sundoka
JF-Expert Member
- Oct 9, 2011
- 2,067
- 2,770
Nakupa hizi cases uzisome uzielewe vizuri wewe na wenzako:Dudu baya kajipambanua kwa kuwa muwazi ila kuna wengi wanalia kama samaki machozi yanaenda na maji. Rubi na wengine wengi kutoka THT walishalalamika sana juu ya mawingu media. Unaweza ukaona bifu kati ya WCB. Jide wengine walioachwa kwenye fiesta kisa waligomea ujira mdogo. Yanayofanywa na clouds media wanayajua wasanii. Sie wasikilizaji tutege masikio na macho.
Sent using Jamii Forums mobile app
1. Hivi nikiwa natafuta mafundi wa kunijengea nyumba yangu nikakutafuta unijengee ukakataa kwa kuwa malipo yangu ni mabaya, nikatafuta mafundi wengine wakakubali kujenga kwa malipo yale yale ambayo ni mabaya kwako, kuna haja ya kulia lia kuwa mimi ni mnyonyaji nawalipa mafundi hela kidogo??
2. Ukiomba kazi CRDB ukakubaliwa ukapewa mkataba ukausoma ukasaini ukaambiwa siku ya kuja kuanza kazi. Ukaenda kumwambia dada yako mshahara uliokubaliana na CRDB kwenye mkataba. Dada yako ambae yeye anafanya kazi Standard Chartered bank na analipwa hela kubwa sana hapo StanChart, akakwambia CRDB ni wanyonyaji usikubali kufanya nao kazi. Kesho wewe ukakataa kufanya kazi CRDB ukabaki nyumbani unalia njaa hauna kazi na huyo dada yako wa StanChart hakusaidii chochote utailaumu CRDB au dada yako aliekurubuni ujinga??
3. Ukiwa wewe ni msanii akapatikana promoter mmoja akakwambia nina show 1 nataka ukapige kwa sh million 5. Alafu akatokea promoter mwingine (mfano Ruge) akakwambia mimi nina shows 10 za Fiesta ila dau langu ni milioni 3 kwa kila show. Wewe na akili yako ya biashara utachagua kupiga show wapi??
Kutoka kwenye hizo cases jifunze vitu hivi vitatu:
1. Dunia ya soko huru iko wazi kwa kila mtu. Unapokataa kufanya kazi kwa ujira mdogo ujue kuna wenzako watakubali kuifanya kwa ujira ule ule. Kitendo cha kuikataa na ukaanza kulia lia kuwaaminisha watu kwamba muajiri analipa ujira mdogo hakizuii wenzako kuendelea kujenga maisha. Usilazimishe wengine waikatae kama wewe
2. Unapopata kazi/deal yotote ya kukuingizia pesa usiwe mtu wa kuwahi kushikwa masikio na waliofanikiwa. Huyo aliyefanikiwa atakushauri hiyo kazi malipo yake ni mabaya usiifanye wakati yeye ana uhakika wa kuingiza hela. Na siku ukiiacha hatakusaidia pesa ila atakusaidia kusambaza malalamiko kwa kuwa alikushauri yeye uamuzi mbovu. Yeye wakati anakushairi hivyo ukibahatika kujua historia yake alipopitia unakuta alishawahi fanya kazi za kunyanyaswa na malipo mabaya saaana kuliko hata hayo lakini ndo zimemjenga na kumfanya a grow hadi hapo alipo.
3. Kwenye biashara lazima uwe na akili ya kukokotoa revenue. Usidanganywe na mtu mmoja anaekulipa hela nyingi kwa deal moja wakati kuna mwingine angeweza kukulipa hela pungufu ila akakupa deal 10! Mil 5 x 1 = Mil 5 lakini mil3 x 10 =mil 30! Sasa wewe kataa kufanya kazi ya mil 3 ukisubiri ya mil5 unaishia kuwaona wenzio wanakubali kufanya hiyi ya mil 3 unawekeza nguvu zako katika kuwalaumu kwamba wanakubali kunyonywa mara ooh jamaa ni mnyonyaji, n.k wakati wenzio wana make money. Ruge alikuwa anajua anachokifanya hata bei ya vitu vya jumla ni ndogo kuliko bei ya reja reja kwa kitu kitu kimoja kimoja.
All in all Ruge alikuwa na mapungufu yake kama binadamu, sio busara kumsema vibaya wakati amepumzika. Tumuombee apumzike pema lakini tusiwe watu wa kujoin upande wa walalamikaji bila kuumiza kichwa kwanza!
Amefariki sasa tutawaona hao walalamikaji wanakuwa kwenye mafanikio makubwa sasa. Ha ha haaaa
R.I.P kyoma Ruge
Sent using Jamii Forums mobile app