Ya Polisi na vyama vya siasa Tanzania

Ya Polisi na vyama vya siasa Tanzania

ONLY FOUR-The Rest mentioned im not sure if they are real people.
 
Polisi ndio wanaoanzisha vurugu kama watu waliandamana bila kufanya vurugu hadi polisi walipoingilia maandamano na kuanza kurusha mabomu na risasi za moto ndipo vurugu zikaanza kwanini polisi wasiwajibike? Tanzania maandamano yote huwa yanafanyika kwa amani isipokuwa tu polisi wanapoingilia kwa kupiga mabomu. Waacheni watu waandamane bila bughudha yoyote hata kama watandamana kilometa 1000 katiba ya nchi inaruhusu na hawa polisi kutabiri mambo kama sheikh Yahaya waache, kila mara wanakuja na habari za kiintelenjisia ooh kutakuwa na vurugu kama wataruhusu maandamano wakati wao ndio wanaoanzisha vurugu. Mimi naamini kabisa bila kushabikia upande wowote watu wakiruhusiwa kuandamana bila kuingiliwa na polisi hakuna vurugu itakayotokea.
 
Hii ndio tatizo la kuwa na police wanaofanya kazi zao kisiasa. Hivi kama wanasema "taarifa za kiinteligensia zimebaini kutakuwa na fujo wakati wa maandamano," sasa wao ndo wamefanya nini?? Mbona wanafanya mauaji? Si wangetumia taarifa hizo kuwadhibiti na si kupiga marufuku maamdamano.

Mbona maandamano ya kupokea na kuunga kauli za viongozi wakuu hayapati msuguano? Hii ni aibu kwa Kikwete na serikali yake nani aibu kwa Taifa letu.
 
Inasikitisha sana tunapojinadi kuwa Tanzania ni nchi ya amani. Kwa yaliyotokea Arusha jana maana nilikuwepo naona kabisa nchi yetu ikiingia shimoni.
Tukumbuke kuwa hata ivory coast nao walikuwa kisiwa cha amani kama tunavyojinasibu na wametumbukia kwenye machafuko.
 
Igp mwema,kamanda andengenye,kikwete,wakuu wa usalama wa taifa arusha n.k ocampo lazima awachukue the hague no way out tumechoka angalieni wenzenu wa kenya
 
Sikubaliani kabisa na kipigo walichokipata hawa chademan huko Arusha, ingawa ni vizuri sana watu wote waliosherehekea mauaji ya mwembe chai, na wale ambao hufurahia kuiona CUF wakila virungu, sasa na wao wameionja joto ya jiwe. Swali langu jee, kwanini Arusha wakati serikali ipo Dar? Kukimbilia Arusha kuna ishara ya vitu viwili.

1. Huko ndiko kwenye wafurukutwa wa chadema.

2. Woga wa chadema kwa kudhania kwamba mkono wa serikali utawagusa tuu wakiwa dar, na Arusha ni mbali na serikali kuu na hivyo basi watakuwa salama. (wahindi wanasema "...onea buji, gombe ogopa eeh.....!")

Hongera serikali yetu tuliyoichagua kwa kuwaonya wahuni ambao wakataka kuijaribu serikali na wamekutana nayo.

Safi sana....................
 
habari za kuaminika huwa zina chanzo na uthibitisho! kwa mfano majina ya waliokufa na sehemu wanazoishi!

Basi kama uamini idadi hiyo ya walikufa,basi amini kuna watu wamekupa,ni wangapi na walikuwa wanakaa wapi hiyo utajua tuu!!
 
Igp mwema,kamanda andengenye,kikwete,wakuu wa usalama wa taifa arusha n.k ocampo lazima awachukue the hague no way out tumechoka angalieni wenzenu wa kenya

Mkuu unadhani ocampo akija kwa hili unadhani Slaa atatokea mlango gani?
 
Jaribu kuamini ninachokuambia coz nipo Arusha City Centre
mkuu hata sisi tuko Arusha hebu tumia maneno machache kutuelewesha umezipata wapi maana yanasemwa mengi sana kwa sasa kuhusiana na tukio zima....hivyo utakuwa umeijengea JF title pia maana mpaka sasa hakuna chombo chochote tanzania ambacho kimesubutu kusema hayo kama kipo mimi sijakisikia..
 
Haya, dunia nzima sasa inajua Tanzania si kisima cha amani tena...

Tanzanian police kill two rioters, seize opposition chiefs

Thu Jan 6, 2011

By Fumbuka Ng'wanakilala

DAR ES SALAAM (Reuters) - Police have shot dead two anti-government protesters in Tanzania and arrested at least 10 leading opposition figures during a violent demonstration, a senior police official said on Thursday.

Riot police fired at crowds of opposition supporters in the northern town of Arusha on Wednesday after the authorities banned their rally.

Opposition leader Willibrod Slaa, who ran in last year's disputed presidential election, was among those detained. His Chadema party spoke of a deliberate crackdown on the opposition.

"Two people died ... after being shot by the police while trying to forcefully invade a police station to free their colleagues who were arrested by the police," Arusha Regional Police Commander Thobias Andengenye told Reuters.

Police arrested 49 people in total, including Chadema's chairman, Freeman Mbowe, and at least four opposition lawmakers.

Opposition leaders have cried foul over the election of a ruling party candidate to mayor of Arusha, an opposition stronghold, saying Chadema councillors who are equal in numbers to councillors from the ruling CCM party were barred from voting.

The arrest of Slaa, the main challenger to President Jakaya Kikwete in an October 31 presidential election marred by a record low turnout and allegations of vote rigging, came days after he called for Kikwete's resignation.

He demanded Kikwete step down following a scandal over a power generation contract amid chronic energy shortages in east Africa's second largest economy.

"There is a deliberate crackdown on opposition leaders. The president has publicly declared that his government will not tolerate demonstrations of any kind," Chadema's acting secretary-general, John Mnyika, told Reuters.
 
Sikubaliani kabisa na kipigo walichokipata hawa chademan huko Arusha, ingawa ni vizuri sana watu wote waliosherehekea mauaji ya mwembe chai, na wale ambao hufurahia kuiona CUF wakila virungu, sasa na wao wameionja joto ya jiwe. Swali langu jee, kwanini Arusha wakati serikali ipo Dar? Kukimbilia Arusha kuna ishara ya vitu viwili.

1. Huko ndiko kwenye wafurukutwa wa chadema.

2. Woga wa chadema kwa kudhania kwamba mkono wa serikali utawagusa tuu wakiwa dar, na Arusha ni mbali na serikali kuu na hivyo basi watakuwa salama. (wahindi wanasema "...onea buji, gombe ogopa eeh.....!")

Hongera serikali yetu tuliyoichagua kwa kuwaonya wahuni ambao wakataka kuijaribu serikali na wamekutana nayo.

Safi sana....................

Nadhani si busara kufurahikia vifo vya watanzania wenzetu (kwani kuna mtu baba yake au mama yake au ndugu yake amefariki) hivyo basi anapofariki sio msiba wa kuondokewa na mtu bali pia kuna mtu watu wanamtegemea na hivyo basi ni msiba pia wa kimaisha. Mie sikubaliani na hilo na Chadema kama wanavyosema CUF kuwa watu wa vurugu na wao pia wanapaswa kulaaniwa kwa kuwadumbukiza wananchi katika vurugu zisizo za lazima. Vile vile polisi wwasingelitakiwa kutumia nguvu bali ni ustaarabu na hekima na busara zingelitumika kucontain hayo maandamano.
 
mkuu hata sisi tuko Arusha hebu tumia maneno machache kutuelewesha umezipata wapi maana yanasemwa mengi sana kwa sasa kuhusiana na tukio zima....hivyo utakuwa umeijengea JF title pia maana mpaka sasa hakuna chombo chochote tanzania ambacho kimesubutu kusema hayo kama kipo mimi sijakisikia..

Askari wa kwanza alikuwa tu mtaani na sare zake akavamiwa, wa pili alijichanganya na raia akashtukiwa, raia wawili walikuwa wanakimnbia wakaanguka vibaya wengine walipigwa risasi

majeruhi wengi wa vurugu wapo Hosp ya Mount Meru nenda utapata full data
 
hivi unafikiri wanajua kitu hawa wacheza kiduku?
 
Back
Top Bottom