Ya Symbion na Pesa za MCC yaibuka upya kule Marekani

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,679
119,316
Wanabodi, hii nimeikuta kule fb, kama imeishaletwa humu, iunganishe kule ilipo!.

Hillary Was Scheduled To Meet Privately With Crony Lobbying Her For Africa Business
Hillary Clinton's State Department schedule includes an entry for a meeting with former Ambassador Joseph Wilson in December 2009, just a month after the…
DAILYCALLER.COM

Maria Sarungi-Tsehai
12 hrs ·
Jamani hii imeandikwa na gazeti la huko Marekani siyo sisi waafrika na ma-conspiracy theory zetu! Sasa tunaona kumbe MCC yote huku inahusiana na Clinton na Symbion. Dah! Hebu someni article yote kwanza Dan Nkurlu Evarist Chahali Lusajo Lazarus Mwaisaka Mbaraka Islam Mimi Mwanakijiji Zitto Kabwe Maxence Melo
Months after Wilson contacted Clinton about Symbion, a small, quasi-federal agency called the Millennium Challenge Corporation (MCC) granted the company $100 million in ....
See More

My Take.
Maria Sarungi-Tsehai, Sisi Tanzania tulichotaka ni umeme, bila kujali kampuni ni nani, ni ya wapi na inamilikiwa na nani!. Tangu ilipokuja nchini kwa jina la Richmond, na baadae Dowans, na kutuletea umeme kwa kutucharge capacity charge ya shilingi milioni 152 kwa siku, ilikutwa ni kampuni hewa!, Tume ya Mwakyembe ilipobaini hayo madudu, tukamtoa kafara Lowassa, tukavunja mkataba na tukahakikishiwa hakuna madhara!. Zitto Kabwe akashauri tuinunue mitambo hiyo, akagomewa!, tena tukaona bora kuwasha mitambo ya IPTL ambayo ni chakavu mara 100 kuliko Richmond, uzalishaji wa umeme kidogo, kwa gharama kubwa na uchafuzi mkubwa wa mazingira, lakini watu bungeni walijiapiza kuliko kutumia Richmond, "Over my dead body!". Tukapelekwa mahakamani, tukashindwa na kudaiwa tozo ya Dowans, watu wakasema hatulipi!. Wenye pesa zao wakainunua na kuibadili jina to Simbion. Ukweli ni kuwa ile tozo tumeilipa kimya kimya na tunaifidia kwenye bili za umeme!, Richmond ndio ile ile Dowans, na ndio hii hii Simbion. There is no any justification at all, kama tuliikataa Dowans na kuikubali Simbion!, mitambo ni ile ile, umeme ni ule ule tulioukataa, na capacity charge ni ile ile milioni 152 kwa siku na tunalipa mpaka kesho!. Watu wale wale walioilaani Richmond, na kujiapiza "over my dead body!", ndio wale wale waliokuwa waki dance na Mama Clintoni pale Siombion!. Ukweli ni kampuni hewa, na wamiliki hewa yenye usajili hewa, ila mitambo ni mitambo ya ukweli, inafua umeme wa ukweli, tunacholipia sisi ni ile mitambo na ule umeme!. .Tukiambiwa sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana, tunajifanya kushangaa!, Hata Magufuli hii kasi aliyoanza nayo ni nguvu tuu ya soda, CCM bado ni ile ile juzi, jana, leo na hata milele!.

Pasco
 
Nilipata kusoma @The Boss mahali fulani akifananisha uharaka wa kusahau walionao samaki na uharaka wa watanzania kusahau mambo.

Yawezekana ni kweli watanzania wengi ni wepesi kusahau, ila mie kumbukumbu yangu bado inanituma kuamini kwamba akili iliyotusababishia shida zetu nyingi haiwezi kuwa na majibu ya makini ya shida hizo. ..

JPM ni mvinyo mpya ndani ya kiriba cha zamani...ccm ni ile ile
 
Sijaelewa au ?? Sasa mbona Maria na Chahali walikesha kwenye mitandao hadi kumwita Lowasa ni jambazi kabla ya uchaguzi, sasa hivi wanapiga kelele za nini ilhali Lowasa alitolewa kafara kwa jambo lililokua nje ya uwezo wake ?

Kwa maana hiyo Mwakyembe na tume yake waliudanganya uma kama hizi habari ni za kweli Mwakyembe hatakiwi kuwa hata diwani achilia mbali waziri
 
Tungeepuka capacity charge ya million 152 kwa siku, tungefanya mambo mengi sana ya muhimu. Kumbuka capacity charge si simbion pekee, tunalipa capacity charge kwa IPTL, Songas, nk.
Najiuliza, kwa nini ulipe capacity charge kampuni inayofanya biashara na wewe? Otherwise kama inafanya biashara on your behalf
 
Back
Top Bottom