Chapa ya mnyama unabii na pesa za kidijitali

Chapa ya mnyama unabii na pesa za kidijitali

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,116
Reaction score
2,732
Miaka ile wakati nasoma Biblia ikiwa imeandika kwamba siku hizo hutouza wala kununua kitu mpaka uwe na chapa ya mnyama nikawa nashangaa sana. How?

Tunaenda sokoni, dukani, tunanunua mahitaji yetu, sasa hii chapa ya mnyama itatumikaje? Nikaona ebu tusubiri labda ni nyakati ambazo sisi tutakuwa tumekufa.

Na kumbuka Biblia imeandika miaka hiyo Zaidi ya 1000 nyuma miaka hiyo hakuna teknolojia, hakuna umeme, hakuna lolote lile ila bado iliandikwa kwamba siku hizo hutoweza kununua wala kuuza kama hutokuwa na chapa ya mnyama. Guess what! Leo hii tumeianza safari kuelekea huko.

By now unaweza kutoka home ukaenda supermarket ukanunua mahitaji yako yote bila kushika hela mkononi. Unatumia kadi au simu. Mwezi mzima unaweza usiiguse hata elfu kumi halafu ukawa umetumia Zaidi ya laki tano. Ndipo tulipo now.

Noti hazitumiki sana wala sarafu, watu wanahamisha tu miamala. Sasa ile lama ya mnyama itapitia humuhumu. Yaani kama huna alama ya mnyama, pesa zako zinazuiliwa hutoweza kuuza wala kununua kama huna hiyo chapa ya mnyama.

Kuweka hela kwenye simu unatakiwa uwe na chapa ya mnyama, majuzi Elon musk amesema miaka ya 2040 inawezekana kabisa kusiwe na matumizi ya fedha kama karatasi, itakuwa ni mambo ya kadi na simu tu. Watu wanamsafishia njia mpinga Kristo kwani kila kitu kishaelezewa. Just imagine.

Kitu kimeandikwa miaka hiyo, kinaanza kufanyika miaka ya 2000.
 
Miaka ile wakati nasoma Biblia ikiwa imeandika kwamba siku hizo hutouza wala kununua kitu mpaka uwe na chapa ya mnyama nikawa nashangaa sana. How? Tunaenda sokoni, dukani, tunanunua mahitaji yetu, sasa hii chapa ya mnyama itatumikaje? Nikaona ebu tusubiri labda ni nyakati ambazo sisi tutakuwa tumekufa. Na kumbuka Biblia imeandika miaka hiyo Zaidi ya 1000 nyuma miaka hiyo hakuna teknolojia, hakuna umeme, hakuna lolote lile ila bado iliandikwa kwamba siku hizo hutoweza kununua wala kuuza kama hutokuwa na chapa ya mnyama. Guess what! Leo hii tumeianza safari kuelekea huko.
By now unaweza kutoka home ukaenda supermarket ukanunua mahitaji yako yote bila kushika hela mkononi. Unatumia kadi au simu. Mwezi mzima unaweza usiiguse hata elfu kumi halafu ukawa umetumia Zaidi ya laki tano. Ndipo tulipo now. Noti hazitumiki sana wala sarafu, watu wanahamisha tu miamala. Sasa ile lama ya mnyama itapitia humuhumu. Yaani kama huna alama ya mnyama, pesa zako zinazuiliwa hutoweza kuuza wala kununua kama huna hiyo chapa ya mnyama. Kuweka hela kwenye simu unatakiwa uwe na chapa ya mnyama, majuzi Elon musk amesema miaka ya 2040 inawezekana kabisa kusiwe na matumizi ya fedha kama karatasi, itakuwa ni mambo ya kadi na simu tu. Watu wanamsafishia njia mpinga Kristo kwani kila kitu kishaelezewa. Just imagine. Kitu kimeandikwa miaka hiyo, kinaanza kufanyika miaka ya 2000.
Vipi pesa za FISADI wa MAUAJI, Samia zenyewe kula siyo dhambi?
 
Yaani kama huna alama ya mnyama, pesa zako zinazuiliwa hutoweza kuuza wala kununua kama huna hiyo chapa ya mnyama. Kuweka hela kwenye simu unatakiwa uwe na chapa ya mnyama
🤔 naamini una point ya kufikisha ila ebu dadavua vyema tukuelewe.. una maana gani hapa ni chapa gani niwe nayo kuweka mpesa ama simbank?
 
Urahisi wa maisha sio suala la uchawi wala unabii, enzi za Biblia walikuwa wanatembea kwa punda, leo watu wanapanda ndege, hiyo nayo ni chapa ya mnyama?
 
Urahisi wa maisha sio suala la uchawi wala unabii, enzi za Biblia walikuwa wanatembea kwa punda, leo watu wanapanda ndege, hiyo nayo ni chapa ya mnyama?
Biblia imetoka mbinguni au imeandikwa na watu kwasababu maalum?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom