Ya Polisi na vyama vya siasa Tanzania

Ya Polisi na vyama vya siasa Tanzania

Mungu awalaze mahali pema walifariki katika vurugu hizi!
 
Kwani viongozi wa CDM walipokuwa wanawaamrisha wafuasi wao haya hawakutegemea ? wao ndio wabebe lawama kwa waliyo tokea kwa kutafuta umaarufu usio na tija. Huwezi shindana na dola, na hii imeonyesha kuwa dola ipo na inafanya kazi, next time watatia akili kichwani

The extent of human stupidity truly baffles me!
 
JK mikono yako imetapakaa damu za watz wasiokuwa na hatia.Damu yao inakulilia popote utakapokwenda. UMEHARIBU SANA CV YAKO NA UTAENDELEA KUJICHAFUA MPAKA MWILI WAKO WOTE UTATAPAKAA DAMU, USIJE SEMA HATUKUKUONYA, ACHANA NA MAFISADI SIKIA KILIO CHA MAMILIONI YA WATANZANIA
 
Labda walipeleka hospitali nyingine hizo maiti au mortuary iko moja tu???????isije ikawa watu wanadanganya kuhusu watu kufa na hapa tunataka tuchangie waliofiwa na kujeruhiwa???????
 
Labda walipeleka hospitali nyingine hizo maiti au mortuary iko moja tu???????isije ikawa watu wanadanganya kuhusu watu kufa na hapa tunataka tuchangie waliofiwa na kujeruhiwa???????

Kina mortuary moja tu Arusha.
We have to be very serious sababu kutakuwa na sources nyingi sana za habari hambazo hazijachujwa
 
Waliandamana CUF mkawabeza. WAHUNI WALE WAVAA BUIBUI NA VIBALAGHASHIA. waliuawa watu wengi kule pemba mkazidi kubeza. Leo mnasema CUF ni CCM-B. Mlisahau historia ya mapambano na DIRA ya siasa na uzalendo wa kitaifa. Aliwahi kuvunjwa mkono Profesa wa UCHUMI mkabeza eti Profesa uchwara. SASA ONJENI SHUBIRI HIYO NA MJUE SERIKALI IPO. NGOMA IKILIA SANA MWISHOWE HUPASUKA.
Sifurahii ila nakumbushia!! viva Dr. Slaa dr wa ukweli

contradicting ideas
 
Mauji yapo wanaficha lakini hukumu hii haitamuepuka Meya feki wa Arusha - Bwana G. Lyimo labda atubu mapema.........Mungu atashulika naye kwani ameingizwa madarakani ki-batili naye akakubaki ubatili.
 
rest in peace fighters, they will kill us but they will never stop us...............
 
Duh, sasa itabidi niamini huu ni uzushi au hao wamiliki wamenyimwa wasiseme ukweli??huwezi jua dola hii bwana!
 
Aisee nimesikia bbc network Africa ya saa tatu usiku kuwa watu zaidi ya 10 wameuawa kwa risasi za moto.

Mwenye habari zaidi atupe wana JF

Kwa ndugu wa marehemu hawa najua wapo kwenye wakati mgumu wa kuondokewa na muwapendao.

But this is just a beggining of new chapter in Tanzania.
i know they blood will nourish the tree that will bear the fruits of freedom and begning of new free and democratic Tanzania

Rest in peace
 
10 wahofiwa kuuawa kwenye ghasia mjini Arusha.




Watu wasiopungua kumi wameripotiwa kuuwawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mji wa Arusha Tanzania, kwenye makabiliano baina ya Polisi na wafuasi wa chama cha upinzani cha CHADEMA.Ghasia zilianza baada ya Polisi kumkamata mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho Freeman Mbowe na mbunge wa Arusha mjini Godbless Jonathan Lema, wakiwa wanaelekea kuhutubia mkutano wa kisiasa.
Baadaye polisi pia walimkamata aliyekuwa mgombea wa chama hicho cha CHADEMA kwenye uchaguzi wa Urais uliofanyika mwezi Oktoba Dr Wilbroad Slaa.

Taarifa zinasema biashara kadhaa zilichomwa moto kwenye vurugu hizo.Kwa mujibu wa waandishi wa habari mjini Arusha, Polisi walikuwa wamewakataza viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao kufanya maandamanao kabla ya mkutano wa kisiasa wa Jumatano, lakini mamia ya wafuasi wa chama hicho wakawafuata viongozi hao walipokuwa wanaelekea eneo la mkutano.Bwana Slaa amenukuliwa akisema maandamano hayo yalikuwa ya kupinga ufisadi katika serikali mpya ya Rais Jakaya Kikwete.Polisi walifyatua risasi hewani mara kadhaa kutoa tahadhari kwa maelfu ya wafuasi waliokwenda kutaka viongozi wao waachiwe huru, na baadaye wakafyatua gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya.

Walioshuhudia wanasema Polisi waliendelea kufyatua risasi mchana kutwa, huku wafuasi wa CHADEMA wakiendelea kukabiliana na askari Polisi katika maeneo mbali mbali ya mji wa Arusha.Kwenye mkutano huo wa kisiasa, Dr Slaa aliwataka Polisi kumwachilia huru Bwana Mbowe na wengine, na pia akamtaka Rais Kikwete kujiuzulu.Hadi kufikia Jumatano jioni hakuna taarifa iliyokuwa imetolewa na serikali kuhusu mzozo huo.Kumekuwa na mvutano wa kisiasa nchini Tanzania tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Urais ambao vyama vya upinzani vinadai ulikuwa na udanganyifu.Kufuatia uchaguzi huo shinikizo zinaendelea za kutaka Tanzania iwe na katiba mpya tofauti na iliyopo sasa, ambayo hairuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais kupingwa mahakamani yanapotangazwa na tume ya uchaguzi.

Source: BBC
 
Hapa ndio nakumbuka usemi wa kaka yangu acid

"I am no psychologist but surely misplaced optimism can lead to a state of delusion"
 
Polisi walitumia nguvu kubwa sana ambayo pia nao inawa cost. KWeli watu zaidi ya 7 wamekufa. Jana usiku polisi mmoja alikuwa anaelekea nyumbani kwake maeneo ya unga limited ghafla alivamiwa na vijana wakidai kulipiza kisasi kwa wenzao walio uwawa na polisi. Polisi kapigwa hadi kufa. Sasa hii nihatari kwa mapolisi kutembea na jezi zao mtaani baada ya kazi. Sasa watalazimika kwenda na nguo za nyumbani kazini.
Ila hii fujo yote kwa jinsi nilivyo tizama kwa macho yangu, driver wa Hon. Mbowe ndio alisababisha hii fujo yote msafara ulivyo fika kwa Dr Mohamed karibu na ofisi za takukuru polisi walitaka kuongoza msafara driver akawa anazuia. hapo ndio mkongoto ukaanza. Hon Lema alikimbilia restaurant ya jirani, Hon Mbowe kaagukia mtaroni. Driver wa Mbowe kweli sijui kama yuko hai, jamaa alipigwa sana kuliko mwizi alieiba kuku. Hon Lema walimsakama alivyo jitokeza tu alipigwa mabuti ya ukweli hadi akasahau jina lake! Ila polisi kwakweli wameuwa sana, walio vyunjwa migu kwa risasi wengi zaidi.

Mbona unanitisha! Ni kweli uyasemayo! Kwamba Polisi wameuwa watu wengi? Kwamba Polisi wamevunjwa watu miguu! TANZANIA BECOMING A POLICE/MILITARY STATE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! GOD FORBID
 
Polisi wanatimiza wajibu kutokana na order za wakubwa wao.Hawa wakiadhibiwa tunawaonea. Kama sheria itachukua mkondo wake iwe ni kwa mabosi wao wanaotoa hizo order.
Aibu!!!
Tena uishie hapo hapo. Kutimiza wajibu wa kuua ama kutuliza ghasia? KWanza nani mwanzilishi wa hizo ghasia kama si hao polisi! Mbaya zaidi hao wanaoandamana wanatetea na maslahi ya hao w.a.s.e.n.g.e (polisi)
 
Hii inabadilisha historia ya Tanzania sasa! Na hali itaendelea kuwa mbaya zaidi inapaswa kesho Watanzania wote waandamane kwa kulaani mauaji ya Watanzania wasiokuwa na hatia yaliyotokea leo.

Hatufurahii mauaji ya ndugu zetu na tunapinga sana na kulaani mauaji hayo,lkn kwa chadema tu ndo yafanyike hayo maandamano ya kulaani? walivouawa wana cuf mulisema chama cha vurugu sio nyie leo je?.. ndo waswahili wanasema usimcheke mamba wakati mto hujavuka..
Tunakuomba ewe MUNGU wetu waondoshe hawa ccm ktk dunia hii..
 
Naamini sas mapambano rasmi ya kuung'a utawala dhalimu wa kimabavu yameanza..ndugu zetu wana CDM Arusha tuko pamoja, tunajipongeza kwa ushindi dhidi ya dhuluma za waziwazi. Mungu awajalie nafuu haraka. JK na madhalimu wenzie wasidhani nguvu ya umma wanaweza kuizuia kirahisi asilani, tena maandamano ya nchi nzima ndio yaanze maandalizi haraka... We Shall Overcome some days, I do believe!!
 
Back
Top Bottom