Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Habari wanaJF,
Leo nataka tujuzane kuhusu Jijoka aina ya Anaconda ambalo hupatikana sana Amerika ya kusini haswa katika misitu ya Amazoni.
1- Anaconda inaweza kuwa urefu wa futi zaidi ya 30 yaani kama basi la shule na uzitowake waweza kufikia Kg 550 . Anaconda jike huwa mkubwa zaidi ya dume na katika maisha yeka nyoka huyu huendelea kukua kila umri wake unpoongezeka.
2- Kwa kawaida joka hili kwa asilimia kubwa huwa na rangi ya kijani iliyokolea sana mfano wa kijani jeshi, pia huwa na rangi nyeusi katika mgongo na pembeni anaweza kuwa na rangi ifananyo na nyeupe ingawa haitawali na kudhihirika sana.
3- Anaconda huwinda kwaajili ya chakula juu ya ardhi na pia hufanya mawindo katika maji, lakini anatumia zaidi ya maisha yake katika maji ambapo hufanya mambo yake kwa urahisi zaidi na wakati wa kuwinda hufanikisha kwa urahisi zaidi akiwa ndani ya maji.
4- Wakati akiwa kwenye maji, anatabia na uwezo wa kuzamisha mwili wake wote ndani ya maji, isipokuwa pua pekee (ambazo ziko juu ya kichwa chake), hivyo kama angekuwa anapatikana hapa nchini kwetu basi wale wanaopenda kushinda kwenye mito mikubwa walitakiwa kuwa waangalifu.
5- Anaconda anaweza kukaa chini ya maji kwa muda wa dakika 10 kabla kutoa kichwa juu ya maji ili kupata hewa na kuangalia usalama wake zaidi.
6- Mijoka hii hupendelea kula samaki, nguruwe pori, chui, na wanyama wengi wafanananao na hao. Anaconda anakula hadi Kg 40 ya chakula kwa siku.
7- Kwa bahati nzuri Anaconda si nyoka mwenye sumu kama walivyo Cobra au Koboko. Yeye anajivunia matumizi ya nguvu alizonazo katika misuli ya mwili kuua mawindo yake. Kama walivyo nyoka wengine huwa anabana hadi kuvuruga mzunguko wa hewa na damu mpaka windo anakufa.
8- Baada ya kuuwa mnyama, Anaconda anameza mzima mzima bila ya kukatakata katika vipande kwasababu hana meno ya kung'atia au kukatia.
Lakini Anaconda hufanya mawindo yake ya wanyama wakati wa usiku.
9- Anaconda hutumia miezi ya Aprili na Mei kwa ajili ya kupandishana. Na baada ya miezi sita baadaye, jike la Anaconda huzaa idadi ya watoto 20-40. Watoto huwa na urefu wa futi 2 na wao wanazaliwa na uwezo kujitegemea maisha.
Nimeweka Video kwa atakayetaka kushuhudia uzazi wa Anaconda unavyo kuwa
10- Anacondas anaweza kuishi miaka 10-12 katika pori na hadi miaka 30 kama atafugwa na mwanadamu.
Nakaribisha hoja kwaajili ya elimu zaidi.