Ya Said Fella, Ruge na washindwa....

Ya Said Fella, Ruge na washindwa....

nilikua naangalia interview ya mwenyekiti wa saccos wa bodaboda ilala.alipokua anaeleza jinsi ruge alivyofight kuwaongoza mpaka wakapata saccos yao huko ilala hao watu wa bodaboda nikajikuta machozi yanatoka!mengi yatasemwa lakini in reality ruge ameacha alama mioyoni mwa watu!swali la kujiuliza ni kuwa siku mimi na wewe tukifa kuna mtu atakaeumia kabisa moyoni ambae sio ndugu yako wala mkeo au mumeo?ukipata jibu hapo ndo utajua kama kweli unapoishi sasa unaliishi lile kusudi la kuumbwa kwako au unaishi mradi tu siku ziende!as for ruge ameliishi kusudi lake na si wote tunaeza kuwa mashahidi but kwa wale tu waliokusudiwa
 
Chief umewahi kua kwenye industry ya muziki!?!?
Ruge is guilty as charged, wanao lalamika sio WAPUUZI.
Yes kashinda lakini kwa kunyonya wanyonge.
Na point yako ya kusema maisha yao yabadilike sasa its too late walifanyiwa ubaya walipokua kwenye peak.
Kwasasa kupitia muziki hawawezi kunufaika na vipaji vyao.
Diamond wanamchukia kwakua alikataa ujinga wao.

Acheni watu watoe ya moyoni haijalishi wana nini.

Haiwezekani msanii umzungushe Tz yote kwenye show halafu umlipe laki tano then akihoji mnafungia nyimbo zake zisipigwe kwenye vituo vyenu kisa media yenu ndio lilipo soko la wasanii hao.
Qul al haqqa walau kana murran
Lakini si mtu kasaini mwenyewe mkuu.
 
Kaharibu mambo mengi sana na kuchangia kuleta mabaya mengi. Kachuma pasipo huruma na kula pasipo kunawa, Mungu amuweke anakostahili.

Pesa aliyokuwa akitokwa na mate ili aipate kaiacha na Mungu hajamwacha afaidi, pesa haijazuia kifo na wala hatazikwa nayo, yameisha na vyote vinaishia mlangoni

Tujifunze ...pesa haitanunua uhai na siku ikifika hakuna mjanja wala pa kujificha
Kwa hiyo wewe hautakufa kwa kuwa hauna hela??

Mkuu kufa ni kufa, usifikiri amekufa kwa kuwa alipiga hela! Subiri zamu yako ifike utaelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatimaye Ruge amelala kwa amani... Siku zake za mwisho hazikuwa rahisi... Amepambania uhai wake kwa nguvu zake zote... Yatasemwa mengi... Yataandikwa mengi... Lakini hatimaye yataisha na maisha kusonga mbele.... Ni wiki ya Ruge...

Kwenye haya maisha kuna makundi mawili.. Kundi la washindi na kundi la washindwa.... Huwa tunaaswa sana kujifunza toka kundi la washindi... Ogopa sana kundi la washindwa... Hili kundi la washindwa linaweza kukuzushia chochote.. Kisha wakakijengea uhalisia na kukitangaza hasa... Mara nyingi hawakuzushii mema bali mabaya.... Kundi hili lina fikra za ajabu kweli... Yani kushindwa kwao kwenye lolote wanakuhusisha na wewe
Mbali ya Ruge na wadau wengine waliofanya mengi kwenye mziki wetu wa kisasa na hata kuibua vipaji vingi ni Said Fella (mkubwa Fella) naye huyu ni mhanga kama Ruge [emoji1019] japo kwa asilimia tofauti
Miaka ya mwanzoni mwa 2000 alileta mapinduzi makubwa kwenye bongo fleva kwa kuwa na kundi la kwanza lililofanikiwa sana la TMK-WANAUME...
Kundi hili lilitikisa mno likiwakilisha Uswazi na ndio likawa chachu ya kuanzishwa kwa makundi mengine rasmi kama East coast nk... Vibao vya TMK vilikuwa moto wa kuotea mbali... Nani hakumbuki Dar mpaka Moro?
Vinara wa kundi kina Juma nature wakiwa ndio wanasikika sana, wakafitinishwa, wakajazwa maneno... Upeo wa kufikiri ukawa mdogo... Wakaambiwa Fella anawanyonya, anawatumikisha wakati yeye si msanii kwahiyo anakula jasho lao bure
Sumu hii ikawaingia baadhi na chini ya Juma nature kundi la TMK-WANAUME likagawika vipande viwili.... Wenye kuona mbali wakabaki na Fella... Wenye kuona karibu wakaondoka na kuunda kundi lingine kwa mbwembwe nyingi na kutoa kibao cha kwanza NDEGE TUNDUNI... wimbo huu ulikuwa masimango tupu kwa Fella...
Fella hakutaka majibizano... Alifahamu wakati ni hakimu mzuri..... Leo hii Fella ni nani na yuko wapi na Juma nature ni nani na yuko wapi! Washindi dhidi ya washindwa....!!!
Makubwa Ruge aliyoyafanya kwenye muziki wa bongo fleva hayaonekani kwa baadhi yetu... Anatuhumiwa, anabezwa, anatukanwa, anakejeliwa... Anaitwa mnyonyaji na kila aina ya jina baya... Lakini ukiangalia wanaofanya hivyo ni akina nani!? Ni kundi dogo la washindwa.

Ruge sio malaika, Ruge sio mkamilifu ni binadamu kama binadamu mwingine yeyote yule ana changamoto zake ana kushinda na kushindwa kwake.. Ni mpambanaji anayehitaji naye kutoka kimaisha... Alifanikiwa kwa kiasi chake... Akapata alichopata.... Kuna wengine kati yetu tungepata nafasi yake pengine tungekuwa wabaya zaidi yake....
Washindwa wamepata pa kutolea nyongo zao.. Yani ugumu wao wa maisha na kushindwa kwingi lawama zote ni kwa Ruge... Ruge alikuwa mjasiriamali angefanyaje kulinda kazi yake? Rip brother!
Basi sasa kwa washindwa... Ruge kaondoka, yule mnyonyaji tapeli.. Aliyekuwa kashikilia funguo za maisha yenu.... Tunataka tuone tofauti sasa... Tunataka kuwaona mkitoka kimaisha sasa kwakuwa kikwazo kimeondoka!!!!

KATIKA MAISHA OGOPA SANA KUNDI LA WASHINDWA!!! ALWAYS LEARN FROM THE BEST....

Jr[emoji769]
Ni kweli time will always say

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaufahamu vizuri lkn mfumo wa capitalism ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Capitalism is just an excuse ...in same mode of capitalism artist in other parts of the world still become rich......kifupi ruge alipaswa kufanya alichomfanyia diamond kwa wasanii wengine na hta diamond alikuwa na bahati coz alikuta ruge tayari alikuwa na kashfa kibao za udhulumati kwa hyo alimtumia diamond kujisafisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We are living in a very cruel world ndugu yangu.... Its a battle of win or lose.. Survival of the fittest.... Kuna vita ya kibiashara haikwepeki popote.... Na Ili ushinde unahitaji hata mbinu chafu... Sometimes kuwakanyaga wengine migongoni mwao kama kipandio chako.. No free lunch....

Jr[emoji769]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hio kauli yako ya vita vya kibiashara imenifanya niikumbuke na vita ya kiuchumi ambayo tunaambiwa sasa hivi tupo kwenye battle field.
Kwa hio inawezekana hata mzee baba yupo sawa kwa mbinu anazotumia.

Maendeleo hayana chama
 
Kabisa,ila Sugu is clever bwana. Akaamua kuingia kwenye siasa na akawa rais wa mbeya. Ruge akashuka mwenyewe.
Ukitaka kumjua Sugu nunua kitabu chake kinaitwa Sugu Biograph from the street to the parliament, kaongea sana kuhusu industry ya Bongofleva na madhambi yake
 
My brother,

Ruge wasn't doing some charity work. He was not a Red Cross messiah or something. Alikuwa anatafuta kama wengine. Ndo kitu wengi tunaongelea humu. The story is the same kuanzia Makinikia ya Barrick mpaka machinga na kitambulisho cha JPM. Au house girl nyumbani kwako au kwangu anayelipwa 50k!!! Au mfanyakazi wa Bakhresa anayepewa laki mbili na nusu ingawa boss wake ndo richest man in the country!! Hakuna anayefanya kazi ya madhabahu. Kila mtu anataka kuchomoza. And in the process lazima wengine waumie. It is a cruel world. Kumlaumu Ruge au Masanja kwa hilo tunawakosea.

Are you aware kwamba nesi wa mshahara wa laki mbili au tatu analipa kodi.. Mbunge na mafao yake ya mamilioni au namba moja mwenyewe halipi kodi? Where's our rage? Au kwa sababu na sisi we are part of that crime pattern? Kwa sababu na sisi tukipata hizo nafasi we will do the same!

My aunt served the country for 40 years kama nesi. Amestaafu, mafao hata 20M hayakufika! Where is our rage.

Hapa sijaribu kumtetea marehemu au wengineo. Point yangu tuangalie wider social and economic dynamics za mifumo yetu.

Mwisho wa siku kwenye hizi debates tunasahau ukweli kwamba ubepari ni unyama. Unfortunately we are all in the tent. Wakati tunawanyoshea vidole wengine.... Tusisahau na sisi tunategemea mifumo hiyo hiyo kuendesha maisha yetu.

Masanja
[emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatimaye Ruge amelala kwa amani... Siku zake za mwisho hazikuwa rahisi... Amepambania uhai wake kwa nguvu zake zote... Yatasemwa mengi... Yataandikwa mengi... Lakini hatimaye yataisha na maisha kusonga mbele.... Ni wiki ya Ruge...

Kwenye haya maisha kuna makundi mawili.. Kundi la washindi na kundi la washindwa.... Huwa tunaaswa sana kujifunza toka kundi la washindi... Ogopa sana kundi la washindwa... Hili kundi la washindwa linaweza kukuzushia chochote.. Kisha wakakijengea uhalisia na kukitangaza hasa... Mara nyingi hawakuzushii mema bali mabaya.... Kundi hili lina fikra za ajabu kweli... Yani kushindwa kwao kwenye lolote wanakuhusisha na wewe
Mbali ya Ruge na wadau wengine waliofanya mengi kwenye mziki wetu wa kisasa na hata kuibua vipaji vingi ni Said Fella (mkubwa Fella) naye huyu ni mhanga kama Ruge [emoji1019] japo kwa asilimia tofauti
Miaka ya mwanzoni mwa 2000 alileta mapinduzi makubwa kwenye bongo fleva kwa kuwa na kundi la kwanza lililofanikiwa sana la TMK-WANAUME...
Kundi hili lilitikisa mno likiwakilisha Uswazi na ndio likawa chachu ya kuanzishwa kwa makundi mengine rasmi kama East coast nk... Vibao vya TMK vilikuwa moto wa kuotea mbali... Nani hakumbuki Dar mpaka Moro?
Vinara wa kundi kina Juma nature wakiwa ndio wanasikika sana, wakafitinishwa, wakajazwa maneno... Upeo wa kufikiri ukawa mdogo... Wakaambiwa Fella anawanyonya, anawatumikisha wakati yeye si msanii kwahiyo anakula jasho lao bure
Sumu hii ikawaingia baadhi na chini ya Juma nature kundi la TMK-WANAUME likagawika vipande viwili.... Wenye kuona mbali wakabaki na Fella... Wenye kuona karibu wakaondoka na kuunda kundi lingine kwa mbwembwe nyingi na kutoa kibao cha kwanza NDEGE TUNDUNI... wimbo huu ulikuwa masimango tupu kwa Fella...
Fella hakutaka majibizano... Alifahamu wakati ni hakimu mzuri..... Leo hii Fella ni nani na yuko wapi na Juma nature ni nani na yuko wapi! Washindi dhidi ya washindwa....!!!
Makubwa Ruge aliyoyafanya kwenye muziki wa bongo fleva hayaonekani kwa baadhi yetu... Anatuhumiwa, anabezwa, anatukanwa, anakejeliwa... Anaitwa mnyonyaji na kila aina ya jina baya... Lakini ukiangalia wanaofanya hivyo ni akina nani!? Ni kundi dogo la washindwa.

Ruge sio malaika, Ruge sio mkamilifu ni binadamu kama binadamu mwingine yeyote yule ana changamoto zake ana kushinda na kushindwa kwake.. Ni mpambanaji anayehitaji naye kutoka kimaisha... Alifanikiwa kwa kiasi chake... Akapata alichopata.... Kuna wengine kati yetu tungepata nafasi yake pengine tungekuwa wabaya zaidi yake....
Washindwa wamepata pa kutolea nyongo zao.. Yani ugumu wao wa maisha na kushindwa kwingi lawama zote ni kwa Ruge... Ruge alikuwa mjasiriamali angefanyaje kulinda kazi yake? Rip brother!
Basi sasa kwa washindwa... Ruge kaondoka, yule mnyonyaji tapeli.. Aliyekuwa kashikilia funguo za maisha yenu.... Tunataka tuone tofauti sasa... Tunataka kuwaona mkitoka kimaisha sasa kwakuwa kikwazo kimeondoka!!!!

KATIKA MAISHA OGOPA SANA KUNDI LA WASHINDWA!!! ALWAYS LEARN FROM THE BEST....

Jr[emoji769]
Brother, always Smart [emoji119]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wanasema aliziba ridhki zao!!sasa kaondoka mziba ridhki na tuone km watatoboa sasa maana wasanii wetu wanakula hadi unga ukiuliza saaaana watakuambia chanzo ni ruge na CMG
 
Hujaielewa meseji yangu, kufa si tatizo
[QUOTEnisundoka, post: 30583057, member: 56685"]Kwa hiyo wewe hautakufa kwa kuwa hauna hela??

Mkuu kufa ni kufa, usifikiri amekufa kwa kuwa alipiga hela! Subiri zamu yako ifike utaelewa

Sent using Jamii Forums mobile app[/QUOTE]

Hujaielewa meseji yangu, alafu kumbuka tatizo siyo kufa tatizo ni unakufaje na unaacha nini? Siyo lazima uwe na pesa lakini legacy yako inasomekaje! Passed like A Shadow?

Tuishi maisha ya utukufu na tumuogope Mungu, mie najiandaa kwa hilo
 
Dudu baya kajipambanua kwa kuwa muwazi ila kuna wengi wanalia kama samaki machozi yanaenda na maji. Rubi na wengine wengi kutoka THT walishalalamika sana juu ya mawingu media. Unaweza ukaona bifu kati ya WCB. Jide wengine walioachwa kwenye fiesta kisa waligomea ujira mdogo. Yanayofanywa na clouds media wanayajua wasanii. Sie wasikilizaji tutege masikio na macho.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakika mkuu....

Kuna watu humu wamesema eti wataona kama kifo cha ruge kitawafanya wasanii kuendelea ..maana wanamtupia lawama kama alishikilia funguo za mafanikio yao?

Hivi anawaza kweli?

Kajumlisha vitu viwili tofauti!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We are living in a very cruel world ndugu yangu.... Its a battle of win or lose.. Survival of the fittest.... Kuna vita ya kibiashara haikwepeki popote.... Na Ili ushinde unahitaji hata mbinu chafu... Sometimes kuwakanyaga wengine migongoni mwao kama kipandio chako.. No free lunch....

Jr[emoji769]
Karma....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom