijani jeshi, pia huwa na rangi nyeusi katika mgongo na pembeni anaweza kuwa na rangi ifananyo na nyeupe ingawa haitawali na kudhihirika sana.

3- Anaconda huwinda kwaajili ya chakula juu ya ardhi na pia hufanya mawindo katika maji, lakini anatumia zaidi ya maisha yake katika maji ambapo hufanya mambo yake kwa urahisi zaidi na wakati wa kuwinda hufanikisha kwa urahisi zaidi akiwa ndani ya maji.

4- Wakati akiwa kwenye maji, anatabia na uwezo wa kuzamisha mwili wake wote ndani ya maji, isipokuwa pua pekee (ambazo ziko juu ya kichwa chake), hivyo kama angekuwa anapatikana hapa nchini kwetu basi wale wanaopenda kushinda kwenye mito mikubwa walitakiwa kuwa waangalifu.

5- Anaconda anaweza kukaa chini ya maji kwa muda wa dakika 10 kabla kutoa kichwa juu ya maji ili kupata hewa na kuangalia usalama wake zaidi.

6- Mijoka hii hupendelea kula samaki, nguruwe pori, chui, na wanyama wengi wafanananao na hao. Anaconda anakula hadi Kg 40 ya chakula kwa siku.

View attachment 344632

7- Kwa bahati nzuri Anaconda si nyoka mwenye sumu kama walivyo Cobra au Koboko. Yeye anajivunia matumizi ya nguvu alizonazo katika misuli ya mwili kuua mawindo yake. Kama walivyo nyoka wengine huwa anabana hadi kuvuruga mzunguko wa hewa na damu mpaka windo anakufa.

8- Baada ya kuuwa mnyama, Anaconda anameza mzima mzima bila ya kukatakata katika vipande kwasababu hana meno ya kung'atia au kukatia.
Lakini Anaconda hufanya mawindo yake ya wanyama wakati wa usiku.

9- Anaconda hutumia miezi ya Aprili na Mei kwa ajili ya kupandishana. Na baada ya miezi sita baadaye, jike la Anaconda huzaa idadi ya watoto 20-40. Watoto huwa na urefu wa futi 2 na wao wanazaliwa na uwezo kujitegemea maisha.

Nimeweka Video kwa atakayetaka kushuhudia uzazi wa Anaconda unavyo kuwa

10- Anacondas anaweza kuishi miaka 10-12 katika pori na hadi miaka 30 kama atafugwa na mwanadamu.

Nakaribisha hoja kwaajili ya elimu zaidi.

Mkuu, kwa chakula anafaa? Maana kwa uhaba wa mboga angesaidia sana huyu.
 
Tafadhali usinipandikizie dhambi ambayo sijaifanya. Huyo uliyemtaja Wewe ndiyo utajijua nae halafu siku nyingine jaribu kuheshimu mafumbo ya wenzako. Kwani kulikuwa na ulazima gani kutaja jina la huyo Mhusika? Watu wengine mna kiherehere sana.

Nakufatiliaga sana SANA thread zako na comments si mtanzania kama mimi, ni mtu mwingine nyuma ya kibodi za simu ila wenye macho 3 tunajua.
 
hawezi salimika maana koboko yeye anagonga tu kisha anatoka speed kali sana, yn lazima anaconda afe tu
Anakonda anagamba,meno ya koboko hayapiti,na pia viumbe huogopana kulingana na species,anakonda ni kaka mkuu wa majoka,koboko ni mtukutu wa majoka
 
Habari wanaJF,
Leo nataka tujuzane kuhusu Jijoka aina ya Anaconda ambalo hupatikana sana Amerika ya kusini haswa katika misitu ya Amazoni.

1- Anaconda inaweza kuwa urefu wa futi zaidi ya 30 yaani kama basi la shule na uzitowake waweza kufikia Kg 550 . Anaconda jike huwa mkubwa zaidi ya dume na katika maisha yeka nyoka huyu huendelea kukua kila umri wake unpoongezeka.

View attachment 344631

2- Kwa kawaida joka hili kwa asilimia kubwa huwa na rangi ya kijani iliyokolea sana mfano wa kijani jeshi, pia huwa na rangi nyeusi katika mgongo na pembeni anaweza kuwa na rangi ifananyo na nyeupe ingawa haitawali na kudhihirika sana.

3- Anaconda huwinda kwaajili ya chakula juu ya ardhi na pia hufanya mawindo katika maji, lakini anatumia zaidi ya maisha yake katika maji ambapo hufanya mambo yake kwa urahisi zaidi na wakati wa kuwinda hufanikisha kwa urahisi zaidi akiwa ndani ya maji.

4- Wakati akiwa kwenye maji, anatabia na uwezo wa kuzamisha mwili wake wote ndani ya maji, isipokuwa pua pekee (ambazo ziko juu ya kichwa chake), hivyo kama angekuwa anapatikana hapa nchini kwetu basi wale wanaopenda kushinda kwenye mito mikubwa walitakiwa kuwa waangalifu.

5- Anaconda anaweza kukaa chini ya maji kwa muda wa dakika 10 kabla kutoa kichwa juu ya maji ili kupata hewa na kuangalia usalama wake zaidi.

6- Mijoka hii hupendelea kula samaki, nguruwe pori, chui, na wanyama wengi wafanananao na hao. Anaconda anakula hadi Kg 40 ya chakula kwa siku.

View attachment 344632

7- Kwa bahati nzuri Anaconda si nyoka mwenye sumu kama walivyo Cobra au Koboko. Yeye anajivunia matumizi ya nguvu alizonazo katika misuli ya mwili kuua mawindo yake. Kama walivyo nyoka wengine huwa anabana hadi kuvuruga mzunguko wa hewa na damu mpaka windo anakufa.

8- Baada ya kuuwa mnyama, Anaconda anameza mzima mzima bila ya kukatakata katika vipande kwasababu hana meno ya kung'atia au kukatia.
Lakini Anaconda hufanya mawindo yake ya wanyama wakati wa usiku.

9- Anaconda hutumia miezi ya Aprili na Mei kwa ajili ya kupandishana. Na baada ya miezi sita baadaye, jike la Anaconda huzaa idadi ya watoto 20-40. Watoto huwa na urefu wa futi 2 na wao wanazaliwa na uwezo kujitegemea maisha.

Nimeweka Video kwa atakayetaka kushuhudia uzazi wa Anaconda unavyo kuwa

10- Anacondas anaweza kuishi miaka 10-12 katika pori na hadi miaka 30 kama atafugwa na mwanadamu.

Nakaribisha hoja kwaajili ya elimu zaidi.

Hivi huyo nyoka hana madhara kwa kufanywa kitoweo?
 
Chatu yeye hujulikana kam Genus Python na Anaconda kama Genus Eunectes lakini wote wako kwenye familia moja yenye jina la kibailojia la Boidae. Mijoka hii miwili inasifa nyingi sana zinazofanana mpaka kuwachanganya wachunguzi wake lakini pia wanatofauti nyingi tu.
Ninachojua chatu ni mboga mzuri sana,ila kwa huyo anaconda sijui ebu naomba uzoefu wako mkuu
 
Anaconda anauwa aina nyingi za wanyama lakini kinyume chake na yeye anauwawa na aina nyingi za wanya na wanamla vilevile mfano Jaguar ipo video ikonyesha namna anavyomuadhibu Anaconda na kumla, pia Tembo naye anauwa vizuri tu anaconda na wengineo kikubwa ni timing tu.
Hivi huyo kiumbe jaguar ana sumu ya aina gani haswa hadi anawatesa majoka tena yenye nguvu na sumu kali?
 
Mkuu kuna kiumbe mwingne asipokasirika anakuwa mdogo lakn akikasirika anavimba anakuwa mkubwa na hupenda kuingia shimon na anatema sumu nyeupe hyo sumu ikikuingia unaanza kuvimba tumbo kwa mda wa miezi tisa vipi huyu kiumbe humwogopi?
Daaaa kweli wewe ni mgirik
 
hawa viumbe kwetu ni mboga inayoliwa na viongozi wakuu kwa ughali wake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom