Ya Mulugo: Was Only a Slip of Tongue! [Aliteleza Ulimi tuu]

Mkuu Pasco
Jamaa alkuwa anahofu tu ya kuongea lugha ambayo hakuwa na raha nayo cha msingi ujumbe ulifika na wote waliokuwapo mkutanoni walijua Tanzania imetokana na muungano wa kitu fulani; muhimu ni ujumbe; na isitoshea nina uhakika wajumbe wa mkutano walikuwa na paper hivyo walipata fursa ya kupitia kilichosemwa na Bwana Mulugo.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hivi kaka kwa trend za siasa na hali halisi ya nchi unadhani huo mchemko ungefanywa na kiongozi wa CDM inge make headlines kama ilivyo sasa?

AshaDii dadangu mbona sasa unataka kututoa kwenye mada? hapa tunamzungumzia naibu waziri wa elimu wa JMT, mambo ya vyama vya siasa yanatoka wapi tena? au ndio njia mbadala ya kumnusuru Mulugo na mashambulizi? huyu anatumia kodi zetu kwenda kutuwakilisha kwenye mikutano ya kimataifa watanzania wote sasa akiboronga huko tuna kila haki ya kumshughulikia. Kama unamfahamu kiongozi yoyote ya Chadema aliyeboronga kwenye presentation unaweza kuanzisha thread tumjadili kuliko hivi unavyojaribu kutu divert toka katika hoja ya msingi inayomhusu Mulugo.

Na hata kama kuna viongozi wa Chadema wanaboronga kuongea kiingereza hiyo haiwezi kuwa excuse kwa naibu waziri Mulugo.
 
Last edited by a moderator:
Nadhani watetezi wa Naibu waziri Mulongo nao kuna jambo wanalikosea...!

Udhaifu wa huyu Mulongo siyo uwezo wake wa "kutamka Kiingereza" wala "kusoma maneno yaliyoandikwa kwa Kiingereza"...!

Udahifu wa Mulongo ni "kutumia ubongo wake kwa ufasaha wakati alipokuwa anasoma ile hotuba" - Kuna shida katika ubongo wake ambayo kwa kiswahili inatafsiriwa kama "ujuzi"...! Mtoto wa miaka mitatu (anayesoma chekechea) ukimpa kitabu asome anaweza kukigeuza "juu chini" na bado akaweza kutambua herufi "a e i o u"...!

Sasa inakuwaje Waziri anashindwa kusoma kilichoandikwa kwenye tarakirishi na kutamka neno lingine tofauti? Na juu ya yote hawezi kutambua kama amekosea au ameteleza ulimi?
 
Dada, majina ya Zanzibar na Zimbabwe ni ya lugha ya kigeni? Kusoma mwaka 1964 kwa lugha ya kiigereza inaweza ikawa tatizo kwa mtu wa lugha nyingine, lakini kusoma majina ya Zanzibar au Zimbabwe kwa mswahili sio tatizo mama!
 

Shukrani, nimezipokea kwa mikono miwili.... Tausi naomba niwe wazi kuwa siku ya kwanza kusikiliza hio clip my first reaction ilikuwa kucheka (utake usitake haiepukiki!); Ikafuata masikitiko, na nikajisemea kuwa bila pointing this out hata yeye Mulugo asingejua kachemka sababu alikuwa akiongea in a way ambayo inaonesha yeye aliona ni sawa. Hata hivyo la kuchanganya Zimbabwe na Zanzibar ni catastrophe na inatowa picha kuwa hata hio hotuba hakuipitia mapema sababu kama angeipitia asingeweza kosea something that straight forward!


Upande wa Critics ndio hilo ambalo limenifanya niliongelee.... Observe Tausi, majority ni criticism dhidi ya lugha. Ni wachache ambao wanaongelea namna ilivyo wazi kuwa inaonesha hayupo qualified kwa hio nafasi aliyopo na namna ambavyo ni mfano wa mawaziri ambao kazi yao ni walakini sana kama anawajibika. Kwa mtazamo wangu ile hotuba yake yoote inatowa picha ya nidhamu yake katika kazi (hayupo makini); Yupo chini ya nafasi aliyopo (kama naibu waziri wa Elimu, its un-excusable kutojuwa kiingereza); hana ufikiri, busara wala washauri (maana anazidi kuchemka anavyozidi kuli justfy); hivo at the end of the day tupo pamoja katika hoja yako kuhusiana naye.
 
AshaDii Nadhani tatizo la Waziri sio kutomudu kutumia lugha vema, ila tatizo kubwa hana uwezo wa kufanya presentation.. Na kwa mtu mwenye cheo kikubwa kama hicho ni aibu kubwa.
 
Last edited by a moderator:

hata mimi naona
 
i know the guy back in 2002,jamaa alkuwa mkuu wa shule pale southern highland mbeya ye ndo alikuwa mwiz namba moja wa mitihan kujipendekeza na usalit ndo vilimpa mashavu
 
Umepewa sh. Ngapi za kuja kumtetea hata aibu huna! Tatizo cc watanzania tunaficha sana udhaifu wetu na hatupendi kujikosoa na kusema ukweli, hainiingii akilini hata kidogo kwa mtu anaye mtetea labda awe ni chizi

Kwa mfano, huwezi ukaniambia ni kosa la kibinadamu wakati udhaifu upo kuanzia kusoma hadi kukosa kujiamini, yeye kama kiongozi hakuonyesha umakini na kujiamini, na kumbuka yeye ni mwalimu sifa kubwa za mwalimu ni kujiamini na kuwa makini.

Huwezi ukawa waziri/naibu waziri ukaongea yale halafu(pemba, zimbabwe na tanganyika) ushindwe hata kujikosoa halafu useme it was a slip of the tongue, kwani aliapa kwa jamhuri ipi?

lazima tukubali viongozi wetu wengine uwezo wao ni mdogo, kama tatizo ni lugha za kigeni watumie kiswahili na kuwepo na mkalimani.
 
Namna Waziri anavyotamka maneno ya kiingereza naona kama alifaa sana kushiriki kwenye lile tangazo la haki Elimu la THIPIUUUU na Pie chart , ni full comedian hakuna cha utetezi hapa, jaribu kufikiri kuwa waziri kama huyu ndio anaenda kutetea maslahi ya Nchi kimataifa sia atabaki anaunga mkono hoja tu hana skills za kujadili hoja kwa kiingereza
 
naomba kuweka angalizo kidogo, wakubwa wamezoea kuandaliwa kilakitu hotuba PPT nk. nimefanya kazi wizarani kwa miaka 9, na tatizo kama hili limejitokeza sana. Lakini mh mulugo hana uzoefu katika kuwasilisha mada mbele za wataalam jamani
 


Mwakalinga hapo namba 1 kuna mambo mengine sio lazima ya ainishwe... Inaweza kuwa haijaandikwa popote lakini hio ni common knowledge kuwa office nyingi nchini lugha ya Kiingereza ni mbadala kwa asiyejua Kiswahili hasa mjini.

Hio ya 3 naona unachukulia kila kitu literally, sijasema hayo in blue... Ila nimesema kuwa 'moja ya' (zingatia tofauti tafadhali..)

Hio paragraph ya mwisho nakubaliana na wewe, na hio inanifanya niwe na wasi wasi kama kweli umelielewa vema bandiko langu, sijamtetea Mulugo kwa lolote zaidi ya kusema kuwa yeye kukosea ni kosa la kibinadamu.

Pia niligusia kuwa kachemka na ilitakiwa awe wazi kusema haelewi lugha na pia nimegusia kuwa hayo ni matunda ya utendaji mbovu wa serkali kwa kuchagua kwa vigezo vya undugu na connections.
 
Hakuna excuse kwenye hili. Mfano ingekuwa ni mtihani wa Uraia,nchi ya Tanzania ilitokana na muungano wa nchi zipi na mwaka gani? Jibu liwe ilitokana na Tanganyika iliyoungana na visiwa vya Bahari ya Hindi vya Pemba na Zimbabwe mwaka 11964 wasahihishaji wangesema kalamu imeteleza? Kosa ni kosa tu hakuna cha utelezi. Viatu alivyovalishwa havimtoshi.
 
kuna mambo ambayo hata kwa kijana makini wa darasa la saba yanatakiwa yawe kwenye finger tips. Pemba na Zimbabwe hazina kawaida ya kutamkwa kwa pamoja (tafuta maandishi yoyote popote). Lakini vilevile labda kama waziri wetu haelewi tafasri ya kiswahili ya aliyokuwa akiyasoma kwa kiingereza. Kwa sababu hakuonekana hata kushtuka kwa lolote, na kama anaelewa tafasri ya aliyokuwa akiyasoma yalikuwa na maana gani kwa kiswahili basi huyo Waziri inawezekana alikunywa kidogo ili kutafuta confidence bandia kumbe kapitiliza. Kwa hivyo suala la kuteleza hapa halipo, LAZIMA KUNA TATIZO.

Lakini pia suala la elimu ya Waziri nalo si la kupuuza unless tuseme elimu haina maana yoyote katika nafasi za kisiasa. Ni kweli kwamba si kila mwenye elimu anaweza kuwa kiongozi, tunachopaswa ni kutafuta walio viongozi na ambao wameelimika kwa namna yoyote tuijuayo. Inawezekana ni mchapa kazi kama anavyotaka kutuaminisha mtoa hoja, lakini ni muhimu vile vile awe mzuri katika ku-communicate.
 
Ama kweli duniani kuna WATU na VIATU! Yaani GAFFE ya Mulugo kwamba Tanzania ni Muungano wa Viswa vya Pemba Zimbabwe na Tanganyika bado wewe unasema ni SLIP OF TONGUE! Tena VIATU hivyo ni vya Kichina.

Hata kama angesema kwamba Tanzania ni Muungano wa visiwa vya Pemba, Zanzibar na Tanganyika bado angekuwa amekosea achilia mbali hiyo Zimbabwe.

Watu huwa tunafanya rehersal kabla ya presentation, inaelekea yeye alitokea CASINO na kwenda kwenye podium bila kufanya rehersal. Nchi za wenzetu makini huyu angekuwa fired immediately baada ya kumaliza presentation kwani makosa aliyofanya ni kibao.
 
It's a human error. Kwangu sikuona issue kubwa, ingawa always natamani watumie lugha ya kwetu. Mbona viongozi wengi wa mataifa makubwa wanatumia lugha za kwao (sio kizungu)...! Ameshatoa ufafanuzi na kuomba radhi nadhani watanzania tuelewe hivyo pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…