Yajue mambo 10 ya kuvutia kwa Nyoka Anaconda

Yajue mambo 10 ya kuvutia kwa Nyoka Anaconda

duh anaconda na chatu wana uhusiano gani?? mwili umenisismka kwa picha ya hilo joka
 
Anaconda anaujazo mkubwa sana kulinganisha na viumbe wengi wa kwenye mito na mabwawa so Mamba alizwa kama kawaida ingawa mamba naye akimuotea anaconda basi nae anamtafuna vyema tu
Mwenyewe nimewai kushuudia anaconda tena alikua mkubwa sana akajichanga akata kuwinda mamba kumbe anapokwenda kuwinda na mamba wanamuwinda mamba walikua wawili walimtafuna anaconda kama kuku Dstv kuna chanel wanaoyesha wanyama tu kumbe ata jaguar anamtafuna anaconda basi ata simba anaweza kumtafuna anaconda
 
duh anaconda na chatu wana uhusiano gani?? mwili umenisismka kwa picha ya hilo joka
Kama niliposema hapo awali narudia Chatu yeye hujulikana kam Genus Python na Anaconda kama Genus Eunectes lakini wote wako kwenye familia moja yenye jina la kibailojia la Boidae. Mijoka hii miwili inasifa nyingi sana zinazofanana mpaka kuwachanganya wachunguzi wake lakini pia wanatofauti nyingi tu.
 
aisee
 
Habari wanaJF,
Leo nataka tujuzane kuhusu Jijoka aina ya Anaconda ambalo hupatikana sana Amerika ya kusini haswa katika misitu ya Amazoni.

1- Anaconda inaweza kuwa urefu wa futi zaidi ya 30 yaani kama basi la shule na uzitowake waweza kufikia Kg 550 . Anaconda jike huwa mkubwa zaidi ya dume na katika maisha yeka nyoka huyu huendelea kukua kila umri wake unpoongezeka.

View attachment 344631

2- Kwa kawaida joka hili kwa asilimia kubwa huwa na rangi ya kijani iliyokolea sana mfano wa kijani jeshi, pia huwa na rangi nyeusi katika mgongo na pembeni anaweza kuwa na rangi ifananyo na nyeupe ingawa haitawali na kudhihirika sana.

3- Anaconda huwinda kwaajili ya chakula juu ya ardhi na pia hufanya mawindo katika maji, lakini anatumia zaidi ya maisha yake katika maji ambapo hufanya mambo yake kwa urahisi zaidi na wakati wa kuwinda hufanikisha kwa urahisi zaidi akiwa ndani ya maji.

4- Wakati akiwa kwenye maji, anatabia na uwezo wa kuzamisha mwili wake wote ndani ya maji, isipokuwa pua pekee (ambazo ziko juu ya kichwa chake), hivyo kama angekuwa anapatikana hapa nchini kwetu basi wale wanaopenda kushinda kwenye mito mikubwa walitakiwa kuwa waangalifu.

5- Anaconda anaweza kukaa chini ya maji kwa muda wa dakika 10 kabla kutoa kichwa juu ya maji ili kupata hewa na kuangalia usalama wake zaidi.

6- Mijoka hii hupendelea kula samaki, nguruwe pori, chui, na wanyama wengi wafanananao na hao. Anaconda anakula hadi Kg 40 ya chakula kwa siku.

View attachment 344632

7- Kwa bahati nzuri Anaconda si nyoka mwenye sumu kama walivyo Cobra au Koboko. Yeye anajivunia matumizi ya nguvu alizonazo katika misuli ya mwili kuua mawindo yake. Kama walivyo nyoka wengine huwa anabana hadi kuvuruga mzunguko wa hewa na damu mpaka windo anakufa.

8- Baada ya kuuwa mnyama, Anaconda anameza mzima mzima bila ya kukatakata katika vipande kwasababu hana meno ya kung'atia au kukatia.
Lakini Anaconda hufanya mawindo yake ya wanyama wakati wa usiku.

9- Anaconda hutumia miezi ya Aprili na Mei kwa ajili ya kupandishana. Na baada ya miezi sita baadaye, jike la Anaconda huzaa idadi ya watoto 20-40. Watoto huwa na urefu wa futi 2 na wao wanazaliwa na uwezo kujitegemea maisha.

Nimeweka Video kwa atakayetaka kushuhudia uzazi wa Anaconda unavyo kuwa

10- Anacondas anaweza kuishi miaka 10-12 katika pori na hadi miaka 30 kama atafugwa na mwanadamu.

Nakaribisha hoja kwaajili ya elimu zaidi.

Mkuu lkn Sidhani kama anaconda anaweza kweli kummeza simba uyo anaconda akimuotea mamba mdogo anamtafuna sasa cha ajabu mamba mkubwa simba awafulukuti je swali la msingi anaconda anaweza kumzingua simba
 
Kama nilipojibu hapo awali, Anaconda anakula wanyama wakali wote lakini kama na yeye anabanwa basi naye hana chake. Kumbuka nimesema, Jaguar ni muhanga wa Anaconda sasa Simba kitu gani? Ila nasisitiza kama Jaguar au Simba atamuwahi Anaconda basi naye atatafunwa tu.
 
Ni kama polisi na jambazi polisi akiwahiwa anakufa vivyo hivyo kwa jambazi pia its the matter of timing
 
Chatu yeye hujulikana kam Genus Python na Anaconda kama Genus Eunectes lakini wote wako kwenye familia moja yenye jina la kibailojia la Boidae. Mijoka hii miwili inasifa nyingi sana zinazofanana mpaka kuwachanganya wachunguzi wake lakini pia wanatofauti nyingi tu.
Na mimi naona sifa za huyu Anaconda ni sawa na za chatu. Si vibaya ukatuwekea sifa chache zinazotofautisha nyoka hawa.
 
Anaconda anauwa aina nyingi za wanyama lakini kinyume chake na yeye anauwawa na aina nyingi za wanya na wanamla vilevile mfano Jaguar ipo video ikonyesha namna anavyomuadhibu Anaconda na kumla, pia Tembo naye anauwa vizuri tu anaconda na wengineo kikubwa ni timing tu.

Hapo umechemsha! Hakuna tembo mapori na misitu ya Amerika Kusini. Ukimuona tembo huko basi ni wa zoo tu nae itakuwa kaagizwa kutoka Afrika.
 
Mwenyewe nimewai kushuudia anaconda tena alikua mkubwa sana akajichanga akata kuwinda mamba kumbe anapokwenda kuwinda na mamba wanamuwinda mamba walikua wawili walimtafuna anaconda kama kuku Dstv kuna chanel wanaoyesha wanyama tu kumbe ata jaguar anamtafuna anaconda basi ata simba anaweza kumtafuna anaconda
Kwa simba sidhani maana hana uwezo wa kunyumbulika kama jaguar ambaye ni mwepesi sana. Uwepesi wake unamsaidia kumpiga meno haraka huyo Anaconda. Simba yeye anaamini kwenye manguvu zaidi ya akili hivyo siyo rahisi kumuua mnyama anayetumia nguvu na akili kwa wakati mmoja
 
Mwenye hiyo video ya anaconda na mamba aiweke hapa tafadhali
 
Anaconda anaujazo mkubwa sana kulinganisha na viumbe wengi wa kwenye mito na mabwawa so Mamba alizwa kama kawaida ingawa mamba naye akimuotea anaconda basi nae anamtafuna vyema tu
Huyo anaconda anatafuna jamii ya vimamba vya america waitwao cayman na aligator -jamii ya mamba wetu hawa wa tani moja nile croc hathubutu!
 
Je naye hushambulia binadamu?
Mkuu, tafuta ile senema ya Anaconda iliyochezwa Amazon forest na Jennifer Lopez, ice cube na Mzee Jon Voight. Utapata habri ya mjomba anaconda!
 
Huyo anaconda anatafuna jamii ya vimamba vya america waitwao cayman na aligator -jamii ya mamba wetu hawa wa tani moja nile croc hathubutu!

Kweli mkuu nimekuelewa mamba wa uku wakubwa sana aisee hawezi mamba anaemsema alimezwa na anaconda alikua mdogo sana vimamba vya kule vidogo sana
 
Back
Top Bottom