Yote yasemwe, lakini mijitu inaposema Magufuli ni nguvu ya soda inakera sana. Watanzania, inabidi tufike mahali tukubali kuwa tunahitaji mahali pa kuanzia. Magufuli ni mwanzo mpya. CHADEMA was the right choice kabla haijaingiliwa na majambazi. Lowassa hawezi kulingana na Magufuli hata kama hamtaki kuukubali ukweli. Lowassa ni sehemu ya uharibifu, hivyo hakuna namna angefanya marekebisho.
Halafu ni aibu kwa wachambuzi mitandaoni kutarajia rais arekebishe kila kitu within a blink of an eye! Ni miezi miwili tu tangu serikali iwepo madarakani, tayari baadhi ya watu wanajaribu kuivunja nguvu. Critic mzuri hazungumzii guess work, lazima facts ziwepo, sio kusema hii ni nguvu ya soda. Huku ni kupiga ramli.