Kama vile mbegu iendapo ardhini kwa kuupoteza uhai wake ndivyo huchipua uhai ule ule katika mbegu nyingi. Watu hawa waliouawa Arusha na huyu rpc a.k.a malyamungu kwa kutetea haki yao ya kikatiba, hawakuenda bure. Damu yao imekuwa chachu iliyoziwasha nia na ari mpya ya sisi wananchi kudai haki zetu za msingi na fursa ya kuthaminiwa ubinadamu wetu katika taifa letu wenyewe. Hatutalala wala sasa hatutapumzika na tutatumia fursa yoyote itakayopatikana hata tumehakikisha huyu kaburu mweusi ndani ya nchi yetu anatokomezwa. Ni heri sisi sote tufe maana huo utayayari tumekwisha kuuva sasa, ili watoto wetu na kizazi kijacho kiwe salama.
Wana mageuzi wa kweli naomba sasa maneno yetu yawe mafupi bali matendo yetu ndiyo yazungumze zaidi.
.
EEH MUNGU ZILAZE ROHO ZA WAHANGA HAWA MAHALA PEMA PEPONI. NA WALE WOTE WALIOHUSIKA NA VIFO HIVI WATIWE ALAMA ILI WAWE WAZI KWA MALIPIZO, WASIACHWE WASHUKE KUZIMUNI KWA AMANI MAANA HAWAKUITAKA HIYO AMANI!
.