Ya Polisi na vyama vya siasa Tanzania

Ya Polisi na vyama vya siasa Tanzania

POLISI mkoani Arusha, jana lilimwaga damu za watu kadhaa, walioshiriki na wasioshiriki maandamano yaliyoandaliwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).Risasi za moto na mabomu ya machozi vilitumika katika jitihada za polisi kuzima maandamano ya Chadema, wakitekeleza amri ya Mkuu wa Jeshi hilo, Ispekta Jenerali Saidi Mwema.IGP Mwema alitangaza kuyapiga marufuku maandamano ya Chadema akibainisha kwamba taarifa za kiintelijensia zimebaini kwamba kungekuwa na vurugu wakati wa kufanyika kwake.
“Maandamano hayo ni marufuku, lakini wanaruhusiwa kufanya mkutano wao wa hadhara. Kuna taarifa za kiintelijensia kwamba kunaweza kutokea fujo na uvunjifu wa amani,” alisema IGP Mwema alipozungumza na waandishi wa habari juzi jioni.Awali Chadema iliruhusiwa kufanya maandamano hayo yaliyoandaliwa kushinikiza taratibu zifuatwe katika uchaguzi wa wenyeviti au mameya wa halmashauri nchini.Maandamano hayo pia yalilenga kuwahamasisha wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani kushiriki kutoa maoni yao bila woga juu ya kuandikwa upya katiba ya nchi, pindi kamati itakapoanza kazi.

Maandamano hayo yalipangwa kuwashirikisha wabunge wote wa Chadema, na yalipangwa kuanza jana saa 4:00 asubuhi na kuishia kwenye viwanja vya NMB mjini Arusha ambako mkutano wa hadhara ungefanyika.Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Thobias Andengeye juzi aliruhusu maandamano hayo lakini akasisitiza kwamba jeshi lake litatoa ulinzi ili kuhakikisha yanakuwa ya amani.“Tumekubali maandamano na mkutano wa Chadema lakini tunaomba wafuate taratibu na wahakikishe hakuna uvunjifu wa amani ambao unaweza kutokea,” alisema Andengenye.

Hata hivyo baadaye juzi jioni IGP Mwema, aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kutangaza kuyafuta.
IGP Mwema aliwaeleza waandishi wa habari kuwa ameamua kufuta kibali cha maandamano hayo kutoka na kupata taarifa za kiintelijensia kwamba “kungetokea vurugu”.Agizo hilo Jipya la IGP Mwema lilifanya viongozi wa chama hicho kilichojizolea umaarufu, hasa baada ya kuanzisha hoja ya Katiba, kukaidi na kusisitiza kuwa maandamano hayo yangefanya jana kama ilivyopangwa.Na walipojaribu kufanya maandamano hayo polisi ilianza kutumia risasi za moto na mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji hao uamuzi ambao ulifanya watu kadhaa wakiwamo wabunge wa Chadema kujeruhiwa vibaya.Hadi jana jioni zaidi ya watu kumi, akiwepo mke wa Dk Slaa, Josephine Mushumbusi, walijeruhiwa kwa kipigo huku watu wengine watatu, wakiwa wako hoi baada ya kupigwa risasi za moto.

Wakati watu hao wakiumizwa kwa vipigo, mali kadhaa ikiwamo gari la mbunge wa viti maalum mjini moshi, Grace Kiwelu viliharibiwa.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe pia alikumbwa na dhoruba pale alipojikuta akitumbukia kwenye mtaro wa maji machafu na polisi kumshabulia, wakati alipokuwa akishiriki maandamano pamoja na wabunge kadhaa wa Chadema.Wakati hayo yakiendelea, shughuli zote katika mji wa Arusha zilisimamia huku barabara kadhaa nazo zikifungwa tangu asubuhi kutokana na vurugu za polisi na kamatakama ya watu iliyokuwa ikiendeshwa na jeshi hilo.Vurugu za polisi pia zilifika katika makazi ya watu na katika hospitali ya wilaya ya Arusha ya Kaloleni ambako, wagonjwa kadhaa walizimia kutokana na polisi kurusha mabomu ya machozi jirani na hospitali hiyo.Daktari za zamu wa hospiali hiyo, Anna Kimaro alielezea kushangazwa na hatua ya polisi kurusha ovyo mabomu ya machozi jirani na hospitali.Baadhi ya wagonjwa, Mwanaidi Mussa na Sabra Khalfani, walisema wamedhurika na hali hiyo kwani walipatwa na mshtuko.“Mwanangu alipoteza fahamu kabisa hadi sasa hajisikii vizuri,” alisema Sabra alipozungumza na Mwananchi hosipitalini hapo, huku akiwa amebeba mtoto wake Abdul Yusuph, mwenye umri chini ya mwaka mmoja.

Katika vurugu hizo, pia baadhi ya waandishi wahabari walijeruhiwa kwa kupigwa na polisi akiwepo mwandishi wa gazeti hili, Moses Mashala,mpiga picha wa kituo cha televisheni cha Channel ten, Ashraf Bakari, mwandishi wa kujitegemea wa BBC, Moses Kilinga na wengine kadhaa.Kamanda Andengenye hakupatikana jana kuelezea idadi kamili ya majeruhi kwani polisi, waliwazuia wanahabari kufika kituo kikuu cha polisi huku wakiwataka kuondoka eneo la kituo hicho katika muda dakika tano.

Source: Mwananchi
 
Hakuna chombo cha habari kilichoripoti kufa kwa mtu yeyote zaidi ya bbc swahili. Kama kweli watu 10 wamekufa, hizi habari zingekuwa kila kona ya dunia, but nimechungulia kila mahali hakuna. Hata magazeti ya ndani hayajaripoti kufa kwa mtu yeyote. Daily Nation ya kenya imeripoti maandamano tu. Mwananchi na Citizen hawajasema kama kuna mtu amekufa. So nadhani kuna haja ya kuwa na udhibitisho wa kweli kabla hatujaanza kutoa pole etc kwa msiba ambao huenda haupo
Vyombo vya habari huwa zinasubiri polisi watoe habari za vifo. Sasa waliohusika ni polisi na hakuna hata mmoja aliyekuwa tayari kutoa tamko kuanzia kwa Andengenye mwenyewe! sasa inabidi uwe na vyombo vyenye thubutu ziweze kutoa taarifa jinsi ilivyo bila kuchakachua. inabidi kama habari za bbc si za kweli basi polisi wakanushe! mara nyingi unaposhindwa kupata habari ya upande mwingine inabidi utoe taarifa uliyonayo ili kama ina kasoro ule upande mwingine utakanusha au utatoa marekebisho n.k.
 
Those bull shit's - Mwema's dogs !!!!! I think one dog has been killed yesterday if I'm not mistaken !!!! So so sorry for innocent civilians who dies due to those cockroach knows nothing about democracy..
 


ni kweli kabisa, maana unavyoshabikia kama vita vikianza wewe na familia yako hamtakuwepo...
Nomba Mungu hata familia yako itakapouawa yote na mimi hapa nitaandika GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOD

watu kama nyie mie nikipata data zenu vita vikianza mimi nakimbilia kwa familia yako kuimaliza tu ili ushabikie vizuri....
watchn you
 
Nalaaani kitendo hiki cha matumizi ya nguvu na Mauaji yasio ya lazima.........Mungu aziweke Mahali pema peponi Roho za ndugu zetu waliokufa tutawakumbuka Daima kama mashujaa waliofia vitani katika Ukombozi wa Nchi Yetu
 
Waliopoteza roho zao ni wale waliokwenda kuvamia kituo cha Polisi kulazimisha viongozi wao waachiliwe ndipo polisi walipojaribu kuwazuia na waandamanaji kuuwa Polisi 3 na hapo ndipo nao wakauwa! na ndipo wafuasi wa CDM wakasambaa mjini kupora na kuchoma moto majumba na maduka!! sasa kama waandamanaji hawakuwa na nia ya machafuko kwanini waue askari na kuchoma magari moto?

kwahiyo ni sawa Askari kuwaua raia??? ficha upumbavu wako, yale mabomu yalikuwa yanachagua waandamaji watalii au raia mwema??
hata wewe mwanao angeweza akawa anarudi shule akakutana na fujo hizo hata kuuwawa, tunawasubiri Vita vya Tanzania vitakuwa vya historia kwani tunawajua wabaya nani na tumetumia muda mwingi kuvumilia na kuwasoma...
wakimbizi wakwanza watakuwa hao mafisadi Papa na familia zao.... Tutatumia tekniki aliyotumia Mungu kumlazimisha farao awaachie wana wa Israeli tutaanza na watoto wao wazaliwa wa kwanza......
 
Saidi mwema ni mpuuzi, majambazi wanatusumbua kimara, mbezi beach, tegeta anaacha kufanya intelejesia yake anakuja kufanya kwenye maandamano, kumbe ndio maana mahita alikuwa anamdhibiti hili jamaa
 
Nisaidieni jambo moja. Polisi wetu wanatumia kifungu gani cha sheria kuzuia au kuruhusu MAANDAMANO/MIKUTANO? Kifungu hicho( kama kipo) hakikinzani na KATIBA yetu mbovu ya JMT? Sote tunajua mahakama zetu zitakachoamua juu ya sakata hili. Hakuna namna ya kumfikishia Ocampo suala hili?
 
Habari wana Jf habari za kuaminika ni kwamba mpk sasa jumla ya watu sita (askari 2, raia 4) mepoteza maisha kwenye vurugu Arusha
 
Habari wana Jf habari za kuaminika ni kwamba mpk sasa jumla ya watu sita (askari 2, raia 4) mepoteza maisha kwenye vurugu Arusha

habari za kuaminika huwa zina chanzo na uthibitisho! kwa mfano majina ya waliokufa na sehemu wanazoishi!
 
Tunahitaji tume huru kuchunguza mchakato mzima wa kumpata Meya Arusha, pamoja na vifo vya watanzania. atakayepatikana amehusika afikishwe katika vyombo vya sheria mara moja.
 
aiseee!! mcheza kuduku yupo ikulu tu anabinuka....kha!
 
We have Lost Four people.

Not only 4, hata police ni watu wetu (ila wapo kazini), Kwani hauna habari Slaa aliongoza Kambi zote za police katika kura za Urais
 
Back
Top Bottom